Does bio-fuel replace food production in Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Does bio-fuel replace food production in Tanzania?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Omugasi, Jun 19, 2009.

 1. O

  Omugasi Member

  #1
  Jun 19, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu hilo liko wazi. Ila wimbo huu unaonekana kutokuwa na maana hasa kwangu kwa viongozi wetu kugawa ardhi nzuri yenye rutuba kwa wageni( eti wawekezaji) kuja kupanda mazao ya mafuta kama Jatropha.Maeneo mengi ya rutuba kama kisarawe na bagamoyo wamepewa 'eti wawekezaji' waje kuvuna mafuta huku mlala hoi akiwa amefukuzwa kwenye maeneo hayo.
  Nani ambaye hataniambia huu ni ukoloni wa 'pili' tena wa aina yake. Kwani walivyokuja mwanzo si walitaka ardhi na tukawapandia mazao 'malighafi' na wakapeleka kwao.
  Inasikitisha kuona viongozi wetu hawalioni hili, wakati huku kwao ulaya walishajitosheleza kwa chakula, na kwa sababu wengi wa vinchi vyao sio vikubwa 'kwa eneo ' kama ya kwangu TZ' basi wanafanya kila hila, wanawalaghai tunaowahita viongozi.
  Nani ambaye hajui kwamba watanzania wanakufa kwa njaa? Mimea kama Jatropha inahitaji rutuba nyingi na mpaka ivunwe inachukua miaka na mbaya zaidi ikishavuwa udongo unabaki bila rutuba yeyote.Matokeo yake tutawalimia na kuwategemea kwa chakula.Labda utajiuliza ndani ya nyumba yako ulikosa chakula inakuwaje?
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaweza kuangalia mchango wangu na wengine hapa

  nakubaliana kwa kiasi kikubwa na maoni yako
   
 3. L

  Limbukeni Senior Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni dhambi kubwa sana sijui msamaha wake utapatikana vipi. Yaani watu wanakufa njaa, halafu wengine wanaendeshea mitambo na vyakula. Hii ni kufuru. Labda wahakikishe kila mtu anasaza ndio wafanye miradi hiyo. Mradi fikirivu utakaoonekana umeenda shule nionavyo mimi ni kwamba watumie vinyesi kutengenezea hiyo nishati kwani chakula kitakuwa kimeshaliwa.
   
  Last edited: Jun 20, 2009
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Wala si dhambi mkuu. Kwani tangu awali ungeambiwa kuwa maharage hayaliwi si jamii ingekubali? Mbona Marekani mahindi wanalishia mifugo? tena ikafika wakati hayo mahindi wakatupa kama chakula. Nilisikia tu ugali wa yanga, i hope nilikunywa uji wake those days. suala ni kujipanga tu. tuwe na intensive agriculture wala si extensive kama ilivyo sasa. yaani kuwe na wakulima wachaache ambao hawa (tena wawe wazalendo) wanajulikana kulima na kulisha nchi. tz ina eneo kubwa sana bado. kama sahihi yangu inavyosema, our main problem is implementation and maintenance.
   
 5. O

  Omugasi Member

  #5
  Jun 20, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijui kama nitaeleweka wakuu, nikweli wenzetu huku kilimo chao kiko so intensive wakitumia sana greenhouses kuzalisha chakula kwa wingi kiasi cha kupitiliza. wanajua pia kwamba wanatakiwa wailishe dunia including Tz tangu, lakini unafikiri hiko chakula watatupa bure? na siku zote ukiwa na njaa ni mtumwa wa yule mwenye nacho. wakati mwingine sijui kwanini hatuwezi kusema hapana?? mnakumbuka wakati Mungai kipindi cha raisi Mkapa ALIFUTA masomo iliwepo la kilimo na biashara sasa ebu niambie ni matope gani kichwani tuliyonayo? vijana wengi hawafiki elimu ya juu wanaishia secondary na kwa msingi wa masomo ya kilimo na biashara wanaweza atleast kufanya kitu katika maisha yao
   
 6. O

  Omugasi Member

  #6
  Jun 20, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda niendelee kwa kueleza madhara machache ya nchi kukosa kijitosheleza kwa chakula:
  kwanza ni kuendelea kwa maambukizi ya ukimwi, mara nyingi wanaouza miili yao ni njaa inayowasukuma kwanza . fikiria mama ambaye watoto wake wanamlilia njaa atafanya nini kama sio practise of survivor sex itakayofanywa na huyo mama.
  Tuangalie pia foood insecurity na umasikini.watu hawawezi kufikiria iwapo matumbo yanaunguruma njaa.
  Watu pia wanaweza kufarakana hata kupigana kwa kukosa chakula, chunguza uswahilini utaniambia.
  mi bado niko palepale kwa viongozi wetu kugawa ardhi yetu ya RUTUBA ilimwe jatropha wakati juzi juzi wakati Kikwete akiingia madarakani ,kulikuwa na baa la njaa.Ardhi za mikoa kama ya kwetu dodoma ni kiasi ukame, basi kama wanawapenda sana hao wawekezaji wawape huko, kwani wenyewe si wameendelea watatumia inputs na kufanya irrigation huko,kuliko kuwapa maeneo kama ya Arusha yenye rutuba ya kutosha.
   
 7. L

  Limbukeni Senior Member

  #7
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i wish you will have quote my ifs and only if
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mbona Kilimanjaro wanalima Kahawa (Bukoba pia) na hawafi njaa? Nakubaliana na wewe kitu kimoja kuwa, jetropha ilimwe kwenye maeneo yasiyotegemewa kuzalisha chakula kingi. Kulima jetropha kwenye mikoa ya pwani ni upotevu wa ardhi. Waende huko Singida, Tabora, Dodoma, Shinyanga nk na watajichukulia ekari kibao bila kubughudhi mtu. Haya maeneo ya pwani nawapa pole sana kwani siku moja atakuja Rais mpya na hamu ya kuchukua ardhi na atawaondoa na hapo kugaiwa jamaa zake na Watanzania wengine. Wangelikuwa na akili hata wao wasingelikubali.
   
Loading...