Don't underestimate Zanzibarians | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Don't underestimate Zanzibarians

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Mar 21, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa Znz kwa muda sasa. Nimekuwa nakaa vijiwe vya CCM (maskani) na CUF. Nilichogundua ni kuwa Wa Znz wapo kitu kimoja kuhusiana na maslahi yao. Wanapiga sana vita muungano kwa madai kuwa haujalinda maslahi yao. Nadhani katika mchakato wa katiba, Wa znz waachwe wajadili mambo yao halafu waje mezani tujadili pande zote ziridhike na aina ya muungano tunaoutaka. Hawa Wa znz wakiendelea kukandamizwa na kupuuzwa, kuna siku watadai nchi yao na hatutaweza kuwazuia. Moto wa nchi za kiarabu utaanza kuwaka znz unless tumewapa nafasi wa determine their own destiny. Ukiangalia kwa makini, marais wa Znz wamekuwa wanawekwa na Bara. Hii inawanyima nafasi ya kuchagua viongozi wanaowapenda. Chadema Znz au chama kingine wanaweza kuja na sauti ya utetezi wa maslahi ya Znz na haki yao ya kufanya maamuzi ipanuliwe. Ikija huja hii, CUF na CCM wataporomoka. Wa znz hawana mtetezi maana CUF baada ya kupewa madaraka hawatetei tena Wa znz.
   
 2. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Si waanze kudai sasa,hawana msaada wowote kwenye Muungano wanatutia hasara tu, mfano wao ndio wadaiwa sugu wa TANESCO wanadaiwa billion 56, lakini ajabu mgao wa umeme hauwagusi kamwe, sasa wanini, wamekuwa mzigo kwetu for over 40 years, I think it is a high tyme now wondoke warudi tu kwao!
   
 3. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  its their bloody country and they can decide their own destiny

  sisi huku tunataka fairness kwenye kukatiwa huuu umeme
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ni Zanzibaris na sio ZANZIBARIANS....
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I have come to believe that there are Zanzibaris in JF who come in & pretend to be non-Zanzibaris. I respect more those who come out & admit they are Zanzibaris & are fighting for Zanzibar.
   
 7. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
   
 8. p

  plawala JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hawajui wao ndiyo wanaufaidi zaidi lakini ndiyo walalamishi zaidi,
  ok hiyo kura ya maoni iletwe,tuipige kila mtu apate anchostahili,halafu tupime baada ya hapo nani ana uhuru zaidi na nani kaupoteza zaidi,siombei upande wowote upoteze kwa kujitenga lakini tukubaliane na matokeo vilevile
  Mpaka sasa wana raisi,bunge lao,jeshi lao(hata kama sio rasmi),katiba yao,bendera yao sijui nk,tumalizie na hivyo vichache vilivyobaki
   
 9. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..ni vigumu sana kuelewa msimamo wa wa-Zanzibar.

  ..kwanza wanasema hawataki muungano, halafu wanageuka wanasema makubaliano ya muungano yamekiukwa.

  ..kama hawataki muungano, basi waachane na hoja kwamba makubaliano ya muungano yamekiukwa. badala yake wajenge hoja kwamba muungano ni hasara na usumbufu kwa wa-Zanzibar.

  ..pia kuna wakati hulalamika kwamba wanataka Raisi wa Zanzibar awe makamu ktk serikali ya muungano. sasa hii nadhani ni hoja ya watu wanaopenda muungano.

  ..kwa upande wa Tanganyika nadhani wengi, haswa wanasiasa, wanaona aibu au uwoga kutamka kwamba hawataki muungano. Watanganyika tunapaswa kujiuliza tunafaidika nini na muungano huu? je, ukiondoka tutapungukiwa na kitu gani?
   
 11. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hasara kubwa tutakayo ipata Tanganyika ikiwa Wa Zanzibari watajitenga ni mafuta yao ambayo mpaka sasa tunalazimisha kuwa ni ya Muungano wakati mapato ya madini yetu huku bara hata senti tano hawapati Visiwani!

