Don Williams V/S Kenny Rogers

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,822
3,651
don william.jpg
kenny rogers.jpg

Napenda muziki. Kuanzia reggae, blues, kwaito, hip hop, zouk hadi rhumba kote huko nimepita ila ladha ninayoipata nisikilizapo muziki wa country sijawahi kuipata kwenye muziki mwingine wowote ule. Akili, ubunifu, juhudi, maarifa na utulivu unaotumika katika kuandaa nyimbo za country huzifanya ziwe na upekee wenye kusuuza nafsi na roho lakini pia kuipa akili fursa ya kutafakari na kuchanganua mambo katika upeo wa juu zaidi.

Leo nimemkumbuka gwiji wa muziki huo, hayati Don William. Ile sauti, lile gitaa, yale mashairi huwezi kuvipata popote pale zaidi ya kwenye muziki wa Don William. Nimepitia rekodi zake kuanzia Desperately, I am in love, We got love halafu nikamalizia na I believe in you, hakika sijajutia kuwa shabiki wa huyu jamaa. Kabla sijamvisha taji la ufalme wa muziki wa country masikio yangu yakasikia mdundo murua ikabidi nisubiri kidogo, ulikuwa ni wimbo uliopangiliwa vyema, kila chombo kikisikika kwa uzuri kutoka kwake Kenny Roggers ngoma ikiitwa gambler. halafu ukafuata mfululizo wa nyimbo kutoka kwa fundi huyo kutoka Texas, nikaisikiliza coward of the county kisha Luccile halafu we have got tonight, nikamalizia na lady. Kila kitu kilikuwa sawa sawa yaani very perfect.

Hawa jamaa wawili wana mchango mkubwa katika muziki wa country ila nimeshindwa kujua nani nimpe taji la ufalme wa muziki huu maridadi. Haya wakongwa niambieni nani funsi zaidi ya mwenzake baina ya hawa manguli wawili.

Kama ulikuwa hujui; Wimbo maarufu wa I will always love you kwa mara ya kwanza ulitungwa na kuimbwa na mwanamama Dolly Parton ukiwa katika mahadhi ya country mwaka 1974 ndipo ukaja kurudiwa na mwanamama Witney Houston mwaka 1992. najua Witney aliweka nguvu kubwa sana katika matumizi ya sauti ila ukitaka kuona hisia zinazopaswa kuwekwa kwenye huo wimbo msikilize Dolly Parton.

CC
Copenhagen DN Heci Consigliere mng'ato elmagnifico Mr Miller Nahirat
MBITIYAZA ArD67 Inanambo kilambimkwidu kiumbe kipya bombei_safaya Shepherd kidadari Kyalow
 
Nampenda zadi Don Williams. Ila naona Kenny Rogers umemuonea.

Napata zaidi wasiwasi kwamba humfahamu kwa karibu Kenny Rogers ambaye alishiriki pia kuimba wimbo wa We Are The World.



Huu wimbo uliandikwa na Brother Gibbs yaani Bee Gees ili aimbe Diana Ross. Diana akawa anakwepakwepa na mwisho wakaona wawape Kenny Rogers na Dolly Parton ambao waliufanya kazi nzuri sana.

2. Don't fall in love with a dreamer.

3. Lady, Something inside so strong, Lady etc.

Don Williams? Mhhhh.... huyu jamaa apumzike kwa amani ila alikuwa anaimba.



Kenny rodgers ni nyimbo tatu tuu ndio maarufu The Gambler, coward of the county, lucine and island in the stream fet dolly parton

Consigliere
 
Kenny Rogers aiseeee... Why? Because ever since I was a kid. Someone really close to me, who paid my fees, kanilisha and even kanipeleka nje kula bata tu, used to play only Kenny Roger's songs in his Land Cruiser 🤣

This is what made me love Kenny Rogers. Unajua sometimes hata kama hupendi singeli, ila mama yako akiwa anapiga nyimbo za msagasumu daily. Itakuja miaka utazipenda tu. Because it reminds you of your mom.

Don Williams is a great singer, but Kenny Rogers gets my vote here. Hivi kwanza mmeusikia 'Buy me a rose'??? I wish all women were like this. Au 'Loving arms'??? And the famous 'Gambler'? All songs touch my life and am sure yours too-whoever is reading this.

-callmeGhost
 
Nadhani sio lazima wakati wote tuwe na mshindi mmoja,leo naomba niseme kwenye country kuna washindi wawili nimeshindwa kuchagua asee.
hahaha pole kwa kupata wakati mgumu chief, kweli unonekana Country music unaipenda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom