Dogo amenikera mpaka nahisi kumchukia mazima

Yani huyo ni kama rafikiyangu ananikeraga sana Yani hata umkopeshe pesa siku ya kumkumbusha akulipe utasikia afadhali wewe hauna watoto hauna madeni sijui nn ananikera nae kenge yule 😀😀😀

Wakati mwenzie Huwa najikaza tu napambana anaona km ninazo
 
Watu Kama mtoa mada ni wagumu Sana kuishi nao
Mambo simple tu wamepandwa na jazba Kama JPM
Hisia zako ungezieleza kwa mdogo wako ili ajue amekukwaza vipi na kumpa ushauri akuchukulie vipi kwenye situation Kama hii then maisha yaendelee
Yaani na hili dogo livunje undugu wenu, upendano wenu? Kushikamana kwenu? Kusaidiana kwenu?
Na je matukio ya wanandugu Kama ya kuibiana pesa, kuibiana mke, kufichuliana Siri mzito, kutukanana, kudhalilishana, kugombania mirathi utaipokeaje?

Hizi roho nyeusi mnazitoaga wapi, wakati Mungu kaumba roho nyeupe tupu?
 
Kuna connection Fulani Kati ya watu wawili ambayo Ni yakipekee Kila familia iyo ipo tu, mwenzako amekuamini na anaithamini hiyo bond yenu
 
Ipo hivi, kuna mdogo wangu mtoto wa mama mkubwa kaolewa Arusha, sasa akikwama mambo ya hapa na pale huwa namsaidia maana tumezoeana sana kwahiyo haonagi shida kunishirikisha akikwama.

Sasa kilichonikera ni kwamba alinipigia simu akaomba nimsave kiasi fulani hivi, nikamwambia kwasasa nipo mbaya sina kitu.

Nikamuuliza kwani hujamuomba kaka j akusaidie? Maana huyu ndo kaka yake wa damu, aisee alichojibu sasa, akasema kwamba si unajua tena kaka j anafamilia yake anaihudumia, mtoto mke wake. kwahiyo siwezi kumuomba ntamharibia mipango yake.

Aisee nikawaza kwahiyo Mimi ambaye sina mke ndo fala ni za kuchota tu na bado namuwaza vibaya mno. Halafu mbaya zaidi ananiforce kwamba nitumie mbinu zote nimtumie hiyo hela ana shida ya muhimu sana.

Daaaaah simmalizi kabisa kenge yule
bro hii nikawaida sana sema wewe una akili ndogo sana na unaroho mbaya sana maana ulichoambiwa hicho ni kawaida sana na kama kweli umemuchukia kwa hicho ukija oa utakuja gombna na ndugu zako wote maana wanawake kama mme anakili kam zako hizo atakugombanisha nawandugui wote
 
Hapo ndo kunatokeaga sintofahamu watu undugu au urafiki unakufa bila sababu,

Kwa vipimo vyako unaona kakosea na kwa vipimo vyake anaona yuko sawa ila wewe umemind na humwambii ( kinyongo), embu kunjua moyo kama mmezoeana kama ulivyosema ongea nae straight forward kama hujapendezwa basi yaishe kuilete humu nako haisaidii wakati muhusika hamjayamaliza.
 
Mtu ukiwa umefulia unakua na mahasira ya kijinga tu.
Hicho ndicho nikionacho kwa mleta mada...
 
Ipo hivi, kuna mdogo wangu mtoto wa mama mkubwa kaolewa Arusha, sasa akikwama mambo ya hapa na pale huwa namsaidia maana tumezoeana sana kwahiyo haonagi shida kunishirikisha akikwama.

Sasa kilichonikera ni kwamba alinipigia simu akaomba nimsave kiasi fulani hivi, nikamwambia kwasasa nipo mbaya sina kitu.

Nikamuuliza kwani hujamuomba kaka j akusaidie? Maana huyu ndo kaka yake wa damu, aisee alichojibu sasa, akasema kwamba si unajua tena kaka j anafamilia yake anaihudumia, mtoto mke wake. kwahiyo siwezi kumuomba ntamharibia mipango yake.

Aisee nikawaza kwahiyo Mimi ambaye sina mke ndo fala ni za kuchota tu na bado namuwaza vibaya mno. Halafu mbaya zaidi ananiforce kwamba nitumie mbinu zote nimtumie hiyo hela ana shida ya muhimu sana.

Daaaaah simmalizi kabisa kenge yule
Unatafuta sababu tu za kumkataa, huna haja ya kuanzia mbali au kuzunguka sana, we mkatae tu yaishe.
Hata wewe ukijakuwa na familia hatakuomba msaada pia coz utakuwa na majukumu muhimu, mbona kakujibu poa sana?
 
We pumbavu kabisa hela niitafte kwa jasho langu alafu iombwe kidharau hivyo, yy alikua ana maana gani kusema za kaka yake zina kazi, inaonekana bado unalelewa na mzee wako ww
bro hii nikawaida sana sema wewe una akili ndogo sana na unaroho mbaya sana maana ulichoambiwa hicho ni kawaida sana na kama kweli umemuchukia kwa hicho ukija oa utakuja gombna na ndugu zako wote maana wanawake kama mme anakili kam zako hizo atakugombanisha nawandugui wote
 
Mtu ukiwa umefulia unakua na mahasira ya kijinga tu.
Hicho ndicho nikionacho kwa mleta mada...
Kufulia hakuhusiani na kudharau changu mkuu, mbona mara nyingi sana nimemsaidia wala sikuwahi kuwaza, iweje aseme za kaka yake zina matumizi? Mimi hata kama sina mke ila hela zina matumiz
 
Unatafuta sababu tu za kumkataa, huna haja ya kuanzia mbali au kuzunguka sana, we mkatae tu yaishe.
Hata wewe ukijakuwa na familia hatakuomba msaada pia coz utakuwa na majukumu muhimu, mbona kakujibu poa sana?
Mnarahisisha kwa sababu sio nyie, ila hata wewe ukiambiwa hio kauli lazima umind, hela ngumu mazee
 
Komentini chap chap kabla hawajaja mabinti wanao omba hela wakaja kuchafua gazeti kuwa mwamba ameshindwa kujiongeza
 
Back
Top Bottom