DPP kuiadhibu CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DPP kuiadhibu CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pepombili, Mar 7, 2011.

 1. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amesema yupo sahihi katika utendaji wa kazi yake, kwa kuwa anafuata sheria na kwamba endapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kitapuuza barua yake ya onyo, sheria za nchi zitachukua mkondo wake ikiwamo kufunguliwa mashitaka na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

  Aidha, Tendwa amesema kamwe hatakitetea wala kukionea huruma chama chochote cha siasa, kikiwamo Chadema endapo kinakiuka sheria nchini.


  Alisema kwa kuwa amewaandikia barua Chadema ya onyo, anaamini watatekeleza sheria kwa kufuata taratibu zinavyotaka, lakini kama wakiamua kumpuuza kama walivyodai viongozi
  wake, sheria itachukua mkondo wake ikiwamo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuona ulazima wa kuwachukulia hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria au kwa maagizo ya Msajili huyo.

  Alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuliambia gazeti hili kuwa Msajili huyo amepoteza sifa ya kushika wadhifa huo kutokana na madai kuwa anakipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mambo mbalimbali, na kutofanyia kazi malalamiko anayopewa na Chadema.


  Katika maelezo yake, Dk. Slaa alilitaja tukio la Jeshi la Polisi mjini Arusha kuwalipulia mabomu ya machozi wafuasi wa chama hicho wakati wa kutawanya maandamano yao mjini Arusha mwanzoni mwa mwaka huu na kusema kuwa licha ya kumuandikia Tendwa barua kulalamikia suala hilo, hakuchukua hatua yoyote.


  Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Tendwa alisema kwa wadhifa wake, anawajibika kukataza au kuvionya vyama vinavyojihusisha na vitendo vya aina yoyote vyenye kuashiria kuchochea machafuko yenye kusababisha uvunjifu wa amani nchini bila kujali kama ni vya upinzani au chama tawala.


  Lakini Tendwa alisema hashangazwi na jambo lolote linalozungumzwa au litakalozungumzwa na Dk. Slaa, kwa madai kuwa anayafahamu matatizo yake ya kuropoka hovyo kutokana na kukosa busara.


  “Anachotaka Dk. Slaa ni kunichafua tu, lakini hilo halinisababishi nipindishe sheria katika utendaji wangu na kukipongeza Chadema pale kinapokosea.


  Nashukuru kwamba anafahamu vizuri kuwa ninawajibika kwa kufuata sheria na sina woga wala unafiki utakaonifanya nikipendelee chama kimoja na kuvikandamiza vingine kwa sababu za kushinikizwa, upendeleo binafsi au hofu ya kutukanwa kama anavyonifanyia yeye,” alieleza Tendwa.


  Akifafanua tukio la Arusha, alisema Jeshi la Polisi lilikuwa sahihi kujihami kwa mabomu yale na Chadema ilikuwa imekosea kisheria kulazimisha maandamano yale na hata kutaka kuvamia kituo cha polisi.


  “Tatizo la Dk. Slaa ni ufikiri mdogo na kukosa busara, hawakuwa na haki kwa lolote kule Arusha hivyo alipaswa anyamaze na kukishauri chama chake kufuata sheria.


  Kila mtu aliona kilichotokea, sasa alitaka mimi nichukue hatua gani dhidi ya Dola? Sana sana walistahili onyo kwa kutishia amani ya nchi na sio kutetewa,” alieleza Msajili huyo.


  Kwa mujibu wa Tendwa, Padri huyo wa zamani wa Kanisa Katoliki, anapaswa kutulia na kujiuliza ni vipi atarudi kwenye mstari ulionyooka baada ya kuharibu kwa Mungu na wala sio kusimama mbele kuleta vurugu nchini kwa kutumia chama cha siasa.


  “Unajua alisoma sana dini hata akaitwa daktari, sasa huyu nilitegemea angekuwa kiongozi wa amani nchini na mfano wa busara kwa wengine, lakini nasikitika kuwa anakuwa mchochezi wa vurugu kwa kupitia chama chake cha siasa,” alidai Tendwa na kuongeza:


  “Simshangai Dk. Slaa kwa kuwa nauelewa ufikiri wake finyu, aliweza kuharibu kwa Mungu, sembuse kwenye siasa?


  Sasa kama ninalijua hilo kwa nini niendekeze vitendo viovu vinavyoweza kuvuruga amani nchini? “Nitaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa chama chochote kitakachokiuka sheria na wala sitabagua.


