DPP apingwa sakata la Ulimboka

DPP apingwa sakata la Ulimboka

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,342
DPP apingwa sakata la Ulimboka
• Wanasheria wadai ameungana na polisi kuficha uovu

na Abdallah Khamis
Tanzania Daima

MADAI ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Eliezer Feleshi, kuwa Dk. Steven Ulimboka ameficha ushahidi wa kutekwa kwake, yamepingwa vikali na wanasheria wakisema anaficha uovu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Mwema, DPP alisema kuwa polisi wameshindwa kuwakamata watekaji na watesaji wa Dk. Ulimboka kutokana na kutopata ushirikiano wake.

Dk. Ulimboka ambaye ni Mweyekiti wa Jumuia ya Madaktari, alitekwa na kuteswa vibaya kisha kutupwa katika msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamikia Juni 26, 2012.
Wakizungumza na Tanzania Daima kuhusu utetezi wa DPP, wanasheria hao Mabere Marando, Profesa Abdallah Safari na Method Kimomogoro walisema kuwa amedhalilisha taaluma ya sheria.

Marando alisema DPP amejiunga na jeshi la polisi kuficha uovu unaotokea nchini kwa kile alichoeleza kwamba jukumu la polisi ni kupeleleza tukio kabla ya kumfikiria muathirika awe sehemu ya taarifa ya upelelezi huo.
Alisema kwa kauli ya DPP ni wazi kuwa kama Dk. Ulimboka angepoteza maisha katika tukio hilo, basi wapelelezi wasingekuwa na kazi ya kufanya.

“Hii kwangu ni kauli ya ajabu na sijawahi kufikiria mtu kama Feleshi anaweza kuungana na polisi kuficha ukweli. Jukumu lake ni kutoa maelekezo ya vitu vinavyotakiwa kwa ajili ya kesi, siyo naye anaanza kulalamika!” alisema.
Kuhusu polisi, Marando alisema kwa sasa hawafanyi kazi ya kitaalamu zaidi ya kutegemea kumkamata mhalifu na kisha kumtesa ili atoe maelezo wanayoyataka.

Alisema hali hiyo ndiyo imesababisha takriban asilimia sabini ya kesi zilizo mahakamani kuwa na maelezo ya ‘onyo’ badala ya kufanyiwa kazi kitaalam.
Marando aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo mtuhumiwa anapokuwa na mwanasheria mzuri mara nyingi anashinda kesi na serikali kubaki kuaibika na kutoaminika mbele ya wananchi.
Alisisitiza kuwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, alipaswa kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kupata ushahidi wa uhakika.

“Watuambie walifanya nini kumtafuta Dk. Ulimboka, si wana wachunguzi? Kwa nini wasiende nyumbani kwake wakapate huo ushahidi wanaoona haukutolewa?” alihoji.

Marando alisema Dk. Ulimboka alishamtaja ofisa wa Ikulu aliyeshiriki katika kumteka, hivyo lilibaki jukumu la polisi kumkamata mtuhumiwa aliyetajwa na kufanya gwaride la utambuzi.
Alisema hali hiyo ya kumtaka Dk. Ulimboka aende katika ofisi za polisi kutoa maelezo mengine huenda ikawa ni mtego mwingine wa kumdhuru baada ya kumtaja mtu wa serikali anayehusika na kadhia hiyo.

Naye Prof. Abdallah Safari alifafanua kuwa kisheria suala la kutafuta ushahidi ni la serikali yenyewe.
Alisema kuwa tayari Dk. Ulimboka alishawaonyesha njia na kwamba serikali ilipaswa kuanzia alipoishia kwa kuwakamata wote waliotajwa ili kupata ushahidi zaidi.

Mwanasheria mwingine kutoka jijini Arusha, Method Kimomogoro, alisema kuwa Dk.Ulimboka alishatoa maelezo yenye kujitosheleza juu ya mhusika aliyemteka.
Alisema DPP Feleshi ni wazi kwa sasa anachagua matukio ya kufanyiwa kazi na kwamba watu wenye mawazo huru wanapopata tatizo ofisi yake haioni haja ya kushughulika nao.

