PostGE2025 Doria mitandaoni zinaendelea

PostGE2025 Doria mitandaoni zinaendelea

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Asante sana, uko sahihi. Ndiyo maana nilisema kwamba maombi pekee hayatoshi; sikumaanisha kwamba maombi hayana umuhimu. Hakuna taifa, jamii (au hata mtu binafsi) iliyowahi kupiga hatua kwa kutegemea maombi pekee.

Mungu ametupa uwezo wa kufikiri na kutatua changamoto. Kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu, hatupaswi kumwachia Mungu pekee kufanya badala yetu, kwa kuwa kufanya hivyo kunaashiria uzembe na kukwepa wajibu.

Maisha ni muunganiko wa vipengele vya kiroho, kimwili na kiakili. Changamoto za kiroho hupambana na nguvu za kiroho; za kimwili hushughulikiwa kimwili; na zilizo katika uwezo wetu wa kiakili lazima tukabiliane nazo kwa kutumia maarifa na busara tulizopewa. Big up to TEC, na wengine wenye kusimamia haki na utu bia kuangalia mtu usoni.

View: https://www.instagram.com/reel/DR4YbptEl6G/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==


Just imagine? kwa yote yaliotokea bado tuna watu hawa. So sad. Nasikita kusema, hawa wamechangia kulifikisha taifa letu hapa. Kuvumilia maovu
 
Ndio maana sikujua kumbe inawezakana kuteka mtu na kumtoa kafara:
Ndio ya hao wasiondugu watatu:
Yesu arudi haraka kukomesha huu uzumbukuku:
 
Back
Top Bottom