Double Standard za TRA kwenye kurejesha/kufidia gharama za EFD mashine

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
1,171
2,000
Hii ipo haswa kwenye taasisi zinazokusanya ushuru na mapato.

Mfano ni hii.

Wao (TRA) wanasema ukinunua mashine ya EFD una haki ya kurudishiwa gharama kwa punguzo la kodi, kufidia gharama ulizonunulia mashine.

Picha linaanza mashine umenunua mwezi wa 10 mwaka 2020, kumbuka hapo ulishakadiriwa kodi unayopaswa kulipa kwa mwaka mzima.

Mwaka 2021 unaanza, unaenda kufuatilia kurejeshewa gharama ili makadirio yakishafanywa wakate na gharama za mashine.

Unapewa jibu la kwamba haiwezakani eti kwasababu mwaka huu ni mpya ulipaswa kufuatilia mwaka ulio nunua mashine.

ILA WAO MADENI YAO HUWA HAYANA KIKOMO UTADAIWA KILA SENTI HATA KAMA NI YA MWAKA 1999.

Wanachokifanya ni sawa namimi kwenye biashara yangu nisipolipa kodi au ikaoneka kuna upungufu wa kodi mwaka husika, wakiniletea deni niwajibu siwezi kulipa kwasababu hesabu za biashara za mwaka husika zilishafungwa, hili jibu halina tofauti na wanalotoa wao.

Mitano tena.
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
4,514
2,000
Wakati wao ukienda kufungua biashara mwezi wa 10 utakadiriwa na kodi ya robo 3 za mwaka(mwezi wa 3,6,9) kwanini wao hawaachi kudai kodi ya wkt huo hujaanza kufanya biashara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom