Dodoma: Watu 250 hupima afya ya akili Mirembe kila siku

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,818
4,569
Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe jijini Dodoma, inapokea wastani wa wagonjwa wa akili 150 hadi 250 kwa siku kwa ajili ya matibabu.

Idadi hiyo imetajwa kuwa katika kitengo cha huduma za nje ambapo kati ya wagonjwa hao, wagonjwa 30 hadi 70 hupewa matibabu na wagonjwa tisa hadi 15 hulazwa.

Taarifa hiyo imeelezwa leo Alhamisi, Oktoba 6, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk Paul Lawala wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea wiki ya maadhimisho ya afya ya akili jijini hapa.

Dk Paul amesema kutokana na kuongezeka kwa matukio ya kikatili na mauaji kwenye jamii, yanadhihirisha kukua kwa tatizo la akili ambayo husababishwa na sababu mbalimbali.

Kwa upande wake, Daktari wa vyanzo vya akili Veronica Lyimo amesema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo hukutwa na sababu za kibaiolojia, saikolojia na kijamii.

“Tukizungumzia sababu za kibaiolojia hapa unazitaja sababu za magonjwa ya akili ya kurithi na magonjwa ya ndani kama kifafa.

Lakini kwa sababu za kisaikolojia ni malezi mabovu ambapo katika jamii kukiwa na sababu za makundi yasiyo rafiki, matumizi ya pombe, msongo wa mawazo na matumizi ya madawa ya kulevya,” amesema.

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom