Hivi BRELLA wanaposajiri kampuni lenye ubia na makampuni mengine yaliyoko nje ya nchi hawafanyi uchunguzi wowote? Na kutokana na habari hizi BRELLA hawawajibiki kwa lolote? let say kufuatilia nyaraka zilizowasilishwa na hao wahuni, kuwasiliana na portek kisha kuwashtaki waliotoa taarifa za uongo!
Usalama wa taifa bado wapo matatizoni, inakuwaje watu watoe taarifa za uongo na kujipatia mabilioni ya walipa kodi bila usalama wa taifa kushtukia na kuchukua hatua. Hivi kweli Mkuu wa Usalama wa Taifa hana habari kuwa Dowans haina uhusiano na portek?
Hawa portek wanachukua hatua gani baada ya kuona wamepakaziwa? Nashauri tuanzishe move ya kuwataka portek watoe taarifa rasmi.
Tuanzishe petition ya kuitaka Serikali itaifishe mitambo ya dowans.
haya mambo yameanza toka Kikwete anaingia madarakani, sasa inakamilika miaka minne, sijui anayachukulia serious kwa kiasi gani, hasira za wa-Tanzania including JWTZ zinazidi kupanda, haya ya Madagaska yanaweza kutokea si muda mrefu.