Dola moja itakua sawa na tsh.2500/= miezi mitano ijayo

Dola moja itakua sawa na tsh.2500/= miezi mitano ijayo

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,852
Reaction score
35,620
Naomba.
hizi kumbukumbu mzikumbuke kua baada ya miezi mitano mbele shilingi ya Tanzania itaporomoka kwa kiwango kikubwa kama serikali haitochukua hatua za makusudi za kulinda pesa yetu.
Naiomba serikali ijitahidi kujenga mahusiano mema na wafadhili wetu wakuu na waangalie kabla ya kutamka chochote wajue tuko kwenye rada za mabeberu ambao kimsingi hatuna ubavu na hatujaweza kuwashinda kwa lolote.
Busara ni muhimu zaidi hasa wakati huu ambao wafadhili wakiwa wameanza kuzua vikwazo iwe taa kwetu kwani hata kwingine ilianza hivi hivi.
 
Hata iwe 5000 it doesn't affect me anymore, ntakupa mbinu ya kuyapuuza hayo mambo,

Serikali ikishindwa kutoa elimu bora mwanao mpeleke private

Serikali ikishindwa kuboresha public Transportation nunua ki passo chako,

Ikishindwa kuleta umeme, nunua solar
Ikishindwa kuleta maji nunua Sim Tank
Ikishindwa kupunguza mfumko wa bei chenji hela za madafu , weka hata nje ya nchi hela yako,

Kwa sisi tunaolipwa currency moja na Trump, Teresa May, Pep Guadiola, Mourinho, Obama ,Nyani Ngabu

Hakuna mshtuko endeleleeni na madafu yenu
 
USD 1 = Tsh 2500.
Umepuyanga mkuu.
USD 1 = Tsh 2780.19/=
Baada ya mwezi 12 tu, yaani hapa namaanisha February tunaifikia hiyo rank.
 
Wacha uoga mkuu, sisi ni sembe kantiri na tun rasilimali nyingi sana hata korosho tunanunua wenyewe. Utakua mchochezi wewe na huna uzalendo na nchi yetu.
Na jeshi letu lipo imara tena tunagari 75 zilizo imara na rais amezikagua. Hao wazungu watuchokoze waone tusipowatumia watu wasiojulikana, au tuwatume makomando wetu wale wawezao kuvunjia tofali kichwani.
Unacheza na kichaa wewe.
 
Wacha uoga mkuu, soso ni sembe kantiri na Tina rasilimalo nyingi sana hats korosho tunanunua wenyewe. Utakua mchochezi wewe na huna uzalendo na nchi yetu.
Na jeshi letu lipo imara tens tunagari 75 zilizo imara na rais amezikagua. Hao wazungu watuchokoze waone tusipowatumia watu wasiojulikana. Au tuwatume makomando wetu wale wawezao kuvunjia tofali kichwani.
Unacheza na kichaa wewe.
uwe unakagua maandishi maana Tecno ina kichaa
 
Mnazungumzia dola hivi mafuta hamuoni yanavyopanda kila siku? Huku niliko petrol 2500 sijui huko kwenu wadau dah. Hali inatisha
 
Ngoja nika badilishe akiba yangu iwe kwenye usd maana isije fyekelewa mbali na huu uchumi wa jiwe.
 
Ni rahisi kuingiza bidhaa nchini kuliko kuuza bidhaa zetu nje,na tukiuza mara nyingi inakuwa ni Bidhaa ghafi.Tumekuwa dampo la bidhaa za nje nzuri na mbaya,ilhali kuna ugumu mkubwa,usumbufu na ukuritimba mwingi pale mfanyabiashara wa kitanzania anapotaka kupeleka bidhaa yake kuuza n nje,serikali haina policy nzuri za kuvutia na kurahisisha export trade kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo,ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya bidhaa zetu huko nje.pamoja na kutoa taarifa na update ya bei ya bidhaa mbalimbali kwenye soko la kimataifa.
 
maaninah serikari itamke vyovyote vile ipendavyo

Msipoangalia mtakuja kupapaswa wowowo na hao mnaowaita wafadhili, WANAWAFADHILI NINI HASA? NA JE NI LAZIMA KIFADHILIWA? KAMA NDIVYO WAO WANAFADHILIWA NA NANI?

Acheni mawazo ya kfala wabongo, ina maana hata ile historia ya form two ya kusema misaada ya wazungu ina lengo la kutuufanya tuwe wategemezi wabongo hamjaielewa?

Si tanzania pekee hata mke wako akipewa bure kitu na mangi dukani usichekelee jua shida ipo
 
Hata iwe 5000 it doesn't affect me anymore, ntakupa mbinu ya kuyapuuza hayo mambo,

Serikali ikishindwa kutoa elimu bora mwanao mpeleke private

Serikali ikishindwa kuboresha public Transportation nunua ki passo chako,

Ikishindwa kuleta umeme, nunua solar
Ikishindwa kuleta maji nunua Sim Tank
Ikishindwa kupunguza mfumko wa bei chenji hela za madafu , weka hata nje ya nchi hela yako,

Kwa sisi tunaolipwa currency moja na Trump, Teresa May, Pep Guadiola, Mourinho, Obama ,Nyani Ngabu

Hakuna mshtuko endeleleeni na madafu yenu
nikisha nunua simtank what next?
 
Back
Top Bottom