Dodoma yasubiri baraka kuwa Jiji

Dodoma yasubiri baraka kuwa Jiji

Tanga nalo ni Jiji lakini hakuna cha maana, Dodoma bado ni mji mdogo sana bora hata mji wa Moshi unastahili kuwa Jiji lakini siyo Dodoma.
Hujui usemalo, Dodoma kwa sasa inapaa na idadi ya watu katika manispaa ya Dodoma huenda ni mara mbili ya watu katika mji wa Moshi.
 
PICHA NO.2.jpg

OMBI la Dodoma kuwa Jiji litawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais John Magufuli ambaye ndiye mwenye Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza na wafanyakazi wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu (CDA), kabla ya kuwapangia vituo vya kazi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tamisemi, George Simbachawene alisema ataliwasilisha ombi hilo kwa Rais ambaye ndiye mwenye dhamana ya wizara hiyo.

Awali akiwasilisha ombi hilo kwa Waziri wa Nchi (Tamisemi), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi alisema vigezo vyote wamevitimiza hivyo wanaomba halmashauri ya Manispaa ya Dodoma liwe Jiji. Kunambi alisema halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imepitia taratibu zote kwa kupitisha mapendekezo katika Kamati za Ushauri za Wilaya DCC).

“Pia tayari Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) imepitisha na taratibu imekamilisha, kwa sasa mapendekezo hayo yamewasilishwa Tamisemi,” alisema na kuongeza: “Tunaomba Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma iweze kupandishwa hadhi na kuwa Jiji kwa kuzingatia sasa Makao Makuu yamekwishahamia hapa.” Akijibu ombi hilo, Simbachawene alisema kama taratibu zote zimekamilika na vigezo vipo vya kuifanya manispaa hiyo kuwa jiji, atazifuatilia nyaraka hizo na kuzipitia na baadaye kuzifikisha kwa Rais mwenye dhamana ya wizara.

Aliwaomba watendaji wa ofisi yake kama wamepashapata nyaraka za Dodoma kuwa jiji kuzifikisha mezani kwake haraka ili kuzipitia na kuziwakilisha kwa mwenye dhamana ya Tamisemi ambaye ni Rais. Tangu mwaka jana, Serikali imahamishia watendaji wake katika mji wa Dodoma ambao hadi sasa ni Halmashauri ya Manispaa, hivyo DCC na RCC imeomba upandishwe hadhi na kuwa jiji kulingana na dhamana yake kubwa ya serikali kuhamia hapo. Rais Magufuli akiridhia Dodoma kuwa jiji litakuwa la sita nchini baada ya lile la Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga na Arusha.

Chanza: HabariLeo
 
Majiji yangebaki: Dar na Mwanza tu: huko Mbeya, Arusha na Tanga wajenge miji yao na kuweka miundo mbinu ya hadhi za jiji ndipo waendelee kuwa jiji. Majiji gani barabara za vumbi nyingi kuliko za lami: mambo ya kishamba shamba mengi-watu wanalima mjini!: mifugo inadhulula mjini; watu wengi wanauza karanga za kukaanga, visheti na tubiashara tudogo tudogo: vijana wanaendesha bodaboda tu: wengine wanashinda kamali za kubet:

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusifanye mambo kwa kukurupuka. Nimezunguka miji yote nchini pia nchini kadhaa za Afrika ikiwemo SOUTH AFRICA. Tanzania hatuna mji wenye hadhi ya jiji. Labda Dar es Salaam japo nako kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Dodoma bado sana ila tutafika. Halmashauri ya Manispaa kwa sasa ijikite kuupanga mji.
Hamia huko kwenye hadhi ya majiji tuachie majiji yetu Ata kama hayana hadhi!!!
Hivi unaweza kulinganisha jiji la Lusaka na jiji Ata la Arusha achilia mbali Dar?hivi unaweza kulinganisha jiji la Bujumbura na jiji la Mwanza?kajipange urudi tena.
Go Tanzania go,ulipo tupo.
 
Tusifanye mambo kwa kukurupuka. Nimezunguka miji yote nchini pia nchini kadhaa za Afrika ikiwemo SOUTH AFRICA. Tanzania hatuna mji wenye hadhi ya jiji. Labda Dar es Salaam japo nako kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Dodoma bado sana ila tutafika. Halmashauri ya Manispaa kwa sasa ijikite kuupanga mji.
Hivi Tofauti ya Jiji na Manispaa ni nini?
 
