snowhite
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,422
- 25,320
yani wala si uongo!Asante sana kwa kupanua definition ya domestic violence. Nadhani masuali yangu ya mwanzo yanahusika pia hapa ingawa hatuwezi kupata jibu la uhakika hapa, but we can still share thoughts: Kwanini victims hawajitokezi? Kwanini pepetrators wanafanya hivo na ni kitu gani sisi kama jamii tunaweza kufanya ili kupunguza domestic violence around us?
Ni muhimu sana victim asiwe ndio responsible kwa yalio mtokea. Kuna familia ambapo binti anabakwa na wanaishia kumtuma hyo huyo binti aende boarding school au kijijini kwa kufunika ile aibu. Inakua as if she is punished for what people did to her. Hili linawafanya watoto wengine ndani ya faamilia wakae kimya pale wanapokutana na tatizo lile lile.
linapotokea hilki kwenye familia kila mtu anabaki kujali image ya familia ile kwa walio wazunguka!
muathirika anabaki na kidonda kikubwa maishani!
tusibaki kushangaa tu kuwa kwanini siku hizi hakuna mapenzi
watoto wanakua kwenye mazingira gani?
binti aliyebakwa na babake/kaka/mabinamu na shemeji au kijana aliyenyanya sika kijinsia na mama mwenye nyumba/mjomba /kaka/babu huyu anawezaje kupenda ukubwani!
nani anakua akishuhudia mamake anaburuzwa mtaani akiwa uchi kwa kipigo kutoka kwa baba anaweza kuipa thamani halisi ndoa!
so ni swla pana sana kwa kweli!
hakuna aliye tayari kuwajibika pengine wala hatujali kuwa ni tatizo mtambuka!tunabaki ah shauri yao!