Dodoma: Rais Magufuli apokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma, awataka wajitumbue

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,464


Mubashara kutoka Ukumbi wa Chimwaga na kupitia hapa JF tunakuletea kinachojiri...

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wameshaingia kwenye ukumbi wa Chimwaga. Yupo Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri wa Utumishi, Mh. Angeka Kairuki, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako, Spika wa Bunge la JMT, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Waziri Mkuu wa JMT, Makamu wa Rais na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshaketi meza kuu.

Kwa ufupi Serikali yote ipo Chimwaga.

Rais Magufuli ameshawasili na wimbo wa Taifa umeimbwa.

Mama Samia Suluhu ameanza kuwasalimia wanafunzi wa UDOM.

Spika wa Bunge la JMT naye anasema maneno machache.

Anasema jinsi chuo kilivyoanza na mchango wake katika kukisimamisha chuo hiko.

Viongozi wote wanatambulishwa kwa wageni. Wako watu kutoka Baraza la Mitihani pia.

Hivi sasa mkuu wa mkoa wa Dodoma anatoa neno la ukaribisho kwa mh rais na wageni wote waliofika katika tukio hili.

Makamu Mkuu wa chuo prof. Kikula anatoa taarifa/maelezo kuhusu UDOM.

Kaimu Mkuu chuo Kikuu Dodoma, Prof. Kikula

Natoa shukrani ya Dhati kwako Rais kwa kututembelea, Karibu sana.

Nasema hilo kwa dhati, shughuli za leo ungeweza kuzifanyia sehemu yoyote lakini ukazifanyia hapa.

Chuo kilianzishwa mwaka 2007. Wanafunzi wa kwanza walitahiniwa 2007 na kumaliza mwaka 2010.

Chuo kililenga kudahiri wanafunzi 40,000 na kinaendeshwa kwa mfumo wa nchini. Chuo kina shule 7.

Mafanikio.
1. Ujenzi wa miundombinu kwa viwango vya juu, shule tatu ndio bado changamoto
2. Chuo kimenzisha na kuendeleza programu 186, hakuna chuo Afrika chenye idadi hiyo
3. Chuo kimesomesha wafanyakazi wake zaidi ya 400 katika level mbalimbali kwa mapato ya ndani
4. Wahitimu wa UDOM wamefanikiwa kupata ajira sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
5. Chuo kimefanikiwa kuweka miundombinu ya mawasiliano kwa wizara zilizohamia Dodoma
6. Ujenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa
7. Kutoa huduma kwa waathirika wa VVU
8.

Changamoto.
1. Chuo kudaiwa kodi ya Ardhi. Chuo hakina hizo hela za kulipa
2. Kutokukamilika kwa miundombinu katika shule tatu za sayansi nilizoainisha
3. Kukosekana kwa vyumba za walimu chuoni.

Matarajio.
-Chuo kina matarajio ya kudahiri wanafunzi 40,000 ikiwa changamoto hizo zitatatuliwa.
-Chuo kina matarajio ya kuendelea kukua.
-Chuo kina matarajio ya kuanzisha viatamishi (Incubators)

Si kweli kuwa kuna muingiliano kati ya Wizara zinazotumia majengo ya chuo hicho na wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo kinaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hafla iliyohudhuriwa na Rais Magufuli, Makamu wa Rais na PM.

Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako
Natoa shukrani za dhati kwa shuguli hii kufanyika Chuo kikuu Dodoma. Zipo taasisi nyingi ambazo shughuli hii ingeweza kufanyika. Wanafunzi, walimu wa Chuo wamefurahi sana ujio wako UDOM.

Ni heshima kubwa sana kwa Chuo kikuu cha UDOM.Pamoja na kuwa utapokea ripoti ya uhakiki wa vyeti pia utafungua shughuli za sherehe za miaka 10 za chuo cha UDOM

Katika wizara yangu kuna changamoto kuhusu suala la kughushi vyeti. Mwaka 2008 tulianzisha mfumo wa kuweka picha kwenye vyeti vya kitaaluma...

Kutokana na dhamira yako ya dhati Mh. Rais uliagiza watumishi wa Umma wafanyiwe uhakiki. Nashuruku mh. Kairuki aliweza kulisimamia vyema suala hili. Tunakupongeza Rais kwa kufanya maamuzi kwa vitendo.

Serikali imeziba njia zote za mkato! Wanafunzi someni, hakuna tena njia za mkato katika elimu wala ajira.

