DODOMA: Bunge lacharuka Wizara kutokutoa fedha za kutosha kwenye miradi mingi ya maendeleo

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara maarufu Bwege amependekeza kuuzwa kwa ndege mbili za Serikali aina ya Bombardier ili fedha zitakazopatikana zitumike kumaliza changamoto za upatikanaji wa maji nchini, kwa madai kuwa zimedumu kwa miaka 57.

Bwege ametoa kauli hiyo leo Mei 8, 2018 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19.
Huku akizungumza kwa sauti ya kupanda na kushuka, Bwege amemuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kusimamia upigaji kura wa wabunge, ili kubaini idadi ya wanaounga mkono ununuzi wa ndege hizo na wale wanaotaka fedha kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maji.

“Leo nakuona kama Spika kweli kweli, upo strong (imara) hongera sana,” amesema na kuwataka wabunge kutoshusha lawama kwa waziri wa wizara hiyo, mhandisi Isaack Kamwelwe na Katibu Mkuu wa wizara, Profesa Kitila Mkumbo kwa madai kuwa bila fedha, hawawezi kufanya lolote.

“Serikali inatakiwa kutoa fedha za maendeleo maana mnachokisema si mnachokitenda. Leo mwananchi umuulize ndege na maji nini kizuri, nyinyi wabunge kama kweli tuwaulizeni kununua ndege na kuwapa watu maji bora nini?”

Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge amesema, “wanaosema inunuliwe ndege na wanaosema tuanze maji wasimame, mkirudi mwaka 2020 (baada ya uchaguzi mkuu) mimi sio Bwege. Mheshimiwa Spika uulize, wanaosema ndege na maji halafu tukawaonyeshe huko, mheshimiwa Spika utaruhusu kweli? Wabunge tuwaheshimu mawaziri, sisemi Magufuli mzigo, nasema Serikali ya CCM mzigo.”

Amesema katika jimbo lake amekuwa akiomba mara kwa mara hospitali ya wilaya ipelekewe maji, kwamba akihoji maji anajibiwa ndege kwanza.
“Miaka 57 ya CCM tunaongelea maji? Serikali ya CCM amkeni kama hakuna maji, kama hatupati maji Serikali ya CCM bai bai, maji ni uhai na masheikh wako magereza hakuna maji.”

Amesema kutokana na uhaba huo wa maji ni vyema zikauzwa ndege mbili ili kutatua tatizo la maji, “mheshimiwa Spika kwa kuwa uko vizuri, piga kura anayetaka ndege au maji.”

Mara baada ya kumaliza kuchangia, Spika Ndugai amesema, “hata tukiwalaumu Waziri na Katibu Mkuu tunawaonea. Tukiacha mfuko wa maji, Serikali imetoa asilimia 11, lakini kesho waziri wa fedha, akisimama hapa watueleze. Hivi kama wewe ungekuwa waziri ukisimama hapa utasema nini.”

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika amewashawishi wabunge kutopitisha bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19 hadi hapo Serikali itakapotoa fedha za maendeleo zilizopitishwa na Bunge katika bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2017/18.

Kwa mujibu wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, kiasi cha fedha za miradi ya maendeleo kilichotolewa na Serikali kwa wizara hiyo hadi Machi mwaka huu ni asilimia 22 tu.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti hiyo leo Jumanne Mei 8, 2018 bungeni mjini Dodoma, Mnyika amesema, “maji kwa wananchi ni zaidi ya mafuta. Mheshimiwa spika maji ni uhai onyesha ukali wako katika hili, tumeshauri sana sasa ni
wakati Bunge kutumia mamlaka yake kuisimamia Serikali. Na katika kuisimamia Serikali, bajeti ya wizara ya maji tusiipitishe
sasa.”

Amesema kama si shauku ya wabunge kuchangia, waruhusiwe kufanya hivyo hadi kesho lakini bajeti hiyo isihitimishwe hadi hapo watakapotoa fedha zilizopitishwa katika bajeti ya mwaka 2017/18.
Bajeti ya wizara hiyo iliwasilishwa jana bungeni, kujadiliwa jana, leo na kutarajiwa kupitishwa kesho.

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameishukia Serikali kuhusu madai ya kupanda kwa bei ya mafuta ya kula akimtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kufikia leo Jumanne Mei 8, 2018 saa 11 jioni kuwasilisha bungeni taarifa ya kinachoendelea kuhusu jambo hilo ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo asubuhi bungeni mjini Dodoma wakati akijibu mwongozo wa mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe aliyehoji kuhusu bei ya mafuta, akidai imepanda na kujibiwa na Mwijage kuwa jambo hilo linashughulikiwa kwa maelezo kuwa kwa sasa umeibuka mvutano.

Tishio la kuadimika kwa mafuta ya kula linatokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzizuia meli mbili zenye tani 62,000 za mafuta ya kula katika Bandari ya Dar es Salaam tangu mwezi uliopita kushusha mzigo mpaka wamiliki wake watakapolipa kodi husika.

Utata wa kulipa kodi inayodaiwa na TRA, unatokana na madai ya mamlaka hiyo inayosema mafuta yaliyoingizwa ni safi ilhali wamiliki wakieleza ni ghafi.
Leo katika majibu yake, Mwijage baada ya kutoa maelezo marefu amesema alitoa ushauri kwa TRA kwamba wenye mafuta, “nusu ya mzigo ushushwe, tatizo linalokuja tunahukumiwa na historia, nashauri hii kazi unipe mimi, nitakuja saa 11 kukueleza kipi kimetokea.”

Baada ya kauli hiyo ya Mwijage, Spika Ndugai alisimama na kusema: “Nalikubali hili la saa 11 na bahati nzuri nitakuwa hapa. Tunapokuwa bungeni lazima tuseme ukweli yaani iko hivyo.Tukiligeuza Bunge hili kuwa mahali pa kubangazia hivi, mimi niombe saa 11 tupate majibu ya uhakika.”

Bei ya sukari yatikisa bungeni

“Mnatufikisha mahali pagumu sana, kwa mambo madogo mno, hivi tuliosoma kemia hivi kupima mafuta kujua ni ghafi au masafi inachukua muda? Kitu cha dakika kumi na tano watu wanazunguka zunguka. Hamuwamini TBS (Shirika la Viwango Tanzania) au pelekeni Nairobi, Afrika Kusini, Kenya mnapima na kupiga kodi.”

Huku akishangiliwa Ndugai amesema, “…tunaumiza wananchi na hata yakikaa huko yakiingia anayeumia ni mwananchi, sisi tunalumbana tu.”
Awali, baada ya majibu ya Mwijage, Ndugai alimtaka mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Suleiman Saddiq kulielezea suala hilo na kusema walipokutaka katika semina Jumamosi iliyopita, lilijitokeza ukiwamo mkanganyiko kati ya TBS, TRA na Mkemia Mkuu wa Serikali.

Baada ya Ndugai kueleza msimamo wake kuhusu jambo hilo, Mwijage alinyanyuka alipokuwa ameketi kwenda kuteta na waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama kisha kwa pamoja kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
 
Waje na majibu mujarabu .......sio kila kitu wanaleta siasa..
 
Wanazunguka tu mbuyu hawa, tatizo la yote haya ni JPM. Wakikutana naye ni kukenua meno tu akishawapa mgongo wanaanza kinung'unika.
 
Wabunge wa CCM ni kama mbwa koko, utashangaa hiyo bajeti inapita, ndio utakapojiuliza, ''Si ndio hawa waliokuwa wanabweka huku wanarusha mate?''

Subiri waitwe ukumbi wa Msekwa, wakapigwe mkwara.
 
Khe kheeeee kheeeeeeee hatimaye BUNGE LAFUFUKA....hahahahahahaha Maajabu ya Tanzania, ni kweli limefufuka au ni usanii mwingine ambao umekithiri nchi hii?
 
Back
Top Bottom