SoC02 Dondoo kuhusu Forex kwa wasioijua kabisa

Stories of Change - 2022 Competition

GoJeVa

Member
Sep 15, 2021
41
59
DONDOO KUHUSU FOREX KWA WASIOIJUA KABISA.

Katika andiko hili, kwanza kabisa inabidi tujue maana ya Forex. Je, Forex ni nini?


Forex ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni. Neno ‘FOREX’ ni kifupisho cha maneno mawili ambayo ni ‘FOR’ ikimaanisha Foreign na ‘EX’ yaani Exchange. Forex ni biashara halali inayoweza kufanywa na mtu yeyote, ilimradi mtu huyo akubali kujifunza kuhusu soko hilo la forex.

Swali la pili tunalopaswa kujiuliza ni kuwa katika soko la forex Je, ni bidhaa gani au ni nini huwa kinafanyiwa biashara?

Katika hii biashara ya forex, fedha ndio kitu kinachofanyiwa biashara. Hivyo ili kufanya biashara hii ni lazima uwe na fedha ambayo ndio huitajika katika mzunguko wa soko hili la forex. Unapofanya biashara hii, huwa unauza sarafu moja na kununua nyingine, au unanunua sarafu moja na kuuza nyingine. Sarafu huuzwa kupitia dalali au mchuuzi (Broker), na huuzwa na kununuliwa katika jozi(pair) mfano euro na dola ya marekani(EUR/USD) au paundi ya kiingereza na yen ya kijapani(GBP/JPY).

Tofauti na masoko mengine ya kifedha kama Soko la Hisa la New York, Soko la Forex halina eneo la kawaida au eneo linaloonekana kama masoko ya kawaida. Soko la forex linafanyikia mtandaoni na hufanyika kwa masaa ishirini na nne(24). Hivyo ili kufanya biashara hii, unahitaji kompyuta, kasi nzuri ya mtandao na mafunzo yanayojitosheleza juu ya hii biashara ya forex.

Katika soko la forex, fedha au sarafu maarufu zinazofanyiwa biashara kwa kiasi kikubwa ni kama ifuatavyo;

ALAMA YA SARAFUNCHI YENYE SARAFU JINA LA SARAFUJINA LINGINE
USDUnited StatesDollarBuck
EUREuro membersEuroFiber
JPYJapanYenYen
GBPGreat BritainPoundCable
CHFSwitzerlandFrancSwissy
CADCanadaDollarLoonie
AUDAustraliaDollarAussie
NZDNew ZealandDollarKiwi
*Sarafu katika soko la forex, mara nyingi huwa na herufi tatu. Herufi mbili za kwanza huonesha jina la nchi la sarafu na herufi ya tatu huonesha jina la sarafu husika.



SIKU NA MUDA MZURI WA KUFANYA BIASHARA YA FOREX KULINGANA NA MASAA NA NCHI HUSIKA.

Soko la forex huwa wazi na kufanya kazi kwa masaa 24, ila kutokana na utofauti wa masaa kutoka nchi moja na nyingine inabidi kujua muda mzuri wa kuingia sokoni kutokana na sarafu na nchi husika.Pia, katika upande siku ipi ni nzuri kwa kufanya biashara ya forex, Yote kwa yote, Jumanne, Jumatano na Alhamisi ndizo siku bora zaidi za biashara ya Forex kwa sababu mzunguko wa sarafu huwa juu na mzuri. Katikati ya wiki, soko la sarafu linaona hatua ya biashara zaidi. Kwa wiki nzima, Jumatatu soko huwa tuli sana, na Ijumaa inaweza kuwa haitabiriki hivyo siku hizi mbili yaani Juma tatu na Ijumaa sio nzuri sana na kama ukifanya biashara siku hizo inabidi kuwa makini zaidi. Hebu tuangalie jedwali hapa chini kwa uelewa zaidi kuhusu masaa ya forex kulingana na nchi;



