BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
DPP atoa kibali, Kikwete apata kigugumizi
Mwandishi Wetu Septemba 24, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
Ilikuwa wakamatwe mwezi huu, sasa Oktoba
Polisi, TAKUKURU nao wavutana
PAMOJA na kukamilika kwa uchunguzi na kuwapo kwa ushahidi wa kutosha, Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imepata kigugumizi katika kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wakubwa wa ufisadi, baadhi yao wakiwa bado ndani ya nafasi za juu za uongozi serikalini, RAIA MWEMA limefahamishwa.
Vyanzo mbalimbali vya habari vya kuaminika ndani ya serikali vimeeleza kwamba vyombo vya dola, ikiwamo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la Polisi, vimekuwa katika shinikizo kubwa la kutowafikisha mahakamani watuhumiwa hao; huku kukiwa na mvutano wa wazi ndani ya vyombo hivyo.
Kwa mujibu wa habari hizo, kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi, alikwishatoa kibali cha kushitaki angalau watuhumiwa watano wakubwa wakati watuhumiwa wengine kesi zao zikiwa katika hatua za mwisho, lakini TAKUKURU na Polisi wamepata kigugumizi cha kuziwasilisha kesi hizo mahakamani.
Ofisa Mwandamizi wa serikali amelithibitishia Raia Mwema ya kuwa tayari angalao watuhumiwa watano walikuwa wafikishwe mahakamani mwezi huu lakini kukatokea "shinikizo" la kutaka kesi hizo zicheleweshwe angalao hadi mwezi ujao.
"Tayari jamaa walikuwa wamejiandaa kuwakamata watu watano muhimu, kati yao wanasiasa wawili maarufu na mtendaji mmoja wa juu serikalini, lakini wakaambiwa wasubiri hadi Oktoba kutokana na sababu maalumu za kiutendaji," alisema ofisa mmoja mwandamizi wa serikali ambaye habari hizo zilimfikia hivi karibuni.
Hata hivyo, ofisa huyo ametetea uamuzi huo kwa kusema kwamba kila serikali ina utaratibu wake wa kufanya kazi na kwamba suala linalohusu haki ya mtu linapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa, kauli ambayo ilitolewa pia na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia Bunge hivi karibuni.
Hivi karibuni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Utawala Bora, Sophia Simba, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hakuna mtuhumiwa wa ufisadi ambaye anaweza kukwepa mkono wa sheria, na kwamba hatima yao inashughulikiwa.
Waziri Simba hakuweza kuzungumzia kigugumizi hicho jana baada ya kueleza kwamba alikuwa katika kikao ambacho hawezi kuzungumza na Raia Mwema, lakini habari zinasema kwamba serikali inaangalia mazingira na athari ya kuwashitaki watuhumiwa hao ambao baadhi wana mahusiano na wanasiasa wenye nguvu nchini.
Pamoja na kuwa kesi zinazosubiriwa na wengi ni zile zinazowahusu watuhumiwa walioiba fedha kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), iliyokuwa ikiratibiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuna kesi nyingine ambazo uchunguzi wake umekamilika na hata Serikali kupitia vyombo vyake imejigamba kuwa uchunguzi wake umekamilika.
Rais Kikwete amenukuliwa mara kadhaa akisema kwamba Serikali imo katika hatua za mwisho za kuzifikisha mahakamani kesi kubwa zinazohusiana na tuhuma za ufisadi, lakini hadi sasa hakuna kesi yoyote kubwa iliyofunguliwa.
Mbali ya Rais, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosea, amenukuliwa mara kadhaa akisema kwamba mwaka huu pekee wamejiwekea malengo ya kufikisha mahakamani kesi kumi kubwa za rushwa, na kwamba kati ya hizo kesi sita zilikuwa zimekamilika kufanyiwa kazi.
DPP Feleshi, amewahi kunukuliwa akithibitisha kutoa kibali cha mashitaka kwa kesi mbili kubwa, kabla ya kukataa kuzungumzia tena suala la kesi alizozitolea kibali ikiwa ni miezi kadhaa kupita tokea atoe kauli ya kutoa kibali cha mashitaka.
Pamoja na Serikali, TAKUKURU na DPP kutotaja kesi hizo hadharani, imethibitishwa kwamba kesi zilizokuwa katika hatua za mwisho kufunguliwa ni pamoja na uchunguzi kuhusiana na tuhuma za rushwa katika kampuni ya uhakiki wa dhahabu ya Alex Stewarts ya Marekani, ambayo iliingizwa na Serikali kuhakiki thamani halisi ya dhahabu inayozalishwa nchini na kuuzwa nje.
