Trump katoa masaa 24 kwa rais wa TZ mama Samia kuomba msamaha kwa kenya na kasema hapendi mtu anaechezea kenya na asipo fanya ivyo ata sitisha misaada yote marekani anayo saidia TZ.
- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa mtandaoni kikimuonesha Rais wa Marekani Donald Trump akimtaka Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan awaombe radhi wakenya. Miongoni mwa maneno yanayosikika katika kipande hiko cha video ni;
“Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu, ninakupa saa 24 za kuwaomba msamaha Wakenya hususan Gen Z”
Uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli. JamiiCheck imebaini kuwa kipande cha video kinachomuonesha Rais wa Marekani, Donald Trump akiitaka Tanzania kuomba msamha Wakenya ndani ya saa 24 imehaririwa kwa kuwekewa sauti iliyotengenezwa kwa Akili Unde (AI).
Uhakiki kwa kutumia nyenzo ya deepfake total umebainisha kuwa 87.3% ya sauti inayosikika imetengezwa kwa akili unde (AI).
Ufuatiliaji kwa njia ya nyenzo ya Google Reverse Image Search umebainisha kuwa video hiyo inaweza kuwa miongoni mwa video za hotuba ya Rais Trump alizozitoa mwaka 2018.
Katika video hiyo pia inasikika sauti iliyohaririwa kwa akili unde (AI) ikimtaja mtengeneza maudhui wa TikTok ajiitaye Cool Kid, sauti hiyo inasikika ikisema;
“Mwisho, niruhusuni nimpongeze kijana kutokea Kenya anayeitwa Cool Kid. Kijana huyu anawapa watu ‘tips’ za bure za kubashiri (betting)”. Sauti hii inathibitisha pia kuwa sauti ama kipande hiko cha video kimehaririwa kwa sauti kwa Akili Unde na kumuwezesha mtengenezaji kuweka maneno anayoyataka.
Aidha hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa kuwa Rais Trump aligusia chochote kuhusu yaliyotokea kati ya Tanzania na Kenya ikiwemo BBC ambao nembo yao inaonekan juu kushoto mwa video hiyo.