Dondoo mbalimbali kuhusu chafya

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
3,247
6,769
1. Mwanadamu kamwe hawezi kupiga chafya akiwa usingizini.

2. Mtu anapopiga chafya vijidudu vya magonjwa, vumbi na hata majimaji yaliyomo puani hurushwa kwa nje kwa spidi ya; 161 kilomita kwa saa.

3. Iguana ndiyo wanyama wanaoongoza kupiga chafya kuliko wanyama wote.

4. Chafya iliyodumu kwa muda mrefu ni ya mwanamama muingereza Donna Griffiths,ilichukua siku 978.

5. Kamwe huwezi kupiga chafya ukiwa umefumbua macho.

6. Unapopiga chafya unarusha zaidi ya vijidudu vya magonjwa zaidi ya 10,000 kwenye mazingira, hivyo unashauriwa kutokupiga chafya bila ya kuziba pua na ni vyema ukatumia kitambaa kuliko mkono.

7. Mwanga mkali wa jua unaweza kupelekea kupiga chafya kwa baadhi ya watu.

Unaweza ongeza chochote kuhusu chafya.
 
Kupiga chafya husaidia kufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri zaidi lakini zisiwe excessive kwani zikizidi sana napo huwa ni shida.
 
Huwezi kupiga chafya ukiwa unangonoka kwa sababu mzunguko wa damu unakuwa mkubwa
 
Kwanini mtu unapopiga chafya nyingi mfululizo huanzwa kutokwa na mafua? kuna uhusiano gani kati ya chafya na Flu?
 
iyo namba 5 siyo kweli.
Mkuu ni kweli huwezi piga chafya macho yakiwa wazi lazima yafumbe.

Kugundua ni shida kwa sababu kitendo chenyewe cha kupiga chafya udumu kwa sekunde chache mno ambapo mpaka unamaliza na macho ufunguka hivyo unashindwa jua kama ulifumba.
 
Kwanini mtu unapopiga chafya nyingi mfululizo huanzwa kutokwa na mafua? kuna uhusiano gani kati ya chafya na Flu?
Chafya husababishwa na foreign particles na irritants kama vile vumbi,pilipili na ugoro.

Vitu mara nyingi vimebeba bacteria na hata baadhi ya virus.

Vinapoingia katika pua wakati unavuta hewa vitu hivi hukusanywa na vinywele nywele(cilia) vinavyopatikana ndani ya pua ili visiweze kupita ndani na hatimaye kusababisha magonjwa.

Vinapokusanywa na hivi vinywele nywele hupelekwa kwenye ukuta wa pua (nasal membrane) ambao uzalisha majimaji(mucus) ambapo majimaji haya uchanganya vumbi na vijidudu na kuvitoa nje kupitia chafya.

Ikiwa kiasi cha vumbi bacteria na other irritants zimeingia kwenye pua kwa kiasi kikubwa mucus pia huzalishwa kwa kiasi kikubwa na mfululizo hali itayofanya utoe nje kama mafua.
 
Namba moja siyo kweli, watu waliopoteza fahamu hupiga chafya wanapoanza kupata fahamu
No mtu akiwa amelala hawezi kupiga chafya kwa sababu motor neurone kutokuwa stimulated na hivyo reflex signal kutopelekwa kwenye ubongo.

Ingawa kiasi kikubwa cha external irritants kama vile ugoro unaweza mfanya mtu aliyelala kupiga chafya itakayopelekea kuamka na si kuendelea kulala.
 
Kumbuka hata motor neurone zipo voluntary na involuntary kasome vizuri anatomy and physiology
 
wewe acha kuongea vitu bila uhakika,unajua Kazi ya motor nerve system?autonomic nerve system?
 
Kumbuka hata motor neurone zipo voluntary na involuntary kasome vizuri anatomy and physiology
Yeah, i know that.

Na kumbuka usingizi una five phase,kuna baadhi ya phase tuna zi consider kama partial sleep ambapo mtu anakuwa katika state ya kati ya usingizi na kuamka na mtu katika stage hizi anaweza piga chafya under very strong stimulus na ukishapiga chafya tu lazma uamke kabisa.

Lakini ni ngumu during rapid eye movement(REM) ku sneeze.
 
Mkuu ni kweli huwezi piga chafya macho yakiwa wazi lazima yafumbe.

Kugundua ni shida kwa sababu kitendo chenyewe cha kupiga chafya udumu kwa sekunde chache mno ambapo mpaka unamaliza na macho ufunguka hivyo unashindwa jua kama ulifumba.

usinganganie taarifa za internet,so kila unachosoma kwenye internet ni sahii.

unaweza kupiga chafya bila kufumba macho,ila kwa baadhi ya watu zile chafya Kali unajikuta umefumba macho.
 
usinganganie taarifa za internet,so kila unachosoma kwenye internet ni sahii.
unaweza kupiga chafya bila kufumba macho,ila kwa baadhi ya watu zile chafya Kali unajikuta umefumba macho.
Kwani tendo la chafya lina last kwa sekunde ngapi?.
 
Back
Top Bottom