Dodoma yasubiri baraka kuwa Jiji

Dodoma yasubiri baraka kuwa Jiji

Tusifanye mambo kwa kukurupuka. Nimezunguka miji yote nchini pia nchini kadhaa za Afrika ikiwemo SOUTH AFRICA. Tanzania hatuna mji wenye hadhi ya jiji. Labda Dar es Salaam japo nako kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Dodoma bado sana ila tutafika. Halmashauri ya Manispaa kwa sasa ijikite kuupanga mji.
Majiji yalitakiwa yabaki matatu tu Dar live, Mwanza rocks na Arusha kitu cha Arusha. Mengine ni matakataka na sasa imeleta tabia kila mahala watu wanashindana eti kwetu liwe jiji nalo. Huu ni upuuzi na ingewezekana tusingetangaza jiji lingine hadi 2025 walau. Tumiji twa hovyo eti ndo iwe majiji, na ndo maana jamaa wa everton waliita Dar "kijiji", sasa kama ni kijiji unafikiliaje vieneo vingine vya ajabu ajabu?
 
Majiji yalitakiwa yabaki matatu tu Dar live, Mwanza rocks na Arusha kitu cha Arusha. Mengine ni matakataka na sasa imeleta tabia kila mahala watu wanashindana eti kwetu liwe jiji nalo. Huu ni upuuzi na ingewezekana tusingetangaza jiji lingine hadi 2025 walau. Tumiji twa hovyo eti ndo iwe majiji, na ndo maana jamaa wa everton waliita Dar "kijiji", sasa kama ni kijiji unafikiliaje vieneo vingine vya ajabu ajabu?
Jamaa wa Everton wepi? Lete source K wewe lile ni Gazeti/jarida ndo liliandika na wala Siyo Everton
 
Tanga nalo ni Jiji lakini hakuna cha maana, Dodoma bado ni mji mdogo sana bora hata mji wa Moshi unastahili kuwa Jiji lakini siyo Dodoma.

Acheni siasa unajua vigezo gani vinatumika kuipa miji kuwa majiji??
 
Unatumaje vigezo vya SA?Tunavyo vigezo vyetu mkuu ndio vinavyotumika kufanya maamuzi!
Kama imekidhi vigezo na taratibu zimfuatwa kwa mijibu wa sheria ya mipangomiji ya mwaka 2007 wapewe hadhi hiyo. Wanapinga labda wasema sheria na vigezo vyetu vina mapungufu, lakini wajue mipangomiji hata kama inaongozwa za falsafa ila mazingira ya nchi au mji husika yanachangia utekeezaji wake. Kwahiyo kutaka majiji ya Tanzania yawe sawa na London, Johannesburg na maengine ya duniani, sio sahihi.
 
Naomba kujua kwanza vigezo vya kuitwa Jiji.!
 
Rais ndiyo mwenye dhamana na TAMISEMI Simbachawene anafanya nini? Acha kupotosha umma wamepeleka maombi kwa Rais siyo kwa sababu eti TAMISEMI ipo chini yake la hasha ni kwa sababu sheria za serikali za mitaa zinasema Rais ndiye atakayehusika kwenye uanzishaji wa Majiji, likija swala la kuanzusha halimashauri au manispaa hawawezi kupeleka maombi kwa Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama umezunguka nchi zote hizo, utakubaliana na mimi kuwa si Tanzania peke yake yenye majiji madogo. Mfano ni Jiji la Mzuzu nchini Malawi. Mzuzu ni city japo ukubwa wake huenda hauifikii Mbeya. Tofauti ya Mbeya na mzuzu ni kwamba mzuzu imepangwa vizuri kuliko Mbeya. Mbeya is just a big slum.
Hivi tunavyosema Mbeya jiji mawazo yako ni kwamba mpaka mwakaleli ni jiji? Dodoma ikiwa jiji unafikiri mpaka kongwa itakuwa jiji? Si kweli tunapotoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe Dodoma umefika lini mara ya mwisho? Naamini ni zaidi ya miaka 5 iliyopita ndo maana unaona hata Moshi pakubwa.Dom sasa hivi kwa ukiwa wa mji uilinganishe na Arusha na Mwanza,si Moshi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom