Dodoma yasubiri baraka kuwa Jiji

Dodoma yasubiri baraka kuwa Jiji

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
OMBI la Dodoma kuwa Jiji litawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais John Magufuli ambaye ndiye mwenye Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza na wafanyakazi wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu (CDA), kabla ya kuwapangia vituo vya kazi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tamisemi, George Simbachawene alisema ataliwasilisha ombi hilo kwa Rais ambaye ndiye mwenye dhamana ya wizara hiyo.

Awali akiwasilisha ombi hilo kwa Waziri wa Nchi (Tamisemi), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi alisema vigezo vyote wamevitimiza hivyo wanaomba halmashauri ya Manispaa ya Dodoma liwe Jiji. Kunambi alisema halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imepitia taratibu zote kwa kupitisha mapendekezo katika Kamati za Ushauri za Wilaya DCC).

“Pia tayari Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) imepitisha na taratibu imekamilisha, kwa sasa mapendekezo hayo yamewasilishwa Tamisemi,” alisema na kuongeza: “Tunaomba Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma iweze kupandishwa hadhi na kuwa Jiji kwa kuzingatia sasa Makao Makuu yamekwishahamia hapa.” Akijibu ombi hilo, Simbachawene alisema kama taratibu zote zimekamilika na vigezo vipo vya kuifanya manispaa hiyo kuwa jiji, atazifuatilia nyaraka hizo na kuzipitia na baadaye kuzifikisha kwa Rais mwenye dhamana ya wizara.

Aliwaomba watendaji wa ofisi yake kama wamepashapata nyaraka za Dodoma kuwa jiji kuzifikisha mezani kwake haraka ili kuzipitia na kuziwakilisha kwa mwenye dhamana ya Tamisemi ambaye ni Rais. Tangu mwaka jana, Serikali imahamishia watendaji wake katika mji wa Dodoma ambao hadi sasa ni Halmashauri ya Manispaa, hivyo DCC na RCC imeomba upandishwe hadhi na kuwa jiji kulingana na dhamana yake kubwa ya serikali kuhamia hapo. Rais Magufuli akiridhia Dodoma kuwa jiji litakuwa la sita nchini baada ya lile la Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga na Arusha.

Chanzo: Habari leo
 
Tusifanye mambo kwa kukurupuka. Nimezunguka miji yote nchini pia nchini kadhaa za Afrika ikiwemo SOUTH AFRICA. Tanzania hatuna mji wenye hadhi ya jiji. Labda Dar es Salaam japo nako kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Dodoma bado sana ila tutafika. Halmashauri ya Manispaa kwa sasa ijikite kuupanga mji.
 
Nakuunga mkono 100%
 
Sioni haja ya kukimbilia ukubwa wakati Bado kabisa hata population ni kigezo! Wafanye ya muhimu kwanza
 
Kwa Ccm Hilo Limeshapita Utasikia Tu Punde Jiji Ingawa Wakitulia Wataupanga Vema Wakitangaza Kuipa Hadhi Ya Jiji Dodoma InakuwA Sawa Sawa
 
naunga mkono.wapanue infrastructures kwanza ziendane na wakati ndio wafikirie kuanza kutafuta hayo majina ya kuita majiji.wabongo fake kila kitu.shida.

by jol
 
Tusifanye mambo kwa kukurupuka. Nimezunguka miji yote nchini pia nchini kadhaa za Afrika ikiwemo SOUTH AFRICA. Tanzania hatuna mji wenye hadhi ya jiji. Labda Dar es Salaam japo nako kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Dodoma bado sana ila tutafika. Halmashauri ya Manispaa kwa sasa ijikite kuupanga mji.

Hivi hadhi ya Jiji ni nini hasa? Mfano wikipedia wanasema, "Marianna is a city in Jackson County, Florida, United States. The population was 6,230 at the 2000 census." Je ni nini kimefanya Marianna yenye watu Elfu sita kuitwa Jiji wakati Dodoma yenye watu 410,956 kuwa mji.
 
Tuache maskhara jamani ukiangalia na kuzingatia vigezo vyote vinavyotakiwa ili mji ufanywe jiji dodoma bado kabisa wajameni yani tena baaado kabisa..
Hizi politiki zetu jamani hizi yani basi tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Dar ni "fishing village" , sasa Dodoma sijui itakuwa kitu gani?
 
Tusifanye mambo kwa kukurupuka. Nimezunguka miji yote nchini pia nchini kadhaa za Afrika ikiwemo SOUTH AFRICA. Tanzania hatuna mji wenye hadhi ya jiji. Labda Dar es Salaam japo nako kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Dodoma bado sana ila tutafika. Halmashauri ya Manispaa kwa sasa ijikite kuupanga mji.
Mkuu kama umezunguka nchi zote hizo, utakubaliana na mimi kuwa si Tanzania peke yake yenye majiji madogo. Mfano ni Jiji la Mzuzu nchini Malawi. Mzuzu ni city japo ukubwa wake huenda hauifikii Mbeya. Tofauti ya Mbeya na mzuzu ni kwamba mzuzu imepangwa vizuri kuliko Mbeya. Mbeya is just a big slum.
 
Tanga nalo ni Jiji lakini hakuna cha maana, Dodoma bado ni mji mdogo sana bora hata mji wa Moshi unastahili kuwa Jiji lakini siyo Dodoma.
Na kila mkoa una hospitali rufaa.
 
Tusifanye mambo kwa kukurupuka. Nimezunguka miji yote nchini pia nchini kadhaa za Afrika ikiwemo SOUTH AFRICA. Tanzania hatuna mji wenye hadhi ya jiji. Labda Dar es Salaam japo nako kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Dodoma bado sana ila tutafika. Halmashauri ya Manispaa kwa sasa ijikite kuupanga mji.
Unatumaje vigezo vya SA?Tunavyo vigezo vyetu mkuu ndio vinavyotumika kufanya maamuzi!
 
Back
Top Bottom