  Sasa cha msingi akubali kufuata sheria ili mambo yaishe, vinginevyo hata kwa shetani nako kutamshinda.”


  Akimaananisha katika siasa. Katika hatua nyingine, mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Chrisant Mzindakaya amekitaka chama hicho kujibu hoja za Chadema kwa kuwatumia viongozi wa mikoa ambayo Chadema wanafanya mikutano.


  Aidha, alihoji iweje Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kuwa kimya muda wote kama iko likizo na kuiachia Serikali kazi ya kisiasa hasa katika kipindi hiki.


  Mzindakaya aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa hali inayoendelea sasa ni mchezo wa kisiasa ambao CCM wanatakiwa kujibu hoja katika mikoa ambayo Chadema wanapita na kutoa hoja zao za uchochezi.


  Alisema pia NEC ya CCM inatakiwa kukutana na kutoa tamko kwani chama cha kisiasa kikubwa na chenye sifa kama CCM hakiwezi kuacha Chadema ikaendelee kuvuruga nchi.


  “Viongozi wa CCM katika mikoa ambayo Chadema wanapita na kutoa hoja zao, wajibu kwa kuponda hoja hizo ili wananchi waelewe hali halisi na siyo kumsubiri Waziri Mkuu au Rais kujibu hoja,” alisema Mzindakaya.


  Mwanasiasa huyo aliyekuwa mbunge kwa takribani miaka 40 kabla ya kustaafu mwaka jana, alisema wakati huu ndipo kazi ya kisiasa inatakiwa ifanyike kwa nguvu katika kuelimisha wananchi nini Chadema wanachofanya na siyo kunyamanza kimya na chama hicho cha upinzani kuonekana wanazungumza ukweli.


  Ameitaka Chadema kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo na siyo kuwagawa wananchi kwani kwa kuwa na wabunge wengi, walitakiwa kushirikiana na Serikali kujenga nchi wakianzia katika majimbo yao.


  Alisema uchaguzi umeshafanyika na Serikali imepatikana kinachotakiwa sasa ni kuhangaikia maendeleo kwa kutumia viongozi makini kutoka vyama vya siasa na siyo kuwagawa wananchi.


  Chanzo: Habari leo
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ufundi wa kuongea maneno wa Tendwa si ishu..tulicho na uhakika nacho ni kuwa tumemjua mbaya wetu, na hatubadiliki!
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Jamani< sasa sisi tutegemee nini kutoka kwa mtu ambae "baada ya kuharibu kwa Mungu" anataka kuja kutuharibia na sisi ya duniani!
   
 4. l

  lyimoc Senior Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asisubutu mtu yeyote kufanya kosa ambalo litaigarimu taifa letu huyo tendwa na dpp ni vibaraka ccm .wanafanya kazi kwa kufuata maagizo ya wakubwa wao.miaka 50 inawatosha ccm sasa basi out
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  He Tendwa, mbona mashambulizi makali kiasi kicho kwa nafsi ya Dr Slaa badala ya kuzungumzia KATIBU MKUU wa chama kiitwacho CHADEMA??

  Hivi mpaka hapo kumkashifu koote huko bado ni ndani ya jukumu lako la kusimamia vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba au sasa ni jitihada binafsi kama kada wa CCM kujaribu kumdhibiti Mtanzania aitwae Dr Slaa?? Je, hapa unapojiridhisha nafsi kumwaga ugali sisi vijana tutakapoaanza kumwaga mboga nako bado utaendelea kuongea hivyo??

  Busara, nidhamu ya kazi na ufanisi kama refarii na ianze kukukaa japo kwa mara ya kwanza ungali bado upo katika ofisi yetu hiyo ya umma!!!
   
 6. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kama anadai kuwa hapendelei vyama vya siasa... mbona aliwahi kusema muda wa kampeni umesogezwa mpaka saa 1 kwenye mikoa ambayo machweo yanachelewa wakati sio kweli???

  Eti hawa ndio washauli wa raisi... kweli hii nchi imekosa kwa mungu... maana naona anazeeka vibaya, MUACHE TUIONE HIYO SHERIA ANAYOSEMA ITAFUATA MK*ND*, ila ajue kila neno analolisema kuhusu CHADEMA anaongeza mwanachama mmoja kwa CHADEMA.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hebu tafuta kwanza jibu la kwamba je wale walioharibu msikitini kwa fuska wa ukuzidisha VIDUMU mitaani zaidi ya nafasi nne rasmi Muislamu kuoa wao umewaweka wapi au kuwategemeaje, na huku wakiendekeza ubadhirifu kila kona wao mnawategemea nini hasa duniani kama si ahera??
   
