Dola yafanywa mbadala wa shilingi Dar es salaam! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dola yafanywa mbadala wa shilingi Dar es salaam!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mama Brian, Aug 15, 2010.

 1. Mama Brian

  Mama Brian JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 2. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii ni serious issue tena inaathiri makampuni ya kigeni. Unaweza ukafikiria ni rahisi lakini hakuna muwekezaji anayeweza kushawishika kuja Tanzania kuwekeza wakati shilingi inaporomoka. Km atakuja ni lazima awekeze kwenye foreign currency maana at the end of the day, income yake inakuwa repatriated in foreign currency. Sasa ukiwekeza kwenye Tsh inamaana ukiconvert siku ya mwisho unapata pesa ndogo. Ingawa the other side of the coin ni kwamba weak currency inasaidia exportation, lakini kiuhalisia hatuna cha kuexport. Overall lazima kuwepo na balance otherwise hali itakuwa mbaya saana kwenye importation.
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Viongozi wetu wanajipendekeza mno kwa haya mabaka uchumi! sijui tutafika lini nasisi tukawa na nguvu ya kujivunia vyetu! everytime I see our leaders are "Don't care people". Mimi nashangaa sana napoona watu wanachekewa tu kwa kisingizio cha soko huria, wakati wanaiba.

  Soko huria ni project ya nchi tajiri kutuibia kirahisi sisi wenye mizee iliyojaa kila sehemu haitaki hata kujifunza wala kusoma alama za nyakati.
  Anyway, Ndulu naye anasema ni soko huria, anawataka wafanyabiashara kuacha kupandisha hovyo, nani atakusikia wakati ndo wenye chama, ndiyo hao hao mankutana nao kwenye makasino mnapewa moja baridi moja moto! mnacheka tu. I know this guys are F....ed. Hawana uchungu na nchi, nchi zingine vijana ndo wamejaa maofisini wanauchungu na nchi zao, lakini sisi wazee ndo wamejaa maofisini (hawana jipya) wakati jua lao linazama ndo wanakimbia kimbia.
   
 4. k

  kiuno Member

  #4
  Aug 15, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nipo nje, kuna kitu nilikuwa nataka kutoka tanzania,nikamwambia ndugu yangu naomba niulizie bei, nilishangaa nilipotajiwa bei ya dola baada ya shilingi,hatuna utamaduni wowote na bado watu wachache wenye nguvu wanaacha shiingi pia ipotee, na ule mlima wakenya wameshauchukua,sasa ukitaka kuielezea tanzania kimataifa sijui utajielezeaje ikiwa hata shilingi kumbe haipo.
  ni ulimbukeni tu wakuiga kila kitu.yangu macho na masikio,sasahivi tutatengenezewa noti ya laki moja
   
 5. D

  Dick JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani tunalisingizia soko huria. Hapo BoT kuna uzembe ktk kuweka na kusimamia sera ya matumizi ya sarafu za nje (foreign currencies).

  Chukua mfn wa Afrika Kusini (A. K), wana soko huria lakini mgeni na hata mwananchi yeyote haruhuisiwi kutumia sarafu ya nje. Anachofanya mgeni anaenda benki/bureau de change/hotel anabadili fedha zake ili apate Rand (sarafu ya A. K) ndipo afanye ununuzi wowote. Wananchi wa pale hapokei sarafu ya nje, yuko tayari kuvunja biashara kuliko apokee sarafu ya nje.


  Kwetu sisi imekuwa ni soko holela badala ya soko huria kutokana na uzembe wa usimamizi wa wenzetu wa BoT.
   
 6. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tanzania Dollar yenyewe imekua ni bidhaa (commodity) kila mtu anataka kuinunua
  ndio kwa maana shillingi inateremka kwa kasi, kama dollar inakuwa kidogo katika soko
  na kama sokoni kuna dollar nyingi shillingi inapanda thamani kama theory ya supply and
  demand ilivyo. na mara nyingi dollar inakuwa kidogo katika soko ndio kwa maana shillingi
  haipandi thamani.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Thamani ya shilling kuwa chini against USD sio kitu kibaya mara zote. Wachina wanalaumiwa na wamerekani kwa 'kushusha thamani' ya ya currency yao artificially! Thamani ya sarafu yetu inapokuwa chini, tunakuwa na advantage kubwa zaidi ya kuuza bidhaa zetu nje! Tatizo letu kama taifa ni kununua zaidi kutoka nje kuliko vile tunavyouza.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Ukisoma hiyo document, ukaona comments za governor Ndulu, utajua kwa nini shilingi inashuka thamani kila siku.

  Governor mzima hajui hata "realization principle" ya accountancy. You don't count your eggs until they are hatched.

  Na huyu ndiye governor wetu profesa aliyepata kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa ya fedha, watendaji wengine wa chini yake ambaye hawajapata elimu na exposure kama yake ?
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Aug 16, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa uchumi wa Tanzania ni tegemezi sana kiasi kuwa tunavyouza nje ni kidogo sana kuliko tunavyonunua kutoka nje; watu wa kawaida hawawezi kabisa kuiona ile advantage itokanayo na kuuza nje kwa vile wanaumia kwa kununua hivyo viavyotoka nje. Ni kwa vile wafanya biashara wetu ni waroho sana, lakini wangekuwa na utaratibu wa kuweka beil kulingana na gharama halisi, basi bidhaa chache zilizoko za kiTanzania zingekuwa zinapata soko bora sana hapa nyumbani kwa vile zingeuzwa kwa bei ya chini sana kulinganisha na zile zilizoingizwa kutoka nje. Lakini utashangaa kuona kuwa sabuni za kiTanzania nazo leo zinauzwa kwa bei karibu sawa na sabuni zinazotoka China pamoja na kushuka kwa shillingi
   
 10. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  China fedha yao wameipeg chini kwa sababu wanajenga uchumi unaolenga zaidi export, kwa hiyo currency yao ikiwa chini watauza zaidi. sisi hatuna cha ku-export bali waTZ leo tunashindana kwenda china na Dubai kuleta mazagazaga ndomana kwanza currency yetu inashuka na pili inaposhuka inafanya maisha yetu yawe magumu zaidi sababu hayo mazagazaga yanaongeka bei kila kukicha. kibaya zaidi ni pale wawekezaji wanapotumia ujinga wetu na kufanya dumping nchini kwetu. hakuna haja supermarket za dar kuuza matunda tuka SA wakati ya kwetu yanakosa soko lakini pia waTZ hatujali kununua tunda imported wala hatujui kuwa tunachangia ugumu wa maisha yetu. labda JF tuanze kampeni sasa ya ku-promote bidhaa za ndani km matunda ambayo yapo na tukashifu kununua imported hadi vile vinavyotengenzwa bongo
   
Loading...