Dodoma: Serikali yajipanga kupangua Ripoti

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Baada ya jana PAC kuwasilisha Ripoti ya Escrow,leo ni zamu ya Serikali. Serikali imejiandaa kupangua hoja za PAC. Kujisafisha na kuepusha kuvunjika kwa Serikali. Mikutano mbalimbali ya ndani imefanyika kuamkia leo kujiandaa na mpambano wa leo. Imeafikikiwa kuwa kila mmoja ajibu mapigo yake.Akishindwa ajiuzulu mwenyewe.

Watajwa wa jana wamejipanga na kupangika. Wamewekana sawa mahali fulani fulani. Walipeana tuition usiku kucha. Hakuna hata mmoja,kutokana na vikao vya jana usiku, aliye tayari kujiuzulu kama ilivyopendekezwa na PAC.Na leo wataanza wao kabla ya Mjadala wa Wabunge wote. Kuna nyaraka wamezipata toka sehemu mbalimbali na wameapa kuzitumia kujilinda.

Leo ndiyo leo. Usicheze mbali,unga robo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (Dodoma kwa kazi maalum)
 
Baada ya jana PAC kuwasilisha Ripoti ya Escrow,leo ni zamu ya Serikali. Serikali imejiandaa kupangua hoja za PAC. Kujisafisha na kuepusha kuvunjika kwa Serikali. Mikutano mbalimbali ya ndani imefanyika kuamkia leo kujiandaa na mpambano wa leo. Imeafikikiwa kuwa kila mmoja ajibu mapigo yake.Akishindwa ajiuzulu mwenyewe.

Watajwa wa jana wamejipanga na kupangika. Wamewekana sawa mahali fulani fulani. Walipeana tuition usiku kucha. Hakuna hata mmojautokana na vikao vya jana usiku, aliye tayari kujiuzulu kama ilivyopendekezwa na PAC.Na leo wataanza wao kabla ya Mjadala wa Wabunge wote. Kuna nyaraka wamezipata toka sehemu mbalimbali na wameapa kuzitumia kujilinda.

Leo ndiyo leo. Usicheze mbali,unga robo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (Dodoma kwa kazi maalum)

Waishambulie PAC kwani PAC ndo ilofanya uchinguzi? Hizo nyaraka walishindwa nini kuziwakilisha kwa CAG wakati anawahoji? BULL SHIT
 
Baada ya jana PAC kuwasilisha Ripoti ya Escrow,leo ni zamu ya Serikali. Serikali imejiandaa kupangua hoja za PAC. Kujisafisha na lkuepusha kuvunjika kwa Serikali. Mikutano mbalimbali ya ndani imefanyika kuamkia leo kujiandaa na mpambano wa leo. Imeafikikiwa kuwa kila mmoja ajibu mapigo yake.Akishindwa ajiuzulu mwenyewe.

Watajwa wa jana wamejipanga na kupangika. Wamewekana sawa mahali fulani fulani. Walipeana tuition usiku kucha. Hakuna hata mmojautokana na vikao vya jana usiku, aliye tayari kujiuzulu kama ilivyopendekezwa na PAC.Na leo wataanza wao kabla ya Mjadala wa Wabunge wote. Kuna nyaraka wamezipata toka sehemu mbalimbali na wameapa kuzitumia kujilinda.

Leo ndiyo leo. Usicheze mbali,unga robo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (Dodoma kwa kazi maalum)

Nafikiri watataka kumwaga mboga,yaani kuyaanika mabaya ya wenzao lakini ilo haliwasafishi
 
Pinda aandae leso za kutosha maana hakawii kulimwaga chozi..
 
maccm yanaelekea kunyukana yenyewe kwa yenyewe dakika chache zijazo.watu weweeeeeee!.mtoto hatumwi dukani.
 
leo watakua wakijaribu kuzuia uharo kwa gunzi dadeki, lakin cha kutia moyo ni kwamba hata wabunge wa ccm wamewageuka
 
Kwani serikali inatakiwa kujitetea au kutekeleza maagizo ya bunge! mda wa kujitetea ulishapita na vilevile nyaraka gani zaidi watakuja nazo kujitetea ambazo walishindwa kuzitoa kwa CAG au TAKUKURU?
 
Back
Top Bottom