Usiku mgumu, maamuzi magumu

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
375
1,000
Ujana ni maji ya moto,je ungekuwa ni wewe ungefanyaje?

Miezi miwili iliyopita baada ya kupata habari kuwa dada J ambaye yupo hapa mtaani kwetu amemaliza kidato cha 4 na matokeo hayakuwa mazuri kuendelea na elimu inayofuata,basi moja kwa moja aliingia kwenye target yangu,siyo siri aliingia katika nyama za moyo wangu akapenya na kupenyeka na nikawa namuwaza kwa asilimia 99 namna ya kumnasa

Baada ya siku kadhaa,ghafla nilikutana naye gengeni,akanisalimia ,nikaitikia ila sikutaka kulipuka mle gengeni,ikabidi nitoke nje ili nijilipue kwake

Haraka haraka nikatoka nje nikasimama sehemu Fulani ambayo kiumbe ataingia mtegoni

Baada ya dakika kama 10 mtoto akawa anapita anaenda nyumbani,nikajilipua nikamuita,bila hiyana mtoto akaja ,basi kama kawa ya wanaume nikaanza kuimba maana kwanza alikuwa ananifahamu maana tunaishi mtaa mmoja kama nyumba 5 hivi

Bahati mbaya mtoto akazengua,nikamsihi anipe namba za simu akazengua hakunipa ,basi sikukata tamaa,siku iliyofuata nikakutana na Dada yake nikamuomba namba za simu za mdogo wake akanipa

Basi usiku nikaanza texts whasap na kabla ya text kwenye pd yangu nikaweka picha ili kupunguza maswali wewe ni nani kisha nikamtext

Baada ya sekunde seen ya bluu ,nikaona typing,akajibu poa ,nikaendelea vipi uko poa akajibu fresh Ammy,nani kakupa namba yangu? Nikamwambia dada

Basi nikaanza kuimba na kubembeleza na kusifu na kuabudu kwa kiumbe ili anielewe ,jibu alilonipa "Sorry nina mtu wangu,ulichelewa" Akaniaga akapotea online

Sikukata tamaa,saa 8 mchana siku iliyofuata naingia salon moja pale mtaani nikamuona,nikamuita,akaja,akanisalimia huku amebinua mdomo kama mkonga wa taifa.Nikamgusia akanipa majibu yale yale "Ana mtu wake,nimechelewa" Akaondoka

Siku nenda,siku njoo,kuna rafiki yangu sana alikuwa anaoa siku si nyingi,akawa ameniomba siku moja kabla ya harusi niwepo kwake pale kwenye kamati ya sherehe kuweka mambo sawa

Siku hiyo nikafika nyumbani kwa rafiki tukawa tunafanya maandalizi ya hapa na pale, bahati mbaya au mzuri nikakutana na binti wa ndugu yake jamaa ,nikamuuulizia ulizia akanambia bwana harusi ni binamu,mtoto wa mjomba wake ambaye wanashea mababu ,kichwani nikasema "Acha nifie kwenye hiki kidonda," mtoto alikuwa kisu hatari

Basi nikawa narusha verse mdogo mdogo, mwitikio ukawa unakuwa positive, haukuwa na complications sana

Ikawa imefka saa 12 jioni mtoto akawa amenielewa ile mbaya,basi jamaa akawa ameandaa disco mshenzi la mkesha hapo kwake,basi ikawa imefika saa 3 hivi usiku tukaanza kuzienda,vijana wa mtaa fully, lakin sket chache hatari ,basi mtoto kwa kuwa amenielewa akang'ang'ania kwangu mpaka saa 10 alfajiri,akawa ameniambia amechoka angepata sehemu apumzike

Basi nikasema hapa hapa sifanyi kosa,nikaita Tax nikapeleka mtoto ghetto, pale ghetto tukaoga kwanza,nikamtaka tuoge wote akasema hawezi ,ikabidi nitangulie kuoga kisha na yeye akafuata

Nikaingia kwa kitanda ,mtoto akawa anasita kuja kwa kitanda,nikamshika mkono mtoto akaja kwa kitanda

Tukawa tunapiga stories za hapa na pale ,basi nikawa namtachi kama nataka gemu,basi mtoto akawa anakataa hasa mkono ukielekea ikulu ya chamwino

Akanambia baby nikwambie kitu,nikasema "Yes nambie" akasema"Najua unahamu na mimi ila bahati mbaya siko vizuri ,nipo kwenye siku takatifu" nikagoma nikamwambia siamini acha nishike,akasema "Shika tu" Nikaingiza mkono kwa taiti nikakutana na ped basi nikamwambia "Poa nimeamini"

Baada ya dakika 10 hivi tukapitiwa usingizi ,asubuhi tukaamka tukaoga,akaandaa chai,muda kama saa 4 hivi tukawa tumejiandaa kuzama harusini

Pale harusini demu akawa sambamba na mimi kila niendapo,saa 12 jioni harusi inaingia ukumbini,demu hakukaa mbali na mimi

Ikawa kama ndoto,mara paaapu ,macho yanagongana na mtoto jirani mtaani kwangu niliyekuwa namfukuzia

Akawa amekaa si mbali na tulipokaa ,kwa nyuma yetu,nikigeuza kichwa kidogo nikimcheki jicho lipo kwetu dah nikasiiizi ..mapigo ya moyo yanaenda kasi kama vile nimefumaniwa

Huyu L wangu yeye yupo nami hajui kuwa mawazo yapo kwa mtu fulani hapo nyuma yetu

Tukawa tunakula baadae zawadi zikatolewa baadae vinywaji na mziki ,mtoto L akanidaka,tucheze,mdogo mdogo tukawa tunacheza,ila nikipenyeza jicho kwa J jirani yangu jicho lipo kwangu ,dah nikahisi ananitoa kwenye mudi ya kucheza

Tukacheza hapo kama saa 2 hivi ,L akaomba tupumzike,