Alitolea mfano mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Usa River mkoani Arusha na mwanachama mwingine Mbwana Masudi aliyeuawa Igunga mkoani Tabora.
Pia alitaja mauaji ya kijana Ally Nzona wa mkoani Morogoro aliyepigwa risasi na polisi kwenye maandamanao ya CHADEMA kuwa ni uthibitisho tosha wa namna ofisi ya DPP na jeshi la polisi wanavyofanya kazi kwa ubabaishaji.

Kimomogoro alisema jambo la kusikitisha ni kuona watu wenye mawazo huru ya kuikosoa serikali wanavyokamatwa makundi makundi kama wahalifu kwa wakati mmoja.
Alisema inashangaza kuona kundi la askari lililomzunguka Mwangosi kabla ya kuuawa kwake likiwa halijaguswa hadi leo.

Aliongeza kuwa DPP kwa nafasi yake kwa umma alipaswa aonyeshe dhamira kutenda kitaalamu na si kama mwanasiasa jambo alilosema si jema kwa mustakabali wa taifa.
Wakati wanasheria hao wakikosoa kauli ya DPP, jeshi la polisi limeendelea kushikwa na kigugumizi kueleza kama lilishawahi kuwahoji watu waliotajwa na Dk.Ulimboka.
Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, alipoulizwa jana, alitaka aandikiwe maelezo katika karatasi na yafikishwe ofisini kwake.
“Kwa sasa nashughulikia kutoa taarifa ya Sheikh Ponda, hayo maswali yako yaandae kwa maandishi kisha utaniletea hapa ofisini,” alisema Senso.

DPP mzushi tu huyo,analipwa pesa nyingi kwa kodi zetu halafu walipa kodi hao hawatendei haki,nae amejiunga kwenye mpango wa kutotenda haki kama kilivyo chama chake,nasema chama chake maana hakika ni CCM damu huyo,maana kama angelikuwa ni mpenda haki ni vema akaachia ngazi kama anaona anafanyishwa kazi kwa mashinikizo ambayo yanampelekea kutokutenda haki.kimsingi DPP nayo imekuwa DPPCCM tu,nae amekuwa mzushi ile mbaya
 
Hii njemba na polisi wote wameshakuwa ni vitengo vya CCM. Hili ni jambo hatari sana kwa nchi. Matokeo yake ndiyo kama hayo ya kubambikia kesi watu (Lwakatare na Kileo) ambazo hakuna ushahidi hata chembe wa kuwatia wahusika hatiani. Kuzipotezea kesi za Mwangosi na Dr Ulimboka n.k.

DPP mzushi tu huyo,analipwa pesa nyingi kwa kodi zetu halafu walipa kodi hao hawatendei haki,nae amejiunga kwenye mpango wa kutotenda haki kama kilivyo chama chake,nasema chama chake maana hakika ni CCM damu huyo,maana kama angelikuwa ni mpenda haki ni vema akaachia ngazi kama anaona anafanyishwa kazi kwa mashinikizo ambayo yanampelekea kutokutenda haki.kimsingi DPP nayo imekuwa DPPCCM tu,nae amekuwa mzushi ile mbaya
 
Subirini wakitolewa pale watasema yote!sasa hivi wanatekeleza ilani ya CCM!na ilani ndogo za Riz1!wabishe wafe njaa kijiweni!?wamuulize Dr Hosea anavyolia njaa sasa hivi!ameambiwa akiona mambo hayaendi ajiuzulu!anakoma na nini?
 
another silly season...!! yani hiyo nchi yenu ni upuuzi kila mahali, upuuzi upuuzi tu, yaani polisi hawana namna nyingine ya kupata ushahidi zaidi ya kumuhoji ulimboka?? namba za simu si walipewa na kubenea?? yani kubenea kapata hadi majina ya hao wahusika, polisi wameshindwa!!!! jitu kama feleshi au mwema ukiwaita stupid unakosea?? stupid!
 
