Dodoso za sensa zatolewa copy Manyara

Dodoso za sensa zatolewa copy Manyara

Irqwatu

Member
Joined
Feb 14, 2012
Posts
9
Reaction score
0
Wanajamvi madodoso ya sensa huku manyara yamekwisha kiasi kwamba yametolewa copy ili kazi iendelee, my doubt ni kwamba hizi dodoso zinakwenda kwa serial number sasa kama ikitolewa copy kama 1000 inamaana serial number inajirudia mara 1000, are we serious with this task. Nawakilisha
 
mkuu we are not serious. bilion 114 zilipangwa zitumike ktk zoezi hili. ina maana chuwa na wenzie estimation zao hazikuwa sahihi hadi watoe photocopy. hizo nakala walizotoa ni batili mbele ya sheria na nawashauri wananchi wa huko wasikubali kuhesabiwa kwa dodoso ambalo ni photocopy. wanikamate km nhmehamasisha watu wasijiandikishe.
 
Hata hapa morogoro hali ni hiyo hiyo wametoa copy.....Real we are not serious!
 
Kwa uhakika shughuli ya sensa siku zote ni jambo la kitaifa na wala si la kiitikadi hivyo kuliunga mkono ni wajibu wetu sote. Lakini ni bahati mbaya sana tena sana kwa kwa mwaka huu mambo sivyo ndivyo kabisaa juu ya zoezi hili.

Nilishasema ya kwamba mazingira ilimofanyika sensa ya mwaka huu wala si ile murua na ya kirafiki hata kidogo hivyo hata takwimu zitakazopatikana mwisho wa siku kamwe HAZITOKUA ZENYE KUAMINIKA HATA KIDOGO WALA KUWEZA KUTUMIKA POPOTE KWA SHUGHULI ZA KIMIPANGO WALA KITAALUMA.

Yeyote asiyeamini hili bado basi tena.
 
Manyara kama mkoa, au manyara karibu na babati.
 
Hata gaita wametoa coppy ndo zinazotumika mda huu ninavyoongea.
Ccm hawana suala la kuchukulia umhimu.
 
Unashangaa nini sasa.....
Mimi nimetoka hesabiwa sasa hivi karani anasema kuna kaya kibao zitabaki bila kuhesabiwa.

Na zoezi lilisimama kwa siku mbili yan jana na juzi kutokana na kukosekana kwa karatasi za dodoso. Ndipo baada ya kusubiri kwa siku mbili wakaamua kutoa copy.

Mimi nimehesabiwa na karatasi zilizopigwa copy.

Karani wa sensa mwenyewe anasikitika anasema kama zoezi zima halitaongezewa muda wa wiki nzima nyingine tujiandae na data za kufoji.

Nipo Arusha.
 
Sasa hizo bil zilizoandaliwa hatuwezi kuhoji kweli? Mama yangu mpaka uchaguzi wa 2015 unakwisha waTZ tutatembelea kufuli tu.
 
NYIE MWASEMA HUKO?
Hapa hapa Dar pua na mdomo na huduma na ofisi zote
Nyumba kibao watu hawajahesabiwa pamoja na kusubiri kwa shauku kubwa olas

karani wa sensa alikuwa akipita na kuchagua nyumba kadhaa na nyingine akaziacha
ndani ya makabrasha yake alikuwa na ramani yenye majina/namba ya nyumba zinazohesaiwa hivyo zile zisizo kwenye molongo wake
katu hazikuhesabiwa mpaka hivi tunapokaribia kuwakilishwa kwa takwimu za sensa yenyewe.

Najua watu watabisha, then za eneo husika
kwa mfano ni Buguruni-Vingunguti na mfano wa karani husika alifanya shughuli yake
opposite na barabara ya kuelekea maji machafu (dampo la vingunguti)
 
kinachonikera mm makarani wamelipwa laki 5, semina na sensa yenyewe,wakati viongozi kawawezesaji kujilipa milioni 2, jamani hii kazi isiki tu,ukweli ni ngumu kiasi kwamba inje ya ukosefuwa madodoso uwezekano wa kupika data nakutoa data sizosahihi nimkubwa sana.

Sina budi kumpa pole Rais kwa kulifanya zoezi hili kama zimamoto, vifaa hakuna,ramani za 2002 ndizo wametumia! ***** mtupu.kweli kunahaja ya kuwapa wengine nchi nao wajaribu.
 
Wanajamvi madodoso ya sensa huku manyara yamekwisha kiasi kwamba yametolewa copy ili kazi iendelee, my doubt ni kwamba hizi dodoso zinakwenda kwa serial number sasa kama ikitolewa copy kama 1000 inamaana serial number inajirudia mara 1000, are we serious with this task. Nawakilisha

We are not serious......hilo mbona liko wazi kabisa mkuu!
 
Pia kuna kijiji huko yaeda chini wananchi wamewanyanganya makarani karatasi za sensa na kuzichanachana sasa hivi polisi wa mbulu ndo naona wamevaa zana za kazi kwa ajili ya kwenda huko,kazi ipo kwa kweli kwenye sensa
 
Back
Top Bottom