Donald Trump afuata nyayo za Magufuli

Donald Trump afuata nyayo za Magufuli

Ukiona mtu anapenda kusikia habari za kumfurahisha mda wote ni lazima mtu huyo anaubinafsi mkubwa sana.
Na ukiona mtu anakosoa tu kuanzia january mpaka desemba ujue kuna uwezekano mkubwa anatumiwa na wenye fedha, tena mara nyingi ni fedha chafu.
 
Mkuu magazeti huongozwa na binadamu kama mimi na wewe. Uhuru huwa na mipaka popote pale duniani vinginevyo unakuwa uendawazimu.
sikubaliani na wewe mkuu hasa unaposema 'popote pale duniani'. kwa nchi za wenzetu chombo cha habari kinaparaganyika ikiwa kitakumbwa na kadhia za rushwa na ukwepaji kodi labda; siyo kuandika ukweli au uongo.
 
sikubaliani na wewe mkuu hasa unaposema 'popote pale duniani'. kwa nchi za wenzetu chombo cha habari kinaparaganyika ikiwa kitakumbwa na kadhia za rushwa na ukwepaji kodi labda; siyo kuandika ukweli au uongo.
Mimi pia sikubaliani na wewe. Wazungu huheshimu faragha za watu, ndio maana vipo vyombo vya habari vilivyopigwa faini kubwa kwa sababu tu ya kupiga picha watu wakiwa kwenye mambo yao binafsi.
Mjukuu wa Malkia mwaka jana aliwaambia waandishi na wapiga picha wasimfuatilie mwanae mpaka akiwa anacheza kwenye uwanja wa nyumbani.
Hakuna haki isiyo na wajibu. Hujiandiki tu eti kwa sababu ya free press, uwe na uwezo wa kukitetea kile unachokiandika pindi ukihitajika kufanya hivyo.
 
Marekani haiwezi kufuata nyayo za masikini Tanzania ila masikini Tanzania ndiye anaweza fuata za boss marekani , kuwa na akili ww usiingie humu Kwa sababu umenunuliwa kasmart phone na mjomba wako wa Namtumbo ingia jamii forums kwa sababu una hoja Ok!!!
 
Huyu maskini wa kila kitu kuanzia pesa mpaka akili unamlinganisha na Trump?
Ww una pesa gani mjinga ww, au una akili kiasi gani kuzidi watu wote acha upumbafu tena kamwambie mama yako hayo maneno kuliko kututukania rais wetu pumbafu kabisa kama huna cha kuchangia kaa kimya na kama kuna watu wana kutuma basi na wao waambie ni wapumbafu sana
 
Trump sio mnafiki amekitaja kabisa kituo cha habari cha CNN lakini rais wako yeye ni mafumbo tu ameishia tu kusema magazeti mawili bila kusema ni magazeti gani
 
wrong analysis!

Rais mteule Marekani ameonekana kufuata nyayo za Magufuli katika kuwatumikia wananchi.Rais John Pombe Magufuli ni rais anayekosa usingizi kwa kupigania maisha ya wanyonge bila kutaka kuwafurahisha baadhi ya watu.Tabia hii hata Trump anayo.

Kuna maeneo mengi misimamo ya viongozi hawa inafanana.Hii ni mifano michache..

1.KUBANA MATUMIZI
Viongozi wote hawa wameonesha nia ya kubana matumizi.JPM; ameokoa pesa nyingi holela kama safari za nje, posho, sherehe zisizo na tija na matumizi mengine holela, pesa hizi zimeelekezwa kwenye maendeleo .Trump; amezuia pendekezo la kununua ndege mpya ya rais yenye thamani ya trillion 8 za Kitanzania , pia anafikiria USA kuacha kutoa pesa kwa majeshi ya NATO.

2.UCHOCHEZI WA VYOMBO VYA HABARI
Viongozi wote hawa wanakerwa na uzushi na uchochezi wa vyombo vya habari katika nchi zao.Tumeona JPM alivyokerwa na magazeti mawili yanayohatarisha mustakabali ya amani yetu akiwa ziarani Shinyanga.Hali hiyo pia tumeiona kwa Trump alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kwa kukituhumu kituo cha televisheni cha CNN kwa kutoa HABARI za uongo na uzushi.

3.KUSIMAMIA UKWELI NA KUJIAMINI.
Viongozi wote hawa hawana unafiki wala hawafanyi kazi ili wapendwe.Mara nyingi husimamia haki na ukweli.JPM ; amejitoa kupigania maisha ya Watanzania masikini, amekuwa mkweli siku zote na wala haongozi nchi kuwaridhisha mafisadi wachache na kuwaumiza wananchi wengi.Siku zote yeye husema ukweli.Trump; yeye pia hataki ujinga amekuwa akitoa kauli zenye ukweli kwa mustakabali wa Wamarekani.

4.VIWANDA NA UWEKEZAJI
Viongozi wote hawa wana nia thabiti ya nchi zao ziwe na viwanda vingi.JPM; ameweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kujenga viwanda vingi , vile vile kuwa na mipango ya kuzuia kuingia bidhaa kuingia nchini kiholela .Trump; amepinga hatua ya wawekezaji kujenga viwanda Mexico ili wapate cheap labour na kuifanya Marekani soko la bidhaa zinazotengenezwa Mexico.

Kwa hiyo inabidi viongozi hawa wawe karibu sana kwani wote wana sifa zinazofanana katika kuwatumikia wananchi wanyonge.
 
Na ukiona mtu anakosoa tu kuanzia january mpaka desemba ujue kuna uwezekano mkubwa anatumiwa na wenye fedha, tena mara nyingi ni fedha chafu.
Na ukiona mtu anaamini kwamba kuongoza mda mfupi kwa makosa hutakiwi kukosolewa na hajui kua maamuzi mambovu ya kiutawala ndani ya saa moja tu yanaweza kuleta madhara yatakayo dumu zaid ya miaka, basi ni dhahiri kuwa mtu huyo haijui kesho yake na amedumaa kimawazo
 
Na ukiona mtu anaamini kwamba kuongoza mda mfupi kwa makosa hutakiwi kukosolewa na hajui kua maamuzi mambovu ya kiutawala ndani ya saa moja tu yanaweza kuleta madhara yatakayo dumu zaid ya miaka, basi ni dhahiri kuwa mtu huyo haijui kesho yake na amedumaa kimawazo
Na ukiona mtu anaandika bila ya kufanya utafiti wa anachokiandika ujue huyo ni sehemu tu ya jamii isiyojitambua.
 
Jua kutofautisha njaa na shibe kwanza halafu ndio uende kwenye bichwa na kichwa
 
Trump ameamua mshahara wake wa urais utakuwa dola moja.
kiongozi wetu hata ile salary slip yake aliyoahidi kuionyesha hajaitoa.
 
Back
Top Bottom