  Baadhi ya Faida watakazopata Zanzibar ikiwa watajitenga ni kama ifuatayo:
  1) Zanzibar itajiunga na Jumuiya za Kimataifa kama vile OIC na kushirikiana moja kwa moja na jumuiya hii kwa faida na maslahi ya Zanzibar!
  2) Zanzibar itafaidika na ushuru wake wa forodha bila kusimamiwa au kuingiliwa na TRA!
  3) Zanzibar itakuwa kiuchumi baada ya kuitangaza kisiwa hicho kuwa ni Free Port kama ilivyo Dubai na Hongkong!
  4) Zanzibar itaachana na siasa za kijamaa au nchi isiyokuwa na dini na badala yake kujali mila na desturi zenye kuegemea maadili ya Kiislamu na hivyo kusaidia kupunguza madanguro na vilabu vya pombe na ukimwi na madawa ya kulevya kupungua kwa kasi kubwa!
  5) Vyanzo vya kazi kuanzishwa na kupunguza ukosefu wa kazi uliosababishwa na utawala wa TZ chini ya siasa mbovu zilizoasisiwa na Julius K. Nyerere!
  6) Utawala wa sheria utapamba moto na kufanya tawala za kimabavu na za wauwaji kama za Benjamin Mkapa kuwa historia ktk visiwa hivyo!
   
 12. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  zanzibar na oman (u.a.e?) ni baba moja mamamoja......WAZANZIBAR WAKI-APPLY KAZI WANAPATA KIURAHISI NA SI WA-BARA...(na kumbuka maafisa ajira hapo unakuta ni wazanzibar)...its not a joke....!
  SURE DONT UNDERESTIMATE THEM...!
   
 13. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama hawautaki muungano sioni ubaya kwani ni haki yao kujiamulia nini wanataka na sio kuwaburuza kwa kitu ambacho wenyewe hawaridhii.
  Who knows...may be Zanzibar will be far better off economically kama watatoka kwenye hii ndoa.
   
 14. kuberwa

  kuberwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 568
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ubinafsi umekujaa tu huna lolote! Hawa ni ndugu zetu hatuwezi kuwaacha wakihangaika! Zaidi ni kuwapa uhuru wa kujitetea na kuchagua ni aina gani ya muungano na si unyanyasaji kwa kisingizio eti tunawasaidia!
   
 15. m

  matunge JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Mafuta? kitu cha kufikirika hicho
  Hivi mnafikiri OIC ni suluhisho pekee kwa Zanzibar, ni nchi ngapi zilizo katika OIC lakini bado ni matatizo
  Kila wakati mnajifananisha na Dubai, Hongkong...ni visiwa vingapi viko huru lakini havijafikia hadhi hiyo
  Humtendei haki BABA wa Taifa na pia Ben Mkapa, Nyerere aliongoza nchi ikiwa haina kitu (wasomi wachache, uchumi duni kwa raia).Alitoa elimu bure, alitaifisha shule za wazungu kuwa public.Na mengine kibao Mkapa aliimarisha uchumi wa nchi, haijawahi tokea.
  Nchi kutokuwa na dini maana yake nini? watu ndo wanapaswa kuwa na dini..si nchi. Pia usidharau dini nyingine..inaonesha unaupinga ukristu.Angalia siku ya kiama usije kukuta MUNGU si mkristu, wala muislamu..bali dini yake ni WEMA
  Pia katika dunia ya leo wala huwezi zuia kasino, bar, na mengine...unachopaswa kufanya ni kutunza imani yako na wema wako...maisha ya mwingine yanakuhusu nini
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  JokaKuu,
  Wakati tunasema bila ya kuamini kuwa Wazenj hawautaki Muungano, Je watanganyika na wao wana msimamo gani kuhusu Muungano. Watanganyika ndio wengi kwa idadi sasa kama watanganyika hatuutaki Muungano mbona tuko kimya? Tunasema tu wazenj ni mzigo, tunawabeba. Je tunapenda mzigo? Je tunapenda kuwabeba wazenj?

  Mkuu Zaidi ya Rev. Mtikila na ile move ya G55 nani katika Tanganyika anasema hautaki muungano na amechukua hatua gani?

