Dodoma: Rais Magufuli apokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma, awataka wajitumbue

MOA DSM Achia Kiti wewe!!!!.jpg
 
Hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama navyo wamehakikiwa?
Au hao hawako chini ya Idara ya Utumishi ?
Haki itendeke maana hata utendaji wa baadhi yao waliomo humo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama unatia shaka now dayz...
 
mbona kama vile lengo la kikao ni kusifia udom na sio ishu ya vyeti feki? maana kila anayesimama ni kumwaga sifa kwa chuo na hakuna hata mmoja anaegusia vyeti!
 
Mubashara kutoka Ukumbi wa Chimwaga na kupitia hapa JF tunakuletea kinachojiri...

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wameshaingia kwenye ukumbi wa Chimwaga. Yupo Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri wa Utumishi, Mh. Angeka Kairuki, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako, Spika wa Bunge la JMT, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Waziri Mkuu wa JMT, Makamu wa Rais na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshaketi meza kuu.

Kwa ufupi Serikali yote ipo Chimwaga.

Rais Magufuli ameshawasili na wimbo wa Taifa umeimbwa.

Mama Samia Suluhu ameanza kuwasalimia wanafunzi wa UDOM.

Spika wa Bunge la JMT naye anasema maneno machache.

Anasema jinsi chuo kilivyoanza na mchango wake katika kukisimamisha chuo hiko.

Viongozi wote wanatambulishwa kwa wageni. Wako watu kutoka Baraza la Mitihani pia.

Hivi sasa mkuu wa mkoa wa Dodoma anatoa neno la ukaribisho kwa mh rais na wageni wote waliofika katika tukio hili
hii muvi aanze kuuawa stering ndiyo itakuwa pw
 
mafanikio ya UDOM
1. UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO
2. KUWEZA KUENDESHA PROGRAM 186 KILA MWAKA
3. WANAFUNZI WENGI SANA WAMEWEZA KU GRADUATE
4 CHUO KIMEWEZA KUWASOMESHA/ KUWAENDELEZA WATUMISHI WAKE.
5. WANAFUNZI WA UDOM WAMEWEZA KUPATA KAZI MAENEO MBALIMBALI YA NCHI
6.CHUO KINAENDESHA HUDUMA YA KUSAFISHA DAMU YAANI DIALYSIS AMBAYO IMEWEZA KUOKOA MAISHA YA WATZ WENGI
7. CHUO KINA HUDUMA BORA YA KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA VVU/UKIMWI
8. CHUO KINACHANGIA KUTOA HUDUMA ZA KIUCHUNGUZI WA AFYA KWA WANANCHI
 
Back
Top Bottom