Uhakiki wa vyeti umefanyika kwa awamu tatu

1. Watumishi wa Mamlaka ya serikali za mitaa
2. Watumishi wa Taasisi na mashirika ya umma
3. Watumishi wa serikali kuu

Rais, Wizara yangu imehakiki vyeti vya kidato cha nne, sita na vyeti vya ualimu kwa watumishi wa umma.

Zoezi la uhakiki kwa awamu ya kwanza na pili umekamilika na tulikabidhi.

Uhakiki wa Vyeti vya Watumishi wa Serikali Kuu upo katika hatua za mwisho na utakabidhiwa hivi karibuni.

Napenda kuwaasa wanafunzi wa vyuo vikuu, waliojiunga vyuo vikuu either kwa kughushi au udanganyifu ni bora ukajisalimisha maana unaweza ukamaliza chuo lakini mbeleni ukakamatwa kwa vyeti feki. Majuto ni mjukuu.

Nawashukuru sana wote kwa kunisikiliza.

Waziri Mh. Angela Kairuki

Uhakiki wa aina hii haujawahi kufanyika kwa mkupuo namna hii. Mheshimiwa Rais, umeacha historia.

Tumekuwa tukibezwa sana kuwa kwanini Sensa inachukua muda mfupi lakini uhakiki unachukua muda mrefu lakini ni kwa sababu kazi hii inahitaji umakini.

Zoezi hili la uhakiki lilihusisha watumishi wa umma pekee wakiwemo Makatibu wakuu na watendaji wengine. Watumishi hawa wanatakiwa kuwa na sifa za kutumikia nafasi zao.

Zoezi hili halikuhusisha Viongozi wa Kisiasa wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa/Wilaya na Madiwani ambao wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tu!

Ripoti hii inaonesha kuwa tayari watumishi wa Umma 400035 wamehakikiwa.

Matokeo ya uhakiki yamegawanyika kwenye makundi manne:

1. 376969 sawa na 94.23% wana vyeti halali. Baraza limehakikisha kuwa magamba ya vyeti vilivyohakikiwa vilitolewa na NECTA na taarifa zao zinaendana na zilizopo kwenye vyeti.

2. 9932 sawa na 2.4% wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi. Vyeti vyao havifanani na vinavyotolewa na NECTA.

3. Vyeti 1538 vinatumika na zaidi ya mtumishi mmoja ambayo ni sawa na 0.3% ya vyeti vilivyohakikiwa. Hawa tunasema wana vyeti vyenye utata.

4. 11569 waliwasilisha vyeti pungufu. Hawa waliambatanisha vyeti vya utaalamu kama udaktari au ualimu pekee bila vyeti vya kidato cha nne wala cha sita.

Kwa mujibu wa kanuni ya adhabu, adhabu ya mtu aliyefanya kosa la kughushi cheti ni kifungo Jela miaka 7.

Waziri Kairuki amekabidhi ripoti na boksi lenye majina ya watumishi na taarifa zao kamili kama wako wapi na wanapatikana wapi.

Rais anatoa kitabu na kusoma jina la mtumishi mmoja " Abdallah Chanja" na kusema mengine atayasoma kwa wakati wake.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Tunafurahi kwamba tumepata taarifa mbalimbali hapa. Siku ya Maadhimisho ya Muungano, sehemu kubwa ya waliohudhuria ni wanachuo wa UDOM.

Tunaamini kuwa elimu ni hatua na kujifunza ni mchakato. Hivyo wote wenye vyeti visivyo halali, wachukuliwe hatua. Serikali inatoa fursa mtu kuweza kurudia kidato ili kupata daraja la juu na si kupitia njia ya mkato.

Walioghushi wamepoteza sifa ya utumishi na sasa nafasi zao wapewe wahitimu wapya.
C-gmiCzXcAIzGXT.jpg

Rais Magufuli akipokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Utumishi, Angela Kairuki

Rais John Joseph Pombe Magufuli
Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu. Nimefurahi sana na makaribisho ya wanajumuiya wa chuo kikuu cha Dodoma. Hii inadhihirisha hapa ni makao makuu ya nchi. Nilivyokuwa natembelea vyuo vingine nilikuwa naenda peke yangu, lakini hapa tumekuja wote hivyo mtambue ninyi ndio chuo bora Tanzania.

Chuo kikuu cha UDOM kina historia ya Pekee Tanzania. Kwanza jengo la Chimwaga limeanza kujengwa kwa mawazo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere. Hili jengo huwezi kulikwepa uwe CUF,CHADEMA historia inabaki palepale.

Wakati wa Mzee Mkapa jengo hili lilikuwa chini ya wizara ya ujenzi. Awamu ya nne Jakaya Kikwete alisema lazima hapa kuwe na chuo Kikuu Kikubwa Tanzania.

