MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amesema yupo sahihi katika utendaji wa kazi yake, kwa kuwa anafuata sheria na kwamba endapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kitapuuza barua yake ya onyo, sheria za nchi zitachukua mkondo wake ikiwamo kufunguliwa mashitaka na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).
Aidha, Tendwa amesema kamwe hatakitetea wala kukionea huruma chama chochote cha siasa, kikiwamo Chadema endapo kinakiuka sheria nchini.
Alisema kwa kuwa amewaandikia barua Chadema ya onyo, anaamini watatekeleza sheria kwa kufuata taratibu zinavyotaka, lakini kama wakiamua kumpuuza kama walivyodai viongozi wake, sheria itachukua mkondo wake ikiwamo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuona ulazima wa kuwachukulia hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria au kwa maagizo ya Msajili huyo.
Alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuliambia gazeti hili kuwa Msajili huyo amepoteza sifa ya kushika wadhifa huo kutokana na madai kuwa anakipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mambo mbalimbali, na kutofanyia kazi malalamiko anayopewa na Chadema.
Katika maelezo yake, Dk. Slaa alilitaja tukio la Jeshi la Polisi mjini Arusha kuwalipulia mabomu ya machozi wafuasi wa chama hicho wakati wa kutawanya maandamano yao mjini Arusha mwanzoni mwa mwaka huu na kusema kuwa licha ya kumuandikia Tendwa barua kulalamikia suala hilo, hakuchukua hatua yoyote.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Tendwa alisema kwa wadhifa wake, anawajibika kukataza au kuvionya vyama vinavyojihusisha na vitendo vya aina yoyote vyenye kuashiria kuchochea machafuko yenye kusababisha uvunjifu wa amani nchini bila kujali kama ni vya upinzani au chama tawala.
Lakini Tendwa alisema hashangazwi na jambo lolote linalozungumzwa au litakalozungumzwa na Dk. Slaa, kwa madai kuwa anayafahamu matatizo yake ya kuropoka hovyo kutokana na kukosa busara.
"Anachotaka Dk. Slaa ni kunichafua tu, lakini hilo halinisababishi nipindishe sheria katika utendaji wangu na kukipongeza Chadema pale kinapokosea.
Nashukuru kwamba anafahamu vizuri kuwa ninawajibika kwa kufuata sheria na sina woga wala unafiki utakaonifanya nikipendelee chama kimoja na kuvikandamiza vingine kwa sababu za kushinikizwa, upendeleo binafsi au hofu ya kutukanwa kama anavyonifanyia yeye," alieleza Tendwa.
Akifafanua tukio la Arusha, alisema Jeshi la Polisi lilikuwa sahihi kujihami kwa mabomu yale na Chadema ilikuwa imekosea kisheria kulazimisha maandamano yale na hata kutaka kuvamia kituo cha polisi.
"Tatizo la Dk. Slaa ni ufikiri mdogo na kukosa busara, hawakuwa na haki kwa lolote kule Arusha hivyo alipaswa anyamaze na kukishauri chama chake kufuata sheria.
Kila mtu aliona kilichotokea, sasa alitaka mimi nichukue hatua gani dhidi ya Dola? Sana sana walistahili onyo kwa kutishia amani ya nchi na sio kutetewa," alieleza Msajili huyo.
Kwa mujibu wa Tendwa, Padri huyo wa zamani wa Kanisa Katoliki, anapaswa kutulia na kujiuliza ni vipi atarudi kwenye mstari ulionyooka baada ya kuharibu kwa Mungu na wala sio kusimama mbele kuleta vurugu nchini kwa kutumia chama cha siasa.
"Unajua alisoma sana dini hata akaitwa daktari, sasa huyu nilitegemea angekuwa kiongozi wa amani nchini na mfano wa busara kwa wengine, lakini nasikitika kuwa anakuwa mchochezi wa vurugu kwa kupitia chama chake cha siasa," alidai Tendwa na kuongeza:
"Simshangai Dk. Slaa kwa kuwa nauelewa ufikiri wake finyu, aliweza kuharibu kwa Mungu, sembuse kwenye siasa?
Sasa kama ninalijua hilo kwa nini niendekeze vitendo viovu vinavyoweza kuvuruga amani nchini? "Nitaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa chama chochote kitakachokiuka sheria na wala sitabagua.
Sasa cha msingi akubali kufuata sheria ili mambo yaishe, vinginevyo hata kwa shetani nako kutamshinda."
Akimaananisha katika siasa. Katika hatua nyingine, mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Chrisant Mzindakaya amekitaka chama hicho kujibu hoja za Chadema kwa kuwatumia viongozi wa mikoa ambayo Chadema wanafanya mikutano.
Aidha, alihoji iweje Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kuwa kimya muda wote kama iko likizo na kuiachia Serikali kazi ya kisiasa hasa katika kipindi hiki.
Mzindakaya aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa hali inayoendelea sasa ni mchezo wa kisiasa ambao CCM wanatakiwa kujibu hoja katika mikoa ambayo Chadema wanapita na kutoa hoja zao za uchochezi.
Alisema pia NEC ya CCM inatakiwa kukutana na kutoa tamko kwani chama cha kisiasa kikubwa na chenye sifa kama CCM hakiwezi kuacha Chadema ikaendelee kuvuruga nchi.
"Viongozi wa CCM katika mikoa ambayo Chadema wanapita na kutoa hoja zao, wajibu kwa kuponda hoja hizo ili wananchi waelewe hali halisi na siyo kumsubiri Waziri Mkuu au Rais kujibu hoja," alisema Mzindakaya.
Mwanasiasa huyo aliyekuwa mbunge kwa takribani miaka 40 kabla ya kustaafu mwaka jana, alisema wakati huu ndipo kazi ya kisiasa inatakiwa ifanyike kwa nguvu katika kuelimisha wananchi nini Chadema wanachofanya na siyo kunyamanza kimya na chama hicho cha upinzani kuonekana wanazungumza ukweli.
Ameitaka Chadema kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo na siyo kuwagawa wananchi kwani kwa kuwa na wabunge wengi, walitakiwa kushirikiana na Serikali kujenga nchi wakianzia katika majimbo yao.
Alisema uchaguzi umeshafanyika na Serikali imepatikana kinachotakiwa sasa ni kuhangaikia maendeleo kwa kutumia viongozi makini kutoka vyama vya siasa na siyo kuwagawa wananchi.
Chanzo: Habari leo
Jamani< sasa sisi tutegemee nini kutoka kwa mtu ambae "baada ya kuharibu kwa Mungu" anataka kuja kutuharibia na sisi ya duniani!
Jamani< sasa sisi tutegemee nini kutoka kwa mtu ambae "baada ya kuharibu kwa Mungu" anataka kuja kutuharibia na sisi ya duniani!
niliwah ckia huyu Tendwa ni sh....ga, hv ni kwel au? Maneno yke yananfnya nianze kuamin. Kwel Tendwa umetendwa knyume na ma.....le! Hacra za nn baba? Taratb basi shost.