Mkuu hii nchi yetu tumeifanya wenyewe kuwa ya kipuuzi kwasababu sisi ni wapuuzi... tusingekua wapuuzi, huu upuuzi unaoendelea sasa usingekuwepo

Kuna wakati unajiuliza nini faida ya elimu endapo waliosomeshwa kulipa hadhi ya cnhi wana tabia za kijinga kuliko wajinga wengine
 
another silly season...!! yani hiyo nchi yenu ni upuuzi kila mahali, upuuzi upuuzi tu, yaani polisi hawana namna nyingine ya kupata ushahidi zaidi ya kumuhoji ulimboka?? namba za simu si walipewa na kubenea?? yani kubenea kapata hadi majina ya hao wahusika, polisi wameshindwa!!!! jitu kama feleshi au mwema ukiwaita stupid unakosea?? stupid!

Huo utetezi kama kweli ulitoka kwa DPP basi hayo ni majanga...kwani tayari walishakuwa na tip za mwanahalisi lakini badala yakutumia maelezo ya mwanahalisi ili ku konect dot na maelezo y Ulimboka ambaye akiwa na akilitimamu amethibitisha kwamba alikwapuliwa alipokuwa na Afisa usalama wa Ikulu.... .Any way kwa level ya ofisi yake nadhani hili cha mtoto hebu tujiulize anapofuta Kesi ya Idd Simba wakati huo huo anakata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama kwa kesi ya Kipuuzi ya LWAKATARE ambayo hata hawajawahi kumuhoji Mwenye ushahidi wa Kukubalika hata Mbinguni?!

Ofisi hii ifutwe haina tija tubaki na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama ilivyokuwa zamani nadhani ofisi ya DPP nimoja ya Ofisi chache ambazo performance yake ni extremly poor.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chadema ni wauwaji, wamemtesa kibanda, wamemmwagia tindikali mussa tesha, walikuwa wanataka kumtesa mhariri msaki, watashindwaje kumteka na kumtesa ulimboka???
 
Machadema laana tupu, wanazungumziaje roho za wagonjwa zilizopotea kwa kukosa matibabu kwa sababu ya mgomo wa ulimboka kwa msaada wa chadema
 
DPP Feleshi Ni janga la kidunia, anafanyakazi kama house boy WA Mwigulu Nchemba
 
DPP apingwa sakata la Ulimboka
• Wanasheria wadai ameungana na polisi kuficha uovu

na Abdallah Khamis
Tanzania Daima

MADAI ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Eliezer Feleshi, kuwa Dk. Steven Ulimboka ameficha ushahidi wa kutekwa kwake, yamepingwa vikali na wanasheria wakisema anaficha uovu.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Mwema, DPP alisema kuwa polisi wameshindwa kuwakamata watekaji na watesaji wa Dk. Ulimboka kutokana na kutopata ushirikiano wake.

Dk. Ulimboka ambaye ni Mweyekiti wa Jumuia ya Madaktari, alitekwa na kuteswa vibaya kisha kutupwa katika msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamikia Juni 26, 2012.
Wakizungumza na Tanzania Daima kuhusu utetezi wa DPP, wanasheria hao Mabere Marando, Profesa Abdallah Safari na Method Kimomogoro walisema kuwa amedhalilisha taaluma ya sheria.

Marando alisema DPP amejiunga na jeshi la polisi kuficha uovu unaotokea nchini kwa kile alichoeleza kwamba jukumu la polisi ni kupeleleza tukio kabla ya kumfikiria muathirika awe sehemu ya taarifa ya upelelezi huo.
Alisema kwa kauli ya DPP ni wazi kuwa kama Dk. Ulimboka angepoteza maisha katika tukio hilo, basi wapelelezi wasingekuwa na kazi ya kufanya.

"Hii kwangu ni kauli ya ajabu na sijawahi kufikiria mtu kama Feleshi anaweza kuungana na polisi kuficha ukweli. Jukumu lake ni kutoa maelekezo ya vitu vinavyotakiwa kwa ajili ya kesi, siyo naye anaanza kulalamika!" alisema.
Kuhusu polisi, Marando alisema kwa sasa hawafanyi kazi ya kitaalamu zaidi ya kutegemea kumkamata mhalifu na kisha kumtesa ili atoe maelezo wanayoyataka.