JINA LA SOKOSARAFU ZA HILO SOKOSOKO KUFUNGUKASOKO KUFUNGA
SOKO LA SYDNEYNZD NA AUD01:00Am(usiku)09:00Am(asubuhi)
SOKO LA TOKYOJPY NA CHF02:00Am(usiku)10:00Am(asubuhi)
SOKO LA LONDONEUR NA GBP10:00Am(asubuhi)06:00Pm(jioni)
SOKO LA NEW YORKUSD NA CAD03:00Pm(alasiri)11:00Pm(usiku)
*Kwa nyongeza ili kufahamu haya masaa kwa ufasaha zaidi tembelea kiunganishi hiki(link), www.forex.timezoneconverter.com



KWA NINI TUFANYE BIASHARA YA HII YA FOREX?

Kwanza kabisa inabidi tufahamu dunia ya sasa ni dunia iliyoendelea sana kisayansi na teknolojia, na sisi kama nchi ambazo zinaendelea inatubidi tufunguke kiakili kukabiliana na mabadiliko yanayotokea ili mwisho wa siku tusije tukabaki gizani wakati nchi zingine zikizidi kupiga hatua za kisayansi na kiteknolojia. Inabidi tujifunze biashara hii, na kwa sasa ni rahisi kupata maarifa juu ya forex kwa sababu unaweza kuingia mtandaoni na kupata maarifa kwa lugha yoyote utakayo, biashara ya forex ina faida nyingi sana na baadhi yake ni kama vile;

1.Hakuna tozo wala kodi unapofanya biashara hii, labda tuu hela itakatwa pale unapoweka au kutoa pesa kwenye akaunti yako ya forex. Ila ukishaweka pesa kwenye akaunti yako hakuna makato yoyote unapofanya biashara hii.

2. Soko la forex la forex lipo wazi kwa masaa 24, iwe asubuhi, mchana, jioni na hata usiku. Hivyo ni rahisi kuchagua muda wa kufanya biashara kulingana na ratiba zako.

3.Kabla ya kufanya biashara baada ya kupata mafunzo, dalali(broker) anakupa akaunti ya majaribio bure(demo akaunti) ambayo utafanyia majaribio na ukiona akaunti ya majaribio imepata faida vizuri hapo unaweza kufungua akaunti halisi kwa ajili ya biashara. Inashauriwa utumie akaunti ya majaribio angalau kwa miezi mitatu kabla haujaanza kutumia akaunti halisi(real account).



AINA ZA UCHAMBUZI KATIKA SOKO LA FOREX.

Katika kuchambua soko la forex ili uweze kufanya biashara vizuri ni lazima ujue aina ya hizi chambuzi. Kuna aina kuu mbili za uchambuzi katika soko la forex ambazo ni Uchambuzi wa kiufundi (Technical analysis) na Uchambuzi wa Msingi (Fundamental analysis).

1.Uchambuzi wa Kiufundi(Technical analysis).

Uchambuzi wa kiufundi ni utafiti wa mwendo wa bei, uchanganuzi wa kiufundi unahusisha kuangalia chati na kulichambua kwa kuzingatia mbinu mbalimbali.



2. Uchambuzi wa Msingi(Fundamental analysis).

Uchambuzi wa kimsingi ni njia ya kuangalia soko kupitia nguvu za kiuchumi, kijamii na kisiasa zinazoathiri usambazaji na mahitaji. Nchi ikiwa na uchumi mzuri na hali nzuri ya kijamii na kisiasa mara nyingi inaashiria sarafu ya nchi husika kuwa imara. Vivyo hivyo nchi ikiwa na hali mbaya za kiuchumi, kisiasa na kijamii inaashiria sarafu ya nchi husika kuwa dhaifu.

Hizi ni dondoo chache kuhusu biashara ya forex, na lengo la andiko hili na kuwapa mwanga wale ambao hawajui kabisa kuhusu forex. Ikumbukwe maarifa kama haya juu ya forex yanapatika mitandaoni. Hivyo unaweza kuingia mtandaoni na kupakua vitabu na video mbalimbali ambazo zinafundishi juu ya hii biashara kwa vitendo na kwa lugha yoyote unayotaka.