Kaimu Mkuu wa Chuo Dodoma, Umeelezea changamoto za UDOM, nakuahidi kuwa nitazishughulikia haraka. Najua Prof. Mkadara utakuwa na wivu lakini hiki ndicho Chuo Kikuu kilicho makao makuu ya nchi.

Prof. Kikula amenikabidhi vitabu viwili vinavyoelezea historia ya UDOM. Historia yoyote ni muhimu ili kuelezea umetokea wapi, wapi ulipo na unakwenda wapi.

Nawaomba wanachuo muendeleze mshikamano na kujenga nchi yetu. Serikali ya awamu ya Tano ipo pamoja nanyi.

Toka tumeingia madarakani tumechukua hatua mbalimbali, hatua nyingine zinawaudhi baadhi watu wengine.

Hatua tulizozichua, tulifanya ukaguzi na kuwabaini watumishi hewa 19,706 na kila mwezi walikuwa wanachukua bilioni 2 kama mshahara. bilioni 38 kwa mwaka kama watumishi hewa, tumewatoa wote labda mmoja mmoja. Baada ya kuwatoa hawa mishahara imeshuka na matumizi yameshuka. Kama umepata watumishi hewa ina maana hata increments zilikuwa hewa na kupandisha madaraja hewa.

Baada ya kumaliza zoezi hili tuliingia zoezi jingine gumu la vyeti. Dunia nzima suala hili ni gumu sana. Unakuta mtu ana cheo fulani kumbe cheti si chake.

Unamaliza masomo yako hapa UDOM ukiwa na GPA 4.1 na unakwenda kuomba kazi, unayem-face kumbe ni darasa la saba na hajui hata kusoma GPA anakuzungusha.

Watumishi 9,932 kati ya watumishi waliohakikiwa walikutwa na vyeti vya kughushi. Waziri mkuu, hawa watumishi mshahara wao ukatwe na waondolewe kwenye utumishi wa umma mara moja. Watakaofika na kubisha mpaka mwezi wa tano basi wachukuliwe hatua hata wakafungwe hiyo miaka 7.Hizo nafasi 9,932 zitangazwe ili watu wenye sifa wapate kuzijaza.

Hayo majina yachapishwe kwenye magazeti maana ndio uwazi. Tanzania kuajiriwa sio mpaka uwe na digrii, hata darasa la saba utaajiliwa kulingana na sifa zako. Kila rank ya elimu Tanzania unaweza kupata kazi inayokufaa kutokana na ujuzi wako.

Hata Waziri Mkuu kama alisema ulishindwa kufikia elimu fulani, ''dont Jump''.

Watu wa wizara ya fedha kama mpo hapa nendeni mkafute majina yao kwenye kompyuta, hata mimi nitakuwa naangalia.

Wale ambao watakuwa hawajaondoka mpaka tarehe 15 May, basi wakuu wa idara waripotini kwenye vyombo vya dola ili wakaseme vyeti vyao walivichapisha wapi.

Wale wenye vyeti vyenye utata, mpaka tarehe 15 May muwe mmehakikisha wahusika wa vyeti halali. Na mishahara yao kwanza msianze kuwapa mpaka uhakiki ukamilike.

Mpaka hapa tutakuwa tumepata nafasi za ajira 12,000, si haba.

Watumishi 11,569 waliwasilisha vyeti pungufu. Hawa waendelee kulipwa mishahara wakati uchunguzi ukiendelea tusije tukawanyima watu haki yao.

Nawapongeza sana mawaziri mmefanya kazi nzuri, nimefurahi sana nimewatumbua wengine. Wanafunzi mkae mkao wa kupata hizi nafasi za waliotumbuliwa.

Yani mimi mtu ameghushi vyeti alafu nimsamehe? Kwa weli haiwezekani. Wataondoka mara moja

Katika bajeti ya mwaka huu tutaajiri watumishi 52,456 tutajumlisha na tulizotumbua leo zaidi ya 12000.

Baada ya kazi nzuri iliyofanywa basi nibaki tu kutekeleza ya yaliyonya. Serikali ya awamu ya tano imejipanga kufanya kazi, nchi hii ni tajiri sana. Tunaweza kitu chochote na bahati mbaya mipango yetu tunakuwa tunaikosea na wakati mwingine kwa kulinda siasa. Bahati nzuri nchi imepata asiye mwanasiasa. Hata mimi nilivyokuwa chuo nilikuwa nawachukia wanasiasa.

