Donald Trump adondokea Pua,Matumaini Yafifia

Donald Trump adondokea Pua,Matumaini Yafifia

Donald Trump angeshinda ningewashangaa Sana wamarekani.Kwanza inaonekana Ameingia kwenye Kinyang'anyiro kuongezea umaarufu si kushinda.Alidanganywa na opinion polls Za vyombo vya habari na mikusanyiko ya vijana wa Chuo ambao hata hawakuwa wanamtaka Bali kusikiliza ujinga anaouongea na wengine hata hawakurudi makwao kupiga kura.Sasa anadai uchaguzi ulikuwa si wa haki kulikuwa na udanganyifu .
 
Mleta mada inaelekea siasa za America huzifahamu kiundani,kifupi ushindi wa Ted Cruz ktk jimbo la Iowa haiabashiri taswira ya jumla juu ya nani atakuwa mshindi.Sifa moja kubwa ya Iowa state ni kwamba huwa inawapigia kura wale wagombea wenye misimamo mikali ya kihifadhina,sishangai Cruz kushinda kwani ndio mtu wao.Ila kuna yale majimbo muhimu kama ya Ohio,Pennsylvania, Michigan, North Carolina, Indiana, nk ambapo ndipo kumejaa viwanda vikubwa na wale voters wanaojulikana kama blue collar voters,huko ndipo upinzani utakuwa mkali sana tena nahisi utakuwa kati ya Trump na Rubio. Trump ana New York yake na Rubio ana Florida yake,haya ndio yanaitwa swing states. Hayo mengine ni tossup states tu anyone could win them.Cruz bado ana uphill task at hand to hang on in the election.
maelezo safi mkuu
 
Back
Top Bottom