  Umesema wanasiasa wanaogopa..hata CHADEMA nao wanaogopa kuzungumzia Muungano?

  Kwa maoni yangu wakifanya hivyo itakuwa njia rahisi ya kupata kuungwa mkono Zanzibar. Waseme CHADEMA wata-negotiate upya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. au waseme bila kuuma meno kuwa CHADEMA watairudisha Tanganyika ili members wa Muungano wapate nafasi ya kujadili Muungano kwa uwazi....Pengine kusema kuwa watauvunja muungano kwa sasa wanaweza kumpa sababu Tendwa kukifuta lakini hizo kauli za mwanzo zitawapa wafuasi wengi Zanzibar.

  Kilicho wazi ni kuwa kuna siri kubwa ya Muungano ambayo inaonekana CCM wanaijua na ndio wanalifanya suala la muungano kuwa ni nyeti na lisiguswe.

  Katika arrangement ya sasa Tanganyika inatumia mamlaka ya Muungano katika hali zote,wakati Zanzibar wanalazimika kupitia serikali ya Muungano. Je kuna faida kubwa Zaidi kuliko hii kwa Tanganyika?
  Huu muingiliano wa serikali ya tanganyika,kuwa ndio hiyo hiyo serikali ya muungano ndio inayowapa mwanya wazenj kusema wanaminywa,wanabanwa na kuna ukweli katika hilo. ni serikali ya Muungano ndio ina mamlaka ya mambo ya nje.

  Zamani ushirikiano wa kimataifa haukuwa katika Muungano lakini sasa hili pia limeingizwa katika Muungano na hivyo kuifanya Zanzibar isiwe na uwezo wa kutafuta washirika au wabia au misaada kwa mambo yale yasiyo ya muungano wao wenyewe.kwani ni lazima wapitie Muungano.

  Inawezekana sisi hatuzioni faida wazi wazi za muungano zaidi ya bughudha za wazenj na kuwabeba lakini Zanzibar wakiwa nje ya muungano au Tanganyika pia ikiwa na serikali yake inayoonekana wazi basi tutaweza kuchanganua vizuri juu ya nani anafaidika zaidi na Muungano.

  Ikitokea hivyo kutakuwa kuna mfumo wa majadiliano katika pande mbili ambazo zitaamua mamlaka yepi yawe kwa serikali ya Muungano na mamlaka yepi yabaki kwa serikali ya tanganyika na yepi yabaki kwa serikali ya Zanzibar.kutakuwa na mipaka ya kimamlaka inayoeleweka. sasa hivi ni shaghala baghala tu.

  mkanganyo huu umezaa manung'uniko na kelele na sasa unajenga kejeli na chuki.
  Siku ambayo watu wataamua kuzungumza kwa maana ya "kunegotiate" kama wabia wa Muungano basi kelele zitapungua.
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  mkuu.
  Kuna wengine ni TISS humu JF lakini wanakuja kama washabiki wa vyama fulani kuvua sangara.
  kama wamo humu sio vibaya..nafikiri zaidi tuone hoja zao na kufanya mjadala nao.
  Unaelewa JF imekuwa kama vile ni tawi la chama fulani, wengine wote huonekana ni "mafisadi" au huoni mijadala humu na lugha za JF?
  kama wanakuja kama anonymous hakuna ubaya, tuone hoja zao na tujibu hoja zao. wana sababu zao za kufanya hivyo na tuziheshimu.
  La msingi JF inawaunganisha watu wote.tusianze kuigawa kuwa non zanzibari na zanzibari au Tanganyikans vs Zanzibaris, au Tanzania baras vs Zanzibaris.
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Mbona uajichanganya? Iwapo wote wana msimamo moja sasa wanahitaji msaada wa nani? Ati CHADEMA waje Zanzibar na huku wana roho ya kutopenda mema ya Wazanzibari? Wao si wanaokejeli maamuzi ya Wazanzibari?
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Asiejua neno haambiwi maana lakini mwenye akili yake hujiuliza.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unaweza ukatoa kitu kimoja ambacho Muungano huu umekukosesha?
   
Loading...