DODOMA: Mwanafunzi wa chuo cha Mipango mbaroni kwa Wizi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,565
Reaction score
4,009
Polisi mkoani Dodoma inamshikilia mwanafunzi wa Chuo cha Mipango kilichopo jijini hapa, James Senya (21) kwa tuhuma za kujihusisha na makosa ya uvunjaji na wizi katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Gilles Muroto amesema mwanafunzi huyo amekamatwa baada ya kufanyika doria na kugundua kuwa anashirikiana na wahalifu kuvunja na kuiba katika nyumba za watu.

Amesema mwanafunzi huyo wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho, amekuwa akiwachorea wahalifu ramani ya kuvunja ambapo wahalifu hao hufika na kuvunja na kupora mali zote kwa kushirikiana na mwanafunzi huyo.

“Hii inaonyesha kuwa hata wanafunzi wanajihusisha na uhalifu badala ya kufuata masomo yeye anajihusisha na uhalifu,” amesema Kamanda Muroto.

Mwanafunzi huyo amekamatwa na watu wengine watano anaodaiwa kushirikiana nao katika uhalifu ambao ni Ayubu Hosea (23), Saudi Mosse (23), Semen Njaid (24), Salum Abdallah (16) na Godfrey Mashauri (26) wote wakazi wa Jiji la Dodoma.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa huyo salumu Abdalah nae ana kesi gani kwa umri wake huo?
 
NAONA ALIKOSE MKOPO AKAONA AJITAFUTIE KWA NJIA HIYO
 
tuache mahakama ifanye kazi yake na sio kutumia hisia binafsi za kamanda watapata taab sana kuwahukumu watu
 
Ushauri wangu, kabla ya kukimbilia na kumuhukumu kijana, tungesubiri kwanza tupate ukweli toka mahakamani.. Polisi wa Tanzania ni mabingwa wa kutunga na kuwabambikia watu kesi..
 
Huyo dogo namfaham kindakindaki. Hii issue wamepewa tena kwa kuforce. Dogo alikuwa ametoka kula mida ya saa moja jamaa wakamkamata wakampeleka central, bila maelezo wakawekwa ndani asubuh yake wakapelekwa kwa RPC.
 
Huyu jamaa ni mropokaji mpenda media. Atasemaje ni majambazi wakati hawajapelekwa mahakamani? Fvk him
 
Back
Top Bottom