Dr alphonce ndibalema wa udsm hatunae tena

Kwa kweli imeniuma sana, sema tu ndo hivyo Mungu ameamua kumchukua, nakumbuka kwenye lecture zake pale nkrumah hall. Ni mwalimu pekee ambaye zaidi ya miaka minne toka nimalize pale, mpaka leo nakumbuka somo lake kwa sababu alikuwa anatumia mifano halisi, yaani kwa kweli tulikuwa tunacheka sana.

R. I. P dr
 
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. KWA KWELI ALIKUWA AMEBOBEA KWENYE MASUALA YA Education management and Administration.
 
Napata faraja kuona aliwagusa na kupendwa na watu wengi sana. Marehemu Dr.Ndibalema alphonce ndiye baba yangu mzazi, na mpaka leo" i have not yet come to terms with the fact that he his gone. Baba alikuwa mtu mzuri kwa familia yake na jamii nzima yani wanafunzi wake majirani pamoja na jamaa zake wengine wote, Yeyote aliyemfahamu atakiri ya kwamba alikuwa ni mcheshi sana. Tutamkumbuka milele. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen.

Pia leo tarehe 9 march ndio tarehe yake ya kuzaliwa( Birthday)

Tulikupenda ila mungu alikupenda zaidi, jina la bwana lihimidiwe Amen.
 
Nakumbuka mifano yake ilivyokuwa inatupa the real thing/actual image ya topic anayofundisha.Nampenda,nitampenda daima.Umetangulia sisitunafuata.
 
The guy was very brilliant with his Philosophy 'OBUNTU'

Kitu kizuri ni kuwa watoto wake wote 90 % ni lecturer
 
Back
Top Bottom