Dotto Bulendu: Soka limekabidhiwa wanasiasa na wasanii ndio tutarajie ushindi dhidi ya Uganda? Wanasoka wetu wastaafu hawapo? Hawathaminiwi?

Kuwaweka wachezaji wa zamani kama ni morale kwa timu ya taifa ni sawa kumchukuwa.Lipumba kumpeleka chuo kikuu kama ni mfano kwa undergraduates. It's disheartening.

Kwa miaka hiyo wachezaji walikuwa wanacheza soka kwa moyo wa mapenzi huku wengi wao walikuwa hawalipwi mshahara, bali ni hela ya sabuni tu ya kufulia nguo za mazoezi. Kibaya ni kuwa serikali nayo ikawwacha mkono badala ya kuwatumia kukuza vipaji. Kwa mfano, serikali ingeweza kushirikiana na wizara za elimu na michezo na kuwapangia hawa veterans kipindi japo mwezi x 1 kwa shule zote ili watambue talents na inapobidi kuwaweka hawa vijana karibu na facilities kwa ajili ya kuwa advance.

Sasa unapomchukuwa mtu ghafla kutoka huko.aliko baada ya decades of negligence, kachoka na yuko dhaifu financially, halafu awe ni role model italeta picha gani? Hakuna anayetaka kuwa financially unstable
 
Tatizo Africa kila anaepewa wadhifa hajui atafanya kazi gani mradi anajua cheo chake tu
Kweli kabisa huwa naona matukio yeyote yanapotokea huwa wanatafutwa wastaafu waliopitia hizo kazi na sio kila mtu
Kama mauwaji yalitokea anatafutwa mkuu wa police mstaafu na anajibu na kupangua hoja kwa sababu amebobea katika sekta hiyo ya crime

Lakini kwetu kila mmoja anaingilia yasiyomhusu na akibwana sana utasikia mimi sio msemaji

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
hata kama morali ya kuishabikia taifa stars ilikuwepo ila kwa huyo mwenyekiti na jopo lake mimi na jamaa angu tumeanza kureview mtatazamo kama tulikuwa sahihi, hakuna ambaye hakuwa anaombea na angependa timu yetu ifungwe na kutolewa ila inafikia mahala tunaona ni kheri iwe hivyo ili tujipange upya
 
Kule Ulaya na mataifa mengine ambayo yameendelea kisoka,inapotokea kunahitajika hamasa kubwa ya kujenga morali kwa wachezaji na mashabiki basi wale wachezaji Nguli wastaafu hutumika sana kuhamasisha morali ya ushindi.

Hii hutumiwa sana na Vilabu vikubwa duniani ama timu za taifa ambapo wakongwe(Legendaries) huwekwa jukwaani sehemu maalum kabisa ikiaminika kuwa wale waliopo uwanjani wakitazama jukwaani na kuwaona wakongwe morali inapanda na hata kwenye kujenga hamasa wachezaji waliocheza kwa mafanikio hutumika sana.

Sasa nakaribu kutazama mbinu inayotumiwa na kamati maalum ya kuhamasisha ushindi wa timu ya Taifa hapo keshokutwa.

Kwenye mkutano wao na waandishi wa
habari,mbali na kuwajumuisha waandishi wa michezo,lakini naona inawatumia zaidi waigizaji maarufu nchini akina Wema,Shilole,Steve Nyerere n.k na kuwaweka kando wanasoka waliocheza kwa mafanikio miaka ya nyuma.

Kwa nini kamati inaacha kuwatumia wanasoka waliowika miaka ya nyuma inakimbilia kuwatumia waigizaji?kwa nini tusiandae vipande vya vidio vya wanasoka waliowika huko nyuma wakiwahamasisha vijana wetu na wanasoka hawa siku ya jumapili wakatengewa eneo maalum pale Jukwaani?

Kwa nini tumewatenga wanasoka walio hai ambao waliipekea Tanzania katika fainali za mataifa huru Afrika mwaka 1980 kama
sehemu ya hamasa kwa wachezaji na Watanzania?

Kwa nini tusiwarekodi na hata kwenda nao kwenye "Press Conference" wachezaji wakongwe waliocheza fainali hizi na wakasema neno la hamasa kwa watanzania na hata tukawaambia watanzania wajae uwanjani waungane na wakongwe pekee waliofuzu fainali hizi kutoka Tanzania na badala yake tunawatumia akina Wema pekee?

Nafahamu akina Wema wanamashabiki nyuma,lakini katika hili la Jumapili hebu tunatumie zaidi wachezaji wetu waliocheza kwa mafanikio wakati wao.

Mbali na akina Tenga waliokuwemo kwenye kikosi cha Stars kilichofuzu fainali hizi pekee,kwa nini pia tusiwatumie wanasoka waliocheza kwa mafanikio kwenye Vilabu na hata kufika ngazi ya juu?

Waliokuwemo kwenye Kikosi cha Simba kilichocheza Fainali za kombe la Shirikilo la Soka Afrika mwaka 1991 na walicheza timu ya taifa wengi wao wapo,kwa nini tusiwatumie hawa kama sehemu ya hamasa?

Walioifikisha Yanga hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1998 bado wapo kwa nini tusiwatumie kama sehemu ya hamasa na badala yake tunawatumia zaidi waigizaji na waimba muziki?

Tunapowatumia waigizaji na waimba Muziki kuhamaisha ushindi wa Stars,tusiwaache wachezaji nguli wa zamani akina Leodigar Tenga,Sunday Manara,Abdalah Kibaden,Juma Pondamali,Adolf Richard,Zamoyoni Mogella,Mohamed Mwameja,Ken Mkapa ,Peter Tino
mfumgaji wa bao la
Star lililoipeleka Tanzania kwenye fainali za
mataifa huru na wengine wengi katika kuhamasisha wachezaji,kuhamasisha mashabiki ili jumapili tupate ushindi.
#nizamuyetu
Well said!!kunywa Pepsi mkubwa wao popote ulipo nitakuja kulipa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulaya sio tanzania.
 
Pengo la Ruge RIP ndio linaonekana sasa nmeamin kweli yule bwana alikua master mind wa taifa angekuepo na angeona fursa sidhan kama huu upimbi tunaoushuhudia tungeuona
 
Unafiki ndo mwingi watu hawataki kuusema ukweli, na kama hakuna maandalizi, unaqualify kwenda kushiriki au kushindana...
Nilikasirika sana, Rais anawaita Ikulu anawapa mpaka 50m tena anasisitiza zikalete matokeo, wanaenda kufungwa kijinga kabisa, Lesotho wanakuja Chamazi wanakunywa nao madafu na kuwaachia point moja.
Me naomba Uganda wakaze kabisa, wasijekuharibu rekodi yao na yule goalkeeper wao amaintain cleensheet yake
*Uzalendo siyo unafiki wa kusifia kilicho kibovu*

Sent using Jamii Forums mobile app
Isitoshe game la mpira mi border less kwa kweli politically and geographically

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CAF wanauafuatilia huu mchezo kwa makini sana kama Uganda atalegeza ili jilani yake afuzu,anaweza kukutana na lungu la caf hata kutolewa kwenye mashindano ,vile vile bado Lesotho ana nafasi kubwa kufuzu kuliko stars,kwa hiyo sisi tuendelee kufanya siasa na usanii uchwara haya ndo tunaweza,huyu msomali anatuhalibia sana mpira wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom