Documents za ofisi zinapotumika kufungia maandazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Documents za ofisi zinapotumika kufungia maandazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sinkala, Jul 15, 2010.

 1. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikipigwa butwaa kuona nyaraka zenye mambo binafsi ya waajiriwa katika maofisi mbalimbali zikitumika kufungia maandazi au kutengenezea bahasha za kubebea bidhaa mbalimbali. Katika tukio la hivi karibuni nilipigwa picha ukumbini kwenye harusi ya jamaa yangu (tena bila ridhaa, kama upo Bongo utajua kwamba ukiwa ukumbini kwenye sherehe za harusi jamaa huwa wanapita wanajipigia tu picha na kuzisafisha haraka haraka halafu mwisho wa sherehe wanazianika pale karibu na mlango eti mhusika 'azikomboe'). Kama kawaida nililipia picha yangu na jamaa akaiweka kwenye bahasha na kunipa. Nilipokuwa on the way back to home niliisoma ile bahasha na kugundua kuwa ilikuwa imetengenezwa kwa karatasi ambalo ni payroll ya tarehe za hivi karibuni ya wafanyakazi wa kampuni moja (nahifadhi jina). Nilifadhaika sana nilipoona miongoni mwa wale walioorodheshwa, kuna jina la jamaa nimjuaye. Kikubwa kilichonifadhaisha ni kuona viwango vya mishahara vilivyokuwa vidogo vikiwa vimeanikwa hadharani na kuondoa hali ya usiri wa malipo ya mwajiriwa. Sasa sijui ni nani anayezitoa kiholela kati ya mwajiri au sekretari. Na hiyo si pekee, wakati mwingine unazikuta zinafungiwa maandazi. Ole wao nikute jina langu!
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Jul 15, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Unajua watu wengi hawajui kuwa zile documents ni za siri na zinatakiwa zitunzwe na kama kuharibiwa ziharibiwe chini ya uangalizi maalumu. Lakini imekuwa ni tofauti kwani watu wengine wanafanya ni biashara kwa wauza maandazi na wengine wanaotumia kwa matumizi mengine kama hayo ya bahasha.
   
 3. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Ila huo ni uzembe wa hali ya juu ungemsaidia huyo jamaa kwa kumutahadhirisha ili bomu hilo alifikishe kwenye ofisi yake ijulikane mbivu na mbichi na inachooneka wakati mwingine mabosi kuwaachia tu wahudumu wanaposafisha na kuchukua matakataka ili wakayachome wao bila kujua yamechomwa kweli au ndiyo muhudumu kaanza nayo mbele kwa faida zake.
   
Loading...