Dodoma: Serikali yajipanga kupangua Ripoti

Dodoma: Serikali yajipanga kupangua Ripoti

Pinda alipoacha kulia Jana basi nimeamini ni katili
 
Yaani wanataka kusafisha kinyesi na maji taka? waondoke haraka.
 
Nafikiri watataka kumwaga mboga,yaani kuyaanika mabaya ya wenzao lakini ilo haliwasafishi

Tunajua wamejipanga kumchafua zitto lakini hiyo ni nje ya hoja spika atawadhibiti wajikite kwenye hoja kitu ambacho hawana majibu, hasa swala la kodi ya serikali na kukosekana kwa TAX CLEARANCE ya huyo Jambazi. tuhuma zingine wanaweza japo kuogelea.Pingu zinawasubiri

Watueleze fedha ni;
a) si za UMMA
b) ZA UMMA
 
Kati ya hawa wezi wa pesa za akaunti ya Escrow kuna siku atapigwa mawe mtaani kama kibaka. Shikeni haya maneno yangu. Kwa utetezi wao wote, haifuti kuwa wamegawana hela za wizi.
Ova
 
PINDA MBISHI nimelisikia katika maswali ya papo kwa papo
 
Sio kweli mkuu; INA maana we unatembea na kinyesi? Huwezi safisha. Subiri uone Leo bungeni
 
Waking'ang'ania bunge lifukuze hao wezi! Yaani majizi yashindane na bunge? Fukuzeni hao!
 
Mimi kama nilielewa vyema jamani,AKIBA YA MANENO!wacha tuone kwenye mjadala nani ana akiba ya maneno!!!!!
 
Pinda aandae leso za kutosha maana hakawii kulimwaga chozi..


Pinda in tears.jpg


J. K..jpg
 
kuna kila dalili ya Pinda kukomaaa na kukataa kujiuzulu.
 
Dar watoto wengi wa kike wanasukuma mikoko kumbe ni hela zetu za esekero ndio zinatumika kuwanunulia kupitia mafisadi wanaowahonga.
 
Baada ya jana PAC kuwasilisha Ripoti ya Escrow,leo ni zamu ya Serikali. Serikali imejiandaa kupangua hoja za PAC. Kujisafisha na kuepusha kuvunjika kwa Serikali. Mikutano mbalimbali ya ndani imefanyika kuamkia leo kujiandaa na mpambano wa leo. Imeafikikiwa kuwa kila mmoja ajibu mapigo yake.Akishindwa ajiuzulu mwenyewe.

Watajwa wa jana wamejipanga na kupangika. Wamewekana sawa mahali fulani fulani. Walipeana tuition usiku kucha. Hakuna hata mmoja,kutokana na vikao vya jana usiku, aliye tayari kujiuzulu kama ilivyopendekezwa na PAC.Na leo wataanza wao kabla ya Mjadala wa Wabunge wote. Kuna nyaraka wamezipata toka sehemu mbalimbali na wameapa kuzitumia kujilinda.

Leo ndiyo leo. Usicheze mbali,unga robo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (Dodoma kwa kazi maalum)

Hata ulete OMO gunia kaniki haigeuki nyeupe,hao watu tayari wamesha rikoroga hata wakijisafisha haisaidii ni kweli wezi,ingekuwa China wala wasingeruhusiwa hata kuingia mjengonisaa hii wangekuwa lupango,sasa mtu kama Chenge atajitetea kuwa yeye ni msafi,na huyo ni mmoja tu karibu wote waliotajwa ni mafisadi na kila mtu aubebe msalaba wake,na mwisho baadosijaridhika na hii taarifa ya Zitto,ipo nusu ngoja nifungue uzi mpya
 
mwathirika wa wezi kupangua na kugoma kuwajibika ni ccm yenyewe na Si ukawa. ccm wakijifanya wanaakili wamejimaliza.
 
Back
Top Bottom