OMBI la Dodoma kuwa Jiji litawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais John Magufuli ambaye ndiye mwenye Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza na wafanyakazi wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu (CDA), kabla ya kuwapangia vituo vya kazi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tamisemi, George Simbachawene alisema ataliwasilisha ombi hilo kwa Rais ambaye ndiye mwenye dhamana ya wizara hiyo.

Awali akiwasilisha ombi hilo kwa Waziri wa Nchi (Tamisemi), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi alisema vigezo vyote wamevitimiza hivyo wanaomba halmashauri ya Manispaa ya Dodoma liwe Jiji. Kunambi alisema halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imepitia taratibu zote kwa kupitisha mapendekezo katika Kamati za Ushauri za Wilaya DCC).

“Pia tayari Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) imepitisha na taratibu imekamilisha, kwa sasa mapendekezo hayo yamewasilishwa Tamisemi,” alisema na kuongeza: “Tunaomba Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma iweze kupandishwa hadhi na kuwa Jiji kwa kuzingatia sasa Makao Makuu yamekwishahamia hapa.” Akijibu ombi hilo, Simbachawene alisema kama taratibu zote zimekamilika na vigezo vipo vya kuifanya manispaa hiyo kuwa jiji, atazifuatilia nyaraka hizo na kuzipitia na baadaye kuzifikisha kwa Rais mwenye dhamana ya wizara.

Aliwaomba watendaji wa ofisi yake kama wamepashapata nyaraka za Dodoma kuwa jiji kuzifikisha mezani kwake haraka ili kuzipitia na kuziwakilisha kwa mwenye dhamana ya Tamisemi ambaye ni Rais. Tangu mwaka jana, Serikali imahamishia watendaji wake katika mji wa Dodoma ambao hadi sasa ni Halmashauri ya Manispaa, hivyo DCC na RCC imeomba upandishwe hadhi na kuwa jiji kulingana na dhamana yake kubwa ya serikali kuhamia hapo. Rais Magufuli akiridhia Dodoma kuwa jiji litakuwa la sita nchini baada ya lile la Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga na Arusha.

Chanzo: Habari leo

Kuna miji illikuwa na hadhi ya manispaa kama Tanga,Mbeya, na Arusha.... ikapandishwa hadhi na kuitwa majiji mika kadhaa iliyopita. Ukitembelea miji hiyo ambayo sasa ni majiji huoni kitu kilichobadilika kwa macho, labda kwenye mamlaka kama wameongezewa ruzuku toka serikalini. Nahisi, miji huwa inaji-transform yenyewe kutoka katika hadhi moja kwenda nyingine. Transformation hii itajitokeza kupitia shughuli za kiuchumi ambazo nazo zitakuwa na athari kwenye miundo mbinu, idadi ya watu, n.k. Kupandisha miji hadhi kisiasani kujidanganya
 
Dodoma ni pakubwa jamani halafu pamepangiliwa kimji zaidi huwezi ukaimaliza dodoma kwa miguu utoke st.john university uende Udom kwanza kuimaliza udom 2bkwa miguu ni issue kisha uende ihumwa jeshini hombolo bwawani uingie area a,area c,area d kisasa kisha utokee mailimbili,mnadani,mipango,madini mpaka msalato lazima utakuwa umeshatepeta kwa hiyo kiujumla dodoma now days ni kubwa mno na hujazungumzia katikati ya mji nabpia barabara zake zote zinatoka Iringa,Mwanza,Dar na Arusha unatoka kwa usafiri hata iwe bajaji kuipa sifa ya jiji ni sawa 2 ndio muda wake.
 
Kuna mkuu mmoja hapo juu anasema moshi manispaa Ni kubwa kuliko Dom manispaa imenibidi nicheke tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna miji illikuwa na hadhi ya manispaa kama Tanga,Mbeya, na Arusha.... ikapandishwa hadhi na kuitwa majiji mika kadhaa iliyopita. Ukitembelea miji hiyo ambayo sasa ni majiji huoni kitu kilichobadilika kwa macho, labda kwenye mamlaka kama wameongezewa ruzuku toka serikalini. Nahisi, miji huwa inaji-transform yenyewe kutoka katika hadhi moja kwenda nyingine. Transformation hii itajitokeza kupitia shughuli za kiuchumi ambazo nazo zitakuwa na athari kwenye miundo mbinu, idadi ya watu, n.k. Kupandisha miji hadhi kisiasani kujidanganya
Siku hizi wanasiasa ndio wanaamua mji flani uwe jiji, kama maamuzi haya yangekuwepo enzi ya Mwalimu ama Mwinyi basi Mwanza ingekuwa jiji tangu miaka ya 70
 
Back
Top Bottom