Kwa mtu mwenye akili timamu anaweza kutambua kuwa kitendo wanachotufanyia wabunge sisi watanzania ni mzaha na utani mpaka baadhi ya mawaziri.
Ni mwananchi gani aliyesota kwenye mstari tangu asubuhi atumie demokrasia yake ya kupiga kura halafu ategemee kusikia maneno kama:
1.Siongei na mbwa,naongea na mwenye mbwa
2."....mtoto wa Dr. Slaa ana wiki mbili..."
3."...pumbavu...."
4."....huyu niachieni mimi na mwigulu..."
5.----y you...!
6."....kuna wabunge wana mimba zisizo tarajiwa....." nk.
Najua kuna watu walikuwa wanatumia lugha za picha kumaanisha jambo fulani,ni sawa, lakini kwa hali nchi ilivyo sasa,nadhani wabunge hawa wangejikita kujadili matatizo ya wananchi na nchi kwa ujumla kuliko kuonyeshana ufundi wa kuongea na kushambuliana wao kwa wao.
Pili nilitaka kujua kama wabunge hawa wapotumia muda huu kulumbana kwa matusi,je,majimboni kwao hali ikoje katika mabo haya?
1.barabara
2.elimu
3.afya
4.mfumuko wa bei
5. maji
6.watoto na wazee wenye mazingira magumu nk.
Tatu,kwanini wasijadili hali amani ya nchi,anguko la elimu,mikataba mibovu,ufisadi, utendaji mbovu,mafuriko,nk?
Mawazo yangu,kama hali ni hii ni heri nchi kutokuwa na bunge,na itafutwe namna nyingine ya kujadili na kuendesha nchi kuliko kuwalipa watu kwa kodi zetu ,lakini kazi yao nikuonyeshana ufundi wa matusi.
Aksante.
K
Kuna uwezekano mkubwa Wabunge
Mwigulu Nchemba,Peter Serukamba na Juma Nkamia wakahojiwa na Kamati Maalum ya Nidhamu ya Wabunge wa CCM kwa kile kinachosemwa kuwa ni kukichafua chama-CCM. Wabunge hao,kwa nyakati tofauti,wamesikika wakitukana na kutumia lugha ya kuudhi Bungeni. Nani atawagusa watukanaji hawa? Taarifa zaidi zitafuata kadiri zitakavyopatikana.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)