Kesi nyingine ni ile inayohusu miradi ya dhahabu iliyohusisha makampuni ya Meremeta Limited, Tangold Limited, Deep Green na Mwananchi Gold. Kesi nyingine ni kuhusiana na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama, uchunguzi kuhusu maghorofa pacha ya BoT, mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira na ununuzi wa rada ya kijeshi kutoka kampuni ya BAe Systems ya Uingereza.
Hata hivyo, kuna taarifa za ongezeko la kesi ya mradi tata wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni ya Richmond Development LLC ambayo sasa imetangazwa kufutiwa usajili na Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni (BRELA), na sasa uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA.
"Kaka, hakuna wa kubaki katika hizo kesi. Atakayepona ni yule msafi tu, na ndio maana unaona watu wanafanya kazi kwa uangalifu mkubwa ili kesi zikifikishwa mahakamani hakuna wa kulalamika kwamba anaonewa. Rais ameagiza kusiwe na mwanya wa mtu kuilalamikia serikali wala mtu kujigamba kwamba amependelewa," alisema ofisa mwingine wa serikali.
Baada ya Serikali kuonyesha nia ya kukusanya kwanza fedha badala ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa fedha za EPA, wananchi mbalimbali walianza kulalamika wakielezea kuwapo kwa ubaguzi katika kushughulikia uhalifu; kauli ambayo iliigusa serikali na kutolewa ufafanuzi na Waziri Simba.
"Timu ndiyo ita-establish kesi. Kama ni kwenda mahakamani watakwenda, sheria itachukua mkondo wake, kusikiliza pande zote ndio utawala bora. Mimi sijajua kama hapo baadaye itakuwaje. Naomba tusivuke daraja kabla hatujafika, tuiachie timu ifanye kazi yake, maana bado inaendelea, si unajua iliomba muda?, alisema Waziri Simba alipozungumza na gazeti la Nipashe hivi karibuni.
Wakati hayo yakiendelea, Tanzania kama taifa imekuwa ikihakikiwa na jumuiya za kimataifa, chini ya mwavuli wa wa Umoja wa Mataifa, kuhusiana na jinsi inavyoshughulikia tatizo la rushwa nchini, kazi iliyokuwa ikifanywa na wataalamu kutoka Uingereza na Uholanzi waliotembelea Tanzania hivi karibuni.
Wataalamu hao walikutana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya rushwa, ikiwamo TAKUKURU, waandishi wa habari, asasi zisizo za kiserikali na watendaji wakuu na wa kati wa serikali wanaohusika katika mchakato wa kupambana na rushwa.
Serikali kwa upande wake imekuwa ikijivunia matukio ya hivi karibuni katika mapambano dhidi ya rushwa ikielezea kwamba hali ilivyo sasa ni matokeo ya uamuzi wa Serikali kutoa uhuru wa kutosha kwa vyombo vya habari na wanasiasa katika kukabiliana na tuhuma za rushwa na ufisadi.
Miongoni mwa mambo ambayo Serikali imetumia kama mfano ni pamoja na Rais kukubali kujiuzulu kwa mawaziri wake wanne, akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa. Wengine ni waliokuwa mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, pamoja na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge. Lowassa na wenzake walihusishwa na mradi tata wa Richmond wakati Chenge anachunguzwa kuhusika na rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi.
Mbali ya kujiuzulu kwa mawaziri hao, Serikali imejigamba kwamba hata mabadiliko makubwa ndani ya BoT, yametokana na dhamira ya kisiasa ya serikali ya Kikwete katika kupambana na ufisadi, na kwamba vyombo vya habari na Bunge vimekuwa vikipewa uhuru wa kutosha na Serikali bila kuingiliwa hata pale "vinapoteleza."
Pamoja na kujigamba huko, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Kiongozi Mstaafu, Amiri Manento, alinukuliwa akishangazwa na hatua ya Serikali kusita kuwafikisha mahakamani watuhumiwa mbalimbali wa ufisadi, wakiwamo wale wa wizi wa fedha za EPA.
Uamuzi wa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA kwa sasa bado uko mikononi mwa Timu ya Rais ya Kuchunguza wizi huo, inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na wenzake - Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah.
Timu hiyo imeomba na kukubaliwa na Rais kuongezewa muda hadi Oktoba 31, kipindi ambacho wamedai kwamba watakuwa wamekamilisha kukusanya fedha na ushahidi wa ndani na nje ya nchi.