Dowans! Dowans! Wakati nchi inaangamia....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans! Dowans! Wakati nchi inaangamia.......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BIN BOR, Jan 30, 2011.

 1. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tatizo la fidia sio kwa Dowans peke yake. Ni pesa kiasi gani ililipwa kama compensation kwa South Africa kwa kuvunja mkataba wa ATCL, au Rites wa India nao si wako katika mstari? Ni pesa kiasi gani ilipotea kwa kuvunja mkataba wa TTCL? Na kuna madudu mengi tu, ambayo hatuyajui au tunayajua kama ya mikataba ya madini, vitalu vya uwindaji na hili la kutengeneza noti mpya zenye kasoro kibao. Kwa sasa siasa inatupeleka kupiga mayowe Dowans! Dowans! Lakini ukweli ni kwamba nchi inaangamia kwa madudu mazito kuliko Dowans.
  • Rais apunguziwe madaraka ili katika mambo haya asiwe yeye refa, kipa na mshika kibendera, kama katiba mpya itachelewa hili lifanyike kama kiraka maana tushavizoea
  • Mikataba yote sasa ijadiliwe kwa uwazi bungeni, maana kuna faida za usiri lakini tukiwaachia usiri tunaibiwa
  • Itumike sheria ya uhujumu uchumi kuwafikisha kortini na kuwafilisi waliotufilisi
  • Ile habari ya kinga ya rais kutoshtakiwa haina tija kwa Tz ya leo

  Bado naendelea kutafakari, lakini tunapopiga kelele za Dowans wenzetu wanazidi kutufilisi kupitia madudu mengine mengi tu.
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Dowans ndo mwanzo
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakubaliana na wewe kabisa hicho kiraka tunakihitaji kwanza, na haraka sana sababu sasa tuko uchi, na hatuwezi kuendelea hivyo wakati tunangoja nguo mpya
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  MKuu nakubaliana na wewe na ni kweli kuwa Dowans ni dalili tu na mizizi ya matatizo ni uwezo mkubwa wa rais kikatiba. Ni muhimu sana apunguziwe maamuzi mazito. Katiba hii ilitungwa ikiwa na ideal president in mind kama Nyerere, lakini hawakuona mbele kuwa si kila kiongozi ana moyo na utashi kama wa Nyerere. Maana kuna mengi mzee wetu alikosea lakini hatuwezi kukataa kuwa alikuwa na utashi wa kuona makosa yake na ya kuyarekebisha na hata kuji-limit kwa kujiuzulu (anglieni Mubarak anavyong'ang'ania madaraka huko Misri)

  Kwa hiyo marekebisho haya ni muhimu!
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kwa hilo nakubaliana na wewe. Hila nataka niongeze kwamba apatikane mbunge aliulize swali hilo bungeni, akitaka kujua siyo tu fidia iliyolipwa, bali pia gharama nyinginezo zilizoambana na malipo hayo. Aidha takwimu hizo zihusishe pia fidia ambayo imekuwa ikilipwa kwa kampuni za ujenzi wa barabara kutokana na kuvunja mikataba bila ya kufuata utaratibu.
   
 6. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkubwa chanzo cha matatizo yetu mengi ni hicho!!! Kwa kupitia uchochoro huo Mkwere anatupiga mabao ya kisigino huku akijua hatuwezi kumfanya chochote!!
   
 7. Mr. Tanganyika

  Mr. Tanganyika Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dowans in kama blanketi iliyomfunika mgonjwa mwenye maradhi mengi. Tukimfunua tutayatibu na hayo mengine tutakayoyaona.
   
Loading...