Download Speed: Shkamoo Halotel

sidhani kama fb app ichukue 15minutes kwa kasi ya halotel kuna tatizo jingine
Labda. Ila ni kweli na mimi imebidi nishangae maana nimehamia huku kwa sifa zake
 
Tatizo hapa ni speed. Shida sio urahisi wa vifurushi. Halotel ndio wenye speed optimal na gharama zao
 
Hapa nipo kijijini kwetu idumila 3g ya halotel napata kama kawa na vijiji vya jirani pia wanafaidi. Halotel imetukomboa hatupandi tena kwenye miti kama ngedere
 
Mbona speed ya kudownload app ipo chini hivi? Yaani nilipokuaga na line ya tigo 4G ilikua poa sana kwenye kudownload na speed ya Internet Ila tatizo lao lilikua ni kupoteza network. Nashangaa hapa na download game lenye mb 81 mpaka ninesahau na imekata
 
Sim yako itakuwa made in zingshong village, halotell hadi huku porini kwetu ni 3g+
 
Sim yako itakuwa made in zingshong village, halotell hadi huku porini kwetu ni 3g+
Tatizo sio 3g jaribu kuelewa. Tatizo ni uwezo wa kudownload. Tigo 4G wapo juu japo nimewahama
 


Wenzangu sijui mnaishi wapi kupata speed mbaya kwenye 4g kiasi hicho
 
mi nimetoka kuangalia game ya man na everton kwenye pc yangu kwa kutumia modem ya halotel na kifurushi changu cha mwezi cha mwezi sina presha voda walinishinda kwa kweli
 
Hao lazima wawe na speed kwa kuwa wako watumiaji wachache

Ngoja muwe wengi utanifuata
 
Baada ya kuona mabandiko mengi humu ya kuisifu hii Halotel jana nikaamua kuijaribu nikajiunga na kifurushi cha usiku yaani ni majanga nimeshindwa hataa kuplay video kwenye youtube. Mpaka asubuhi nimeweza kudownload video 2 tu toka dramacool. Yaelekea wengi humu ni wapiga debe. Bora nibakie nlipo
 
Mi nlikwenda kwenye ofisi zao wanitengenezee Special number wakaniambia 20,000/=,nikasita nikawaambia siku nyingine,kumbe mtandao wenyewe ndo hivyo kwa hyo ningepata hasara bure
 
Mimi nimeshatumia mitandao karibu yote katika internet lakini kwa halotel ni mwisho, siuji siku zote walikuwa wapi unatumia mpaka unaifurahia hela yako. na dowload speed iko faster kweli kweli. poleni mnaoibeza kizuri kinajiuza
 
Itakuwa unatumia mchina wewe, mimi nadowload huku natazama mechi 2 au 3 kwa wakati mmoja kwa liverstream na hakuna kukwama wala nini, tena bila moderm natumia simu kuunga kwa wifi,
 
Kama upo ulaya, internet haina mafua wala kikoozi, unaangalia hata tv zote mfano filmon tv etc. nahisi voda, tigo etc wajiandae kifo cha wajia
 
nilikuwa away kidogo sikuweza tuma speed yangu ya 4g ya tigo



na hilo eneo kama unavyoona signal sio kubwa sana nikienda eneo lenye speed Nzuri nitacheki tena speed yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…