Alisema hali hiyo ndiyo imesababisha takriban asilimia sabini ya kesi zilizo mahakamani kuwa na maelezo ya ‘onyo' badala ya kufanyiwa kazi kitaalam.
Marando aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo mtuhumiwa anapokuwa na mwanasheria mzuri mara nyingi anashinda kesi na serikali kubaki kuaibika na kutoaminika mbele ya wananchi.
Alisisitiza kuwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, alipaswa kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kupata ushahidi wa uhakika.

"Watuambie walifanya nini kumtafuta Dk. Ulimboka, si wana wachunguzi? Kwa nini wasiende nyumbani kwake wakapate huo ushahidi wanaoona haukutolewa?" alihoji.

Marando alisema Dk. Ulimboka alishamtaja ofisa wa Ikulu aliyeshiriki katika kumteka, hivyo lilibaki jukumu la polisi kumkamata mtuhumiwa aliyetajwa na kufanya gwaride la utambuzi.
Alisema hali hiyo ya kumtaka Dk. Ulimboka aende katika ofisi za polisi kutoa maelezo mengine huenda ikawa ni mtego mwingine wa kumdhuru baada ya kumtaja mtu wa serikali anayehusika na kadhia hiyo.

Naye Prof. Abdallah Safari alifafanua kuwa kisheria suala la kutafuta ushahidi ni la serikali yenyewe.
Alisema kuwa tayari Dk. Ulimboka alishawaonyesha njia na kwamba serikali ilipaswa kuanzia alipoishia kwa kuwakamata wote waliotajwa ili kupata ushahidi zaidi.

Mwanasheria mwingine kutoka jijini Arusha, Method Kimomogoro, alisema kuwa Dk.Ulimboka alishatoa maelezo yenye kujitosheleza juu ya mhusika aliyemteka.
Alisema DPP Feleshi ni wazi kwa sasa anachagua matukio ya kufanyiwa kazi na kwamba watu wenye mawazo huru wanapopata tatizo ofisi yake haioni haja ya kushughulika nao.

Alitolea mfano mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Usa River mkoani Arusha na mwanachama mwingine Mbwana Masudi aliyeuawa Igunga mkoani Tabora.
Pia alitaja mauaji ya kijana Ally Nzona wa mkoani Morogoro aliyepigwa risasi na polisi kwenye maandamanao ya CHADEMA kuwa ni uthibitisho tosha wa namna ofisi ya DPP na jeshi la polisi wanavyofanya kazi kwa ubabaishaji.

Kimomogoro alisema jambo la kusikitisha ni kuona watu wenye mawazo huru ya kuikosoa serikali wanavyokamatwa makundi makundi kama wahalifu kwa wakati mmoja.
Alisema inashangaza kuona kundi la askari lililomzunguka Mwangosi kabla ya kuuawa kwake likiwa halijaguswa hadi leo.

Aliongeza kuwa DPP kwa nafasi yake kwa umma alipaswa aonyeshe dhamira kutenda kitaalamu na si kama mwanasiasa jambo alilosema si jema kwa mustakabali wa taifa.
Wakati wanasheria hao wakikosoa kauli ya DPP, jeshi la polisi limeendelea kushikwa na kigugumizi kueleza kama lilishawahi kuwahoji watu waliotajwa na Dk.Ulimboka.
Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, alipoulizwa jana, alitaka aandikiwe maelezo katika karatasi na yafikishwe ofisini kwake.
"Kwa sasa nashughulikia kutoa taarifa ya Sheikh Ponda, hayo maswali yako yaandae kwa maandishi kisha utaniletea hapa ofisini," alisema Senso.

Gazeti lenywe tanzania daima......udaku.com
 
Huwezi kupata tarifa toka tanzania daima halafu ukaita ni habari utakuwa unaoga tope halafu unajiafanya msafi.
 
Dpp kimeo kweli yani kweli unafungua mdomo na kusema ulimboka hatoi ushirikiano? Ighondu mshamuhoji?
 
Chadema ni wauwaji, wamemtesa kibanda, wamemmwagia tindikali mussa tesha, walikuwa wanataka kumtesa mhariri msaki, watashindwaje kumteka na kumtesa ulimboka???

Punguza ushabiki,jaribu kuwa na busara
"Vox popoli vox dei"
 
Mmejaribu kuivuruga nchi mmeshindwa mmejikuta mnavurugwa nyie
 
Back
Top Bottom