 8. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  hivi mtu yoyote mwenye busara akimsikiliza Tendwa akiongea anaweza kumtofautisha na Makamba au kada yoyote wa CCM. sikutarajia regulator wa vyama vya siasa kum-attack in person Dk. Slaa. Kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni! mhh Tendwa amekuwa too low!
   
 9. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa cha msingi akubali kufuata sheria ili mambo yaishe, vinginevyo hata kwa shetani nako kutamshinda.”
  Akimaananisha katika siasa. Kumbe tendwa ni msajiri wa vyama vya mashetani.
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wanaoongea kwa kutumia makalio utawajua tu, wewe na Tendwa wote hamna busara na historia itawahukumu na mtamkumbuka Slaa siku hiyo, wewe hujui hali mbaya ya maisha hata wajomba zako kule kijijini inawakuta au kwa sababu baba ako fisadi au sister ako demu wa mkwere, acheni ushabiki wa kishamba.
   
 11. P

  Popompo JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  heshima mbele mkuu!umeongea yote ngoja nikakugongee thenkx!tehe tehe tendwa!aibu ikunamate mwenye ufinyu wa kufikiria ni wewe au ni dr?
   
 12. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Unajua huyo Tendwa sikujua kama ni mbumbu kiasi hiki nilitegema angèfafanua ni sheria gani CDM wamevunja lakn naye ameishia tena kwenye matusi na udini kweli amepoteza sifa ya kuwa msajili
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyo aliyeshika nchi unahakika hajaharibu kwa mungu wako?
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu Tendwa ni MSIAJIRI WA VYAMA VYA SIASA
   
 15. baina

  baina JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tendwa ni maku.
   
 16. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Chadema imarisheni ngome zenu za ulinzi na ushambuliaji, endeleeni kuwaeleza wananchi ukweli juu ya unyonyaji wa serikali ya CCM. Msitishike na maneno ya Tendwa.
   
 17. k

  kayumba JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35


  Kwa haya maneno ya msajili, kazi ipo!

  Hivi msajili uwa anashughulikia vyama au wanachama? Hapa ni kama nguvu zimeelekezwa kwa mwanachama "Dr. Slaa"!

  TAFAKARI!
   
 18. C

  Chaldmhola Member

  #18
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mfa maji haachi kutapa-tapa, CCM wameshikwa pabaya, watafanya kila linalowezekana kudhibiti vugu-vugu hili la mabadiliko linaloongozwa na CDM. Hakika hawataweza! Mungu Ibariki TZ, Mungu Ibariki CDM!!!
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  jamani eeenh naona sasa hawa akina tendwa hawajui wako ktk public service na si usultani au ufalme, huyu mzee busara zimekpitia kando nadhani anataka kuleta ya kivuitu yule wa kenya. ccm mnataka kuleta vurugu na historia itawahukumu kwa hilo. jk aliposema kuandamana ni haki ya kila raia ana maanisha nini? au bado analeta katiba za kijamaa? hamaanishi anachosema? hatufumbwi mdomo na mtu tendwa wala ccm haina uwezo huo hii ni nchi ya wananchi wote na si ccm peke yakewewe babu tendwaa
   
 20. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Mie nadhani CHADEMA watangaze kutomtambua Tendwa. Maana ameonyesha kuwa kada wa CCM. Ofisi yake sio ofisi huru.

  Nawaonya viongozi wa CCM wasizidi kuisukuma CHADEMA. Waogope kwamba inaweza kuamua kuitisha maandamano ya kudai UHURU wa kweli. UHURU chini ya katiba mpya. CHADEMA wakiitisha maandamano makubwa Dar ya wananchi kuitaka serikali ijiuzulu, yatafanikiwa. Baada ya siku mbili au atau hata FFU wenyewe watakataa kushambulia ndugu zao.

  Ni vema vyombo vya kikatiba kushirikiana na CHADEMA kudhibiti vurugu wakati wa maandamano. Kufanya uadui na CHADEMA hakutasaidia.

  Kama DPP ataendelea kukubali kuwa bootlicker wa CCM, naye asitambuliwe. AMANI haidumishwi kwa kukandamiza upinzani.
   
Loading...