Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

Akumbuke tu huo ndo mji ulioweka historia ya uhai wake, ikibidi atembelee eneo la tukio kutoa sadaka na aende hospitaliya mkoa kuwashukuru madaktari na manesi, zaidi ya yote awe MAKINI.
Huyo jamaa anadai eti mwilini mwake kuna damu ya wakenya waliomuokoa na kifo. Damu anayoitambua na hospitali anazozitambua ni za Kenya na Ubelgiji tu.
Kwa watanzania anataka Urais tu.
 
Kesho tutakaza macho kuona itifaki, taratibu, kanuni, sheria na mazowea ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa yaleyale kwa CHADEMA mjini Dodoma kama ilivyokuwa kwa mwenyekiti wa CCM ambaye ni mtia nia Urais aliyowasili ktk Ofisi ya Tume kuchukua fomu

Tujikumbushe jinsi Tume ya Uchaguzi walichofanya kwa Magufuli jana :

WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati Area C Mtaa wa Makongoro.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.

#NiYeye2020
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati Area C Mtaa wa Makongoro.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.

#NiYeye2020
Mimi huwa napenda haya mafuriko na mbwembwe.
 
Hahaaa mtapata kazi sana mwaka huu kwa sababu lissu Ni mropokaji
Lissu hawezi kutofautisha maneno Kati ya kuongea na press,hadhara,bungeni au mahakamani yeye anarusha tu
Wiki ya kwanza tu ya kampeni mtajuta kumchagua lissu,mtamkumbuka Nyalandu
Kama kuna kitu ccm mmechukia ni Lissu kuteuliwa kugombea urais, yaani basi tu mnashindwa mfanye nini nafikiri hata kwenye mizani lazima mpungue.
 
Acha kuweweseka ujinga wowote atakaozungumza lisu hautazidi makauli ya hovyo ya jiwe tunayoyasikia kila kukicha
 
Tunashukuru Molemo kwa kuleta hii habari. Kuna uzito fulani kwenye kitengo cha habari cha cdm, kiasi kwamba kuna uzi humu jukwaani unaohimiza kitengo cha habari kuamka. Kuna ushauri pia kuhusu Tundu Lisu jinsi ya kufanya siasa zake bila kupoteza credibility yake. Ni vyema kama chama mkakaa na Lisu na kumfunda. Kuna baadhi ya maneno anaongea yanampotezea haiba yake.
Umesema yote
Thanks!
Chadema uongozi - mwenye masikio asikie haya
Tundu Lissu anahitaji msaada wa ushauri nini cha kusema nini cha kuepuka
Ajaribu kufocus na kuiongoza Tz na kubadili muelekeo
Mengineyo yatafuata baada ya kitimutimu hapo October 2020 Mwanahabari Huru
 
Kesho ndiyo utajua ni Nini maana ya Nguvu ya umma na kwanini Lissu ni kipenzi Cha Watanzania
Kwa nini mtengeneze mazingira ya uwepo wa nguvu ya umma?.Mgombea wa ACt-Wazalendo kachukua Fomu kwa utulivu ule ule wa jana.Fanyeni masihara,mtajikuta mnawaangalia Magufuli na Membe wakipishana kwenye majimbo huku nyie mkiwa watazamaji.
 
Hahahaha chadema bhana Kama mazuzu kesho Hakuna kaz n Sikukuu ya nane nane na pia na nyie mnaowaza lisu kushinda uchaguz huu inabid mpimwe mkojo
 
Kajifunze Kiswahili kwanza ndiyo urudi hapa
 
Kwa nini mtengeneze mazingira ya uwepo wa nguvu ya umma?.Mgombea wa ACt-Wazalendo kachukua Fomu kwa utulivu ule ule wa jana.Fanyeni masihara,mtajikuta mnawaangalia Magufuli na Membe wakipishana kwenye majimbo huku nyie mkiwa watazamaji.
Jaribuni muone
 
Huyo jamaa anadai eti mwilini mwake kuna damu ya wakenya waliomuokoa na kifo. Damu anayoitambua na hospitali anazozitambua ni za Kenya na Ubelgiji tu.
Kwa watanzania anataka Urais tu.
Ucha uongo na porojo.Acha Fitna na uzushi
 
Back
Top Bottom