Dogo mdadisi

SI unit

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,953
766
Dogo wa miaka 3 alikua klinik na mama yake, mara akamwona mama mjamzito anasubiri kwenda kwa daktari. Kwa kuwa yule dogo ni mdadisi akamfata yule mjamzito, mazungumzo yao yalikua hivi:
Dogo: Mbona tumbo lako ni kubwa hivyo?
Mjamzito: Kuna mtoto.
Dogo: Mtoto yupo ndani ya tumbo lako?
Mjamzito: Ndio mwanangu.
Dogo: Ni mtoto mzuri eeh?
Mjamzito: Ndio, tena mzuri sana, kama wewe.
**
Dogo huku akistaajabu, akaendelea kuuliza
:
:
"Sasa kwa nini ulim'meza?"
 
kwa sababu ni mzuri, hata wewe ulivyo mzuri mama ako atakumeza siku moja, umesikia eeh
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom