Dogo ana Division 1.7; Mambo ya computer aende chuo gani?

Bac3

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2016
Posts
392
Reaction score
437
Nina mdogo wangu wa kiume kapata dvn 1.7 sasa hatujajua achague chuo gani. Yeye hataki kwenda advance..

Anapenda mambo ya computer ila sasa hatujui computer imegawanyika vipi na ipi ni nzuri zaidi.

Pia je mwanafunzi anayetokea o level anaweza pata mkopo?

ipi course nzuri ya computer?

Tunatanguliza shukrani
 
Mwambie aende DIT HAKUNA PENGINE ZAIDI YA HAPO LA MUST ILA SIIJUI.


Akssome diploma ya IT, AKIJA KWA DEGREE ASOME COMPUTER SCIENCE
 
Diploma unapata muhimu ufaulu vizuri uombe mapema basi, aende DIT ni nzuri Sasa UNATAKA MUST kijijini wakati hiyo ni tech.


Arusha tech ni nzuri Kwa WATU WA archtecture
sawa mkuu...

unajua haya mambo hatuyajui..wanasema computer imegawanyika vipengele...ila dogo yeye anapenda mambo ya computer...kipengele kipi kina soko zaidi?

na enzi zetu tulkkuwa tunajaza choices zaidi ya moja..sijajua sasahiv wanachagua vip.....nimshauri ajaze vip?
 
Mkuu cozi za diploma Kwa compyuta ni IT,ICT, INFORMATION SYSTEM, DATABASE ADMINISTRATOR, NETWORKING, TELECOMUNICATION LAKINI ZOTE ZINAINGILIANA HAKUNA HATA MMOJA HAPO JUU ASIYEJUA COMPUTER.

UKISOMA COMOUTER BONGO UNA TOFAUTI NA MEDICAL DOCTOR ASIYE NA SPECIALIZATION.


AKIFIKA LEVEL ANAHITAJI DEGREE ASOME COMPUTER SCIENCE NDO INACOVER VITU BINGI.

ALIYESOMA CS ANAWEZA APPLY POPOTE KIAJIRA.
 

asante mkuu
kwa hiyo kuspecialize mpaka afike degree? diploma anasoma tu general computer tu?
 
Ni bora zaidi kwa sasa kupiga diploma ili kuokoa muda saizi watu waajiri wengi wanataka watu wa kazi sio watu wa kusimamia kazi otherwise kama anataka akimaliza degree awee na wazo pamoja na mtaji ajiajiri chapu chapu
 
Kama anataka kuwa mnyama kwenye practical ATC, kama anataka kumeza prac kidogo
na theory sana aende DIT na kama anataka GPA safi na afaulu kiulaini aende MUST
 
Kama anataka kuwa mnyama kwenye practical ATC, kama anataka kumeza prac kidogo
na theory sana aende DIT na kama anataka GPA safi na afaulu kiulaini aende MUST
mkuu wewe kwa computer angelikuwa dogo lako au mwanao kwa uzoefu wako na kulingana na soko...asomee course ipi ya computer na mkopo anapata?? pls jibu hayo
 
mkuu wewe kwa computer angelikuwa dogo lako au mwanao kwa uzoefu wako na kulingana na soko...asomee course ipi ya computer na mkopo anapata?? pls jibu hayo
Computer science tu hamna kingine japo ningekuwa mimi saivi ningeenda uhasibu, make huku uwe engineer, daktari nk. mhasibu lazima akukalishe. Labda kama ana maidea ya kutengeneza kampuni yake sio kuajiriwa au aajiriwe sio bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…