Dodoma: Ajali ya gari la CAG, yaua watu 7 baada ya kugongana na gari la NSSF

V8 zitaharibika sana mwaka huu na ujao na huo mwingine ujao sababu ya utaratibu mbovu
 
Wewe sio mtumishi wa ofisi ya cag
Unachukua gari la ofisi,unaenda kutembea kijijini,unapata ajali unakufa
 
Haya maisha bhna serikali inazuia ajali kwenye magar mengine ila sasa ajali zimehamia kwao ina mana serikal hawajo serious na kuzuia ajal
 
Wafanyakazi wa serikalini wataanza kuzikataa safari sasa, manake sio kwa vifo hivi..... RIP wote waliopeteza maisha kwenye ajali hiyo, Mungu awarehemu! Poleni majeruhi tunawaombea uponyaji, pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwapoteza wapendwa wenu
Waache per diem
 
STL tena . Mimi bado shida ni uzoefu Wa madereva wasomi Wa serikali. Kwa nini mliwafukuza std vii? Ina maana anakanyaga mafuta bila control ya gari. Sasa ghafla mble mlori umepaki bila hazard hakuna jinsi lazima ulivae tu!!!!! Poleni wafiwa. Ni matokeo ya makosa ya kibinadam.
Mkuu dereva wa CAG alikuwa mzoefu Sana, namfahamu zaidi ya miaka 15 barabarani
Tuseme ni bahati mbaya
 
Huku kuhamia Dodoma kutaondoka na roho za wabongo wengi sana.


Watumishi hamieni Dodoma mazima acheni kuwa mnakuja dar kucheki familia hali si nzuri na hiyo barabara
Lazima madereva wawe makini sio kuendesha kwa mazoe walahi
 
Ajali mbaya sana, Mungu awapumzishe mahali pema. Hizo VX sasa zimegeuka makaburi dah
 
Dereva saa 8 usiku uko njiani tena ukiitokea chato. Kwanza ni safari ndefu sana na ni lazima achoke hata kama ni fereva mzuri. Nasikia boss wake alimwambia awapeleke ndugu zake DSM huku yeye boss akipanda ndege ila dereva ilitakiwa akifika DSM ageuze kurudi Dodoma kuhudumia boss. Hii siyo ethics kwa utumishi wa umma unless kama huyo boss aliomba kibali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara anayoitumikia ambaye hapa itakuwa ni Wizara ya Fedha na Mipango. Wako maboss wengi wa aina hii na ikibidi serikali iwashughulikie.

Yuko boss mmoja Mkuu wa taasisi fulani ambaye gari ya ofisi anatumia kubeba familia kwenda likizo tena Mkoa wa mbali na akilipwa mafuta kwa pesa ya ofisi ambapo Rais wetu mpendwa anaitafuta kwa nguvu ili kuwekeza kwenye mradi ta maendeleo. Mbaya zaidi kwa upande wa Perdiems ndiyo usiseme hapo inahitaji special audits kabisa maana ni madudu. Mh Rais bado una safari ndefu sana ya kupambana na mafisadi. Bado hujapata clean leaders wengi ni corrupt tu.
 
Rudisheni standard seven drivers otherwise hawa bongofleva watawamaliza
 
Ofisi ya CAG,wanafamilia wanasafirishwa kwa gari la shirika huku boss akija na ndege.
 
Wakuu ni ajali Moja mbaya sana imetokea sehemu Moja inaitwa Cjui mbande

Ni kama kelometa 70 kuingia Dodoma mjini ni porini tu hakuna hata nyumba karibu

Hyo gari ya serikali imepiga engo ya tela LA semi kichanja ilikua imebeba embe

Watu watano wamekufa hapo hapo mida ya saa 8 ucku mimi nilikua natokea dar naenda Dom ndo nimeikuta hyo ajali mbichii kabisa.

Mungu awarehemu ndgu zetu.

R.I.PView attachment 919747View attachment 919748View attachment 919749View attachment 919750View attachment 919751View attachment 919762

SAFARI ZA USIKUUSIKU KAMA HUJALALA VYEMA HATA UWEZO WA MACHO KUONA UNAPUNGUA,TUWAPE MADEREVA WA UMMA MUDA WA KUPUMZIKA HASA KWENYE SAFARI NDEFU,UNATOKA MWANZA UNAUNGA MOJA KWA MOJA DAR,WAKATI UNATAKIWA KUENDESHA MASAA NANE HADI KUMI TU!
 
SAFARI ZA USIKUUSIKU KAMA HUJALALA VYEMA HATA UWEZO WA MACHO KUONA UNAPUNGUA,TUWAPE MADEREVA WA UMMA MUDA WA KUPUMZIKA HASA KWENYE SAFARI NDEFU,UNATOKA MWANZA UNAUNGA MOJA KWA MOJA DAR,WAKATI UNATAKIWA KUENDESHA MASAA NANE HADI KUMI TU!
Ni kweli safari za usiku ni nzuri kwa maana hakuna bughdha ila km hujalala mchana vzr ni hatari na hasa ukiwa na abiria wanaolalalala maana dereva pia inakuwa rahisi kusinzia.
 
hii ajali nadhani yoyote ingewez kumtokea sio lazm gari ya serikali, hicho kichanja unaweza kuta kiliharibik kikaach angle barabarn n hamn relactor wala harzard unakionaj usiku?
Unachoongea ni kweli lakini vp kuhusu kusafiri saa 8 usiku na chombo cha umma?
 
Back
Top Bottom