Taarifa zilizotolewa leo ni ushahidi kuwa nchi tuna matatizo. Kila wizara, sekta kuna matatizo makubwa. Kule bandarini pia tulipoanza kuchukua hatua walianza kulalamika mizigo imepungua. Nikasema hata ikija meli moja basi ilipe kodi. Juzi nimeenda bandarini nimekuta meli 30 hadi zinakosa pa kupaki.

Bado kuna maeneo bado tunaibiwa, kwenye makampuni ya simu hawa wanafanya transaction kubwa lakini pesa serikalini haiingii, dawa yao inakuja.

Tumeweza kupata hela za kununua ndege 6 kwa mpigo kwa fedha zetu wenyewe. Tumejitahidi katika kukusanya kodi!

Tumejitahidi sana, kwa sasa tunajenga reli ya kiwango cha kati (SGR) kwa kutumia fedha zetu za ndani! Kwa Afrika ukihesabu ni nchi mbilia au tatu zenye treni hizi.

Nawashukuru wabunge kupitisha mpango wa Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. Vimeshaanza kujengwa! Pwani pekee vimejengwa 83

Nawaomba viongozi wenzangu wa awamu ya tano tusaidiane kila mmoja kwa nafasi yake. Haya ya watumishi hewa haikuwa lazima tumsubiri waziri Kairuki, Mawaziri waliopita hawakuwaona?

Hivi mawaziri wa siku za nyuma hawakuwaona watumishi hewa na wenye vyeti bandia? Lazima tukumbuke dhambi zilizofanywa

Nayaongea haya kwakuwa nimeipata hii venue! Walikuwepo mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wakuu wengine yakitokea haya.

Hatuko hapa kuwalaumu viongozi waliopita lakini ni vyema tukakumbuka dhambi zao

Kama TCU wasingekuwa wanawapangia wanafunzi vyuo vya kwenda, ungekuta UDOM imefikisha wanafunzi 40k

Hakuna mwanafunzi ambaye ataomba chuo ambacho ataenda kukaa kwny chuo ambacho hata sehemu ya kulala hakina... TCU

Eti watu wanahoji Serikali yangu kuhamia kwenye majengo ya UDOM, kwani si ni ya Serikali? Tutahama tu, full stop!

Baba wa taifa alitangaza Dodoma kuwa Makao Makuu nikiwa darasa la sita, ila hadi nimeingia ndio tunahama.

Profesa mmoja hapa UDOM alikuwa mtu wa Vyama nikamwambia aondoke asirudi tena - Siwezi kumlipa mshahara halafu ananitukana.

Ripoti za Benki ya Dunia zinaonyesha Tanzania ni nchi ya Pili barani Afrika kwa uchumi unaokua kwa kasi.
 
Dodoma. Rais John Magufuli leo
anatarajia kuzungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Dodoma(Udom).

Ulinzi umeimarishwa katika ukumbi wa
Chimwaga, udoma huku maofisa
usalama wakifunga mashine za kukagulia magari katika barabara za kuingilia chuoni hapo.


Kadhalika, waliokuwa wakiingia katika
ukumbi huo waliamriwa kuzima simu zao hadi pale watakapotoka ndani ya ukumbi huo.

Pamoja na hilo, leo Rais atakabidhiwa
orodha ya watumishi kwenye vyeti feki
katika mkusanyiko huo sambamba na
kusherekea miaka 10 tangu kuanzishwa chuo hicho ambacho kilianzia katika ukumbi wa Chimwaga zamani ukimilikiwa na CCM.
 
Mubashara kutoka ukumbi wa Chimwaga, kupitia tbc1 na kupitia hapa JF muhabarishaji wako HUGOCHAVEZ niko tayari kukuletea kila kinachojiri.

Wakati huo huo kwa mara ya kwanza tangu Uhuru, Rais Magufuli ataongea moja kwa moja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Ambatana nami tafadhali.

Hilo tukio litanoga na kuwa na maana zaidi kama utekelezaji wake utaanza mara moja kwa kuanzia na Gaidi wa Kisiri na Mtekaji Mkuu wa Bongo City.
 
Katibu mkuu kiongozi ameshawasili pia waziri wa elimu, waziri wa tamisemi na waziri wa utumishi.
 
Ulinzi Umeimarishwa hapa Walioona Ulinzi wa Obama ni the Same Hakuna Access ya Simu Ukumbi wa Chimwaga, Magari Na Watu lazima wafanyiwe Security Check (TISS) nao wamesambazwa Kama Njugu.


Urais Mzuri aisee acha Lowassa Apambane.

2.jpg
 
Back
Top Bottom