Cognitivist
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 1,057
- 2,092
Hi, Great Thinkers,
Ndugu zanguni kuna binti mmoja ambaye ni rafiki yangu wa kawaida na nimefahamiana nae hivi karibuni, amenieleza kisa cha mtoto wake nikaingiwa na huruma sana nikakaona hebu niwashirikishe great thinkers ili kulipatia ufumbuzi jambo hili
Ishu yenyewe ni kuwa huyu binti alijifungua mtoto wake wa kike ambaye ndie first born almost miaka miwili na nusu iliyopita. Mtoto akaendelea kukua vizuri lakini kwa bahati mbaya mtoto huyu kila alipokuwa akifanyishwa mazoezi ya kukuaa alikuwa akilia sana kuashiria kuwa anapata maumivu makali sana.
Hali ikaendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu ndipo ikabidi apelekwe hospitali, majibu ya vipimo yakaonyesha mtoto ana tatizo kwenye central nervous system, kwa maana kwamba ana tatizo kwenye uti wa mgongo na upande flan wa brain unaohusika na kukontrol movement
Ushauri wa madaktari ukawa hakuna dawa ya moja kwa moja ya kutibu tatizo hili isipokuwa ni kwa kumfanyisha mazoezi ili kuactivate hiyo sehemu ya brain iliyo dormant, lakin sasa ni takribani miezi sita but no changes.
Lakini nilipotaka kujua nini chanzo cha tatizo hili, alinieleza kuwa ameambiwa na daktari tatizo hili lilisababishwa na mtoto kuchelewa kulia mara tu baada ya kuzaliwa (hili litalihoji siku nyingine, uhusiano uliopo kati ya kulia kwa mtoto baada ya kuzaliwa na maendeleo yake kiakili)
Ndugu zanguni katika mazingira kama haya, naanza kuona kama vile huenda mtoto huyu ndio akalemaa moja kwa moja na kuwa kilema.
Great thinkers naomba msaada wenu ni kwa namna gani tunaweza kumsaidia huyu binti pamoja na mwanae, kwa upande wangu nachelea kuamini kuwa hakuna dawa ya tatizo hili apart from mazoezi. GT allow me to present.