Donald Trump adondokea Pua,Matumaini Yafifia

Donald Trump adondokea Pua,Matumaini Yafifia

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Katika kinyang'anyiro cha kuwania kuwa mgombea urais kwenye uchaguzi ujao nchini Marekani, Seneta Ted Cruz ameshinda uchaguzi ndani ya chama cha Republican katika jimbo la Iowa. Cruz amemtangulia mpinzani wake Donald Trump kwa asilimia 4, akipata asilimia 28 wakati Trump aliyekuwa akipewa matumaini makubwa akiwa na asilimia 24. Kwa upande wa wagombea wa chama cha Democratic, Hillary Clinton na Seneta wa Vermont Bernie Sanders, wanachuana vikali na bado mshindi hajatangazwa. Gavana wa zamani wa Maryland, Martin O´malley amesitisha lengo lake la kugombea uteuzi huo na gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee amejitoa kwenye mbio hizo upande wa Warepublican. Tupe maoni yako.
 
Nilijua hili litatokea sijui kwa nini hakuona alama za nyakati. Acha watu wapumue sasa maana media coverage ya huyu mtu ilikuwa inakera.
 
Inasikitisha sana kuwa na watu wa aina hii....Eti nanukuu"
Donald Trump adondokea Pua,Matumaini Yafifia" .Acha ujinga ndio uchaguzi wa kwanza na bado hata Primary moja .Sasa hayo matumaini yamefifia kwa kushindwa kwa asilimia 4 katika jimbo moja tu la Iowa. ACHA UPOTOSHAJI labda ungesema Trump aanza vibaya ningekuelewa.Hata kama uelewa mdogo dont wash your dirty linen in public!
 
jimbo lililofanya uchafuzi ni jimbo dogo na wanafuatilia siasa za USA wanasema jimbo la kwanza(mara nyingi) linatowa/kuonyesha mwelekeo kiasi kwamba wagombea walioshika namba tatu kurundi nyuma hujitoa kuwaachia manguli kuchuana hivyo bado
 
fatilia mwenendo wake tangu mwanzo wa kampeni zake utamjua kuwa ana matatizo ya akili.
Mbona nafatilia kaka namuona yuko sawa,na nika toa mfano wa sera zake za ugaidi,mi naona tukubaliane tu jamaa yuko vizuri,na wewe ulikua una andika just for fun
 
Mleta mada inaelekea siasa za America huzifahamu kiundani,kifupi ushindi wa Ted Cruz ktk jimbo la Iowa haiabashiri taswira ya jumla juu ya nani atakuwa mshindi.Sifa moja kubwa ya Iowa state ni kwamba huwa inawapigia kura wale wagombea wenye misimamo mikali ya kihifadhina,sishangai Cruz kushinda kwani ndio mtu wao.Ila kuna yale majimbo muhimu kama ya Ohio,Pennsylvania, Michigan, North Carolina, Indiana, nk ambapo ndipo kumejaa viwanda vikubwa na wale voters wanaojulikana kama blue collar voters,huko ndipo upinzani utakuwa mkali sana tena nahisi utakuwa kati ya Trump na Rubio. Trump ana New York yake na Rubio ana Florida yake,haya ndio yanaitwa swing states. Hayo mengine ni tossup states tu anyone could win them.Cruz bado ana uphill task at hand to hang on in the election.
 
Mbona nafatilia kaka namuona yuko sawa,na nika toa mfano wa sera zake za ugaidi,mi naona tukubaliane tu jamaa yuko vizuri,na wewe ulikua una andika just for fun
hata alivyoaddress iyo issue ya ugaidi inaonyesha wazi hana akili timamu.
mkuu ingia google tafuta kauli mbalimbali za huyo mtu.
 
Back
Top Bottom