Dodoma: Afungwa miaka miwili kujifanya ofisa TRA

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,006
9,872
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma, imemhukumu mkazi wa Dar es Salaam, Kitareti Mahuti, kifungo cha miaka miwili jela na kulipa faini ya Sh. milioni mbili kwa kosa la kujifanya mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hukumu hiyo ilitolewa Jumanne wiki hii na Hakimu Mkazi Aloyce Katemana, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.

Akitoa hukumu hiyo katika kesi namba 170 ya mwaka 2019, Hakimu Katemana alisema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, kutoa adhabu hiyo.

Alisema hukumu hiyo imetolewa ili iwe fundisho kwa watu wanaojifanya watumishi wa umma na kutenda makosa hivyo kuharibu taswira nzima ya serikali na utumishi wa umma kwa ujumla.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Miyango Kezilahabi, alidai kuwa mshtakiwa alifikishwa mahakamani mara ya kwanza mwaka 2019.

Mwanasheria wa TRA, Hadija Senzia, alidai kuwa mshtakiwa alikuwa akitumia kitambulisho bandia cha TRA, alizunguka kwenye maduka na nyumba za kulala wageni na kujitambulisha kuwa ni mtumishi wa mamlaka hiyo, akiwakagua wateja na kuwatishia kuwapa makosa mbalimbali.

"Document (nyaraka) nyingi zilikuwa za kughushi na alikuwa akiwatishia wale wasiotoa risiti kwa njia ya kielektroniki (EFD) na alikuwa akidai fedha,” alidai.

Senzia alidai kuwa mshtakiwa alikuwa akitumia majina tofauti kwenye kitambulisho chake ambacho kilikuwa na namba za kuonyesha kuwa ni mwajiriwa wa TRA na kwamba alikuwa akizunguka mikoa mbalimbali akidai yeye ni ofisa wa kodi akitumia gari aina ya 
Toyota IST.

"Alikuwa na kitambulisho feki cha TRA chenye jina la Miringe James, kazi ofisa wa kodi," alidai.

NIPASHE
 
Hii habari inanikumbusha 2017 dogo mmoja aliajiriwa customs TRA akashikishwa fedha ya moto akajikuta yupo jela. Dogo alikuwa anajitamba kuwa hagusi mshahara wake
Duh ndio Basi tena kwa huyo dogo.

kuna siku nilisikia Commissioner General kichere akiwaambia watumishi wa custom Kule Tunduma alisema ukiletwa kwangu kwa mashitaka ya rushwa nakufukuza kazi tu na hata ukienda mahakamani na ukatushinda then nitakulipa stahiki yako lkn kazini hautarudi maana bado Nina mamlaka ya kutokukurudisha kazini.
 
Hii habari inanikumbusha 2017 dogo mmoja aliajiriwa customs TRA akashikishwa fedha ya moto akajikuta yupo jela. Dogo alikuwa anajitamba kuwa hagusi mshahara wake

Si yule dogo kwenye picha iliyosambaa anepigishwa Magoti alipewa hela za moto na wachina hivi...
Sio ilikuwa 2019-2020?
 
Back
Top Bottom