Kigogo anayefahamika kwa jina moja la Maimu,amevamia eneo la shule ya sekondari Nuru ,iliyopo kata ya Ipagala na kuvunja makufuri yaliyokuwepo kisha akafunga yake na kuendeleza shughuli za ujenzi ,shule hiyo ambayo inamilikiwa na MAMA NURU(nuru group).Inasemekana kigogo huyo amekua na tabia ya kupora maeneo ya watu mbalimbali mkoani dodoma .Akiongea kwa masikitiko makubwa huku akionyesha mipaka ya miti iliyokatwa na mvamizi huyo Mama Nuru anasema "Ninashangaa sana mtu anatoka huko alikotoka na kuja kuvamia eneo langu hivi kweli hii ni haki na kila ninapomwambia tuonane amekua akikwepa ,mtu huyo kwa sura hata simjui lakini amekua akiendelea kuwatuma watu waendelee na shughuli katika eneo langu.
Mwisho mama Nuru anaomba wasamalia wema tumsaidie kufikisha malalamiko yake kwa Waziri wa ardhi nyumba na makazi.
Mwisho mama Nuru anaomba wasamalia wema tumsaidie kufikisha malalamiko yake kwa Waziri wa ardhi nyumba na makazi.