AHSANTENI.
 
Napendaga sana kujua hii kitu
Ni kitu kizuri....kwa ushauri wangu inabidi ujifunze na sio kumpa mtu pesa akufanyie biashara.........hapo chini nime` attach na kitabu, ambacho nami nilianzia kujifunzia Forex. kiangalie kama kitakufaa...... pia jitahidi kutafuta maarifa mengi zaidi ili kuwa vizuri.....hicho kitabu ni kama muongozo tuu.
 

Attachments

  • Forex Godfather Elite.pdf
    3 MB · Views: 75
Ni kitu kizuri....kwa ushauri wangu inabidi ujifunze na sio kumpa mtu pesa akufanyie biashara.........hapo chini nime` attach na kitabu, ambacho nami nilianzia kujifunzia Forex. kiangalie kama kitakufaa...... pia jitahidi kutafuta maarifa mengi zaidi ili kuwa vizuri.....hicho kitabu ni kama muongozo tuu.
Hawa jamaa Ni wazuri nawajua Ila sio Kama ambacho kimekaa Kama pipsology Mar kindergarten, elementary schools,Mara pre University
 
Hawa jamaa Ni wazuri nawajua Ila sio Kama ambacho kimekaa Kama pipsology Mar kindergarten, elementary schools,Mara pre University
Sorry mkuu...kama una kitabu soft copy(leo au siku nyingine) cha hizo forex au mambo ya hisa na mengine kama hayo, tusaidie tuchangamshe vichwa.
 
Sidhani Kama Kuna kitabu Cha trading hakijawahi pita kwa macho yangu ama trading channel yyte ya YouTubers.
Yaani ilifikia ama nimefikia nikisoma mtu anachoandika ama anachoongea najua huyu Ni real traders ama mtunga vitabu aka journalists
 
Siku ukiijua hayo mavitabu yote utaona hayana maana sema yanakusaidia kufika huko. Yamenitesa mno yaani mno
Aahahhhah.......mwenyewe nakomaa nayo, ila kwa sasa nafanya na practice....kama Forex nina hadi real account.
 
Sorry mkuu...kama una kitabu soft copy(leo au siku nyingine) cha hizo forex au mambo ya hisa na mengine kama hayo, tusaidie tuchangamshe vichwa.
Vitabu vipo vingi mno sema nilivifuta ,ingia mtandaoni mbona vimejaa.
Vitabu nilivyo navyo sema wewe saivi huwezi visoma nakuona bado Ila utafika ,tafuta groups , website, trading forums Ila daa nikicheki nilipotoka nikiambiwa nianze upya sikubali. Sema uzuri elimu huwa haibiwi Jamani.
It's very painful journey sio kitoto na sahihi failure rate iwe around 95% Ni sahihi kabisa nimeekiri.
 
Vitabu vipo vingi mno sema nilivifuta ,ingia mtandaoni mbona vimejaa.
Vitabu nilivyo navyo sema wewe saivi huwezi visoma nakuona bado Ila utafika ,tafuta groups , website, trading forums Ila daa nikicheki nilipotoka nikiambiwa nianze upya sikubali. Sema uzuri elimu huwa haibiwi Jamani.
It's very painful journey sio kitoto na sahihi failure rate iwe around 95% Ni sahihi kabisa nimeekiri.
Sawa sawa mkuu....nimekuelewa, nitaendelea kufanya juhudi.
 
Sawa sawa mkuu....nimekuelewa, nitaendelea kufanya juhudi.
Yes mkuu komaa ,hii makitu Ni ngumu wengi wanaingia wanajua kesho watakuwa mamilionea ama mamilionea jamaa akiweka dola buku ama Mia ikiyeyuka anakuja kutukana mtandaoni kuwa Ni uhuni na wizi mkubwa
 
Habari yako ndugu.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo


Ahsante!!
Ahsante kwa mrejesho.....naenda kuipitia makala hiyo sasa hivi..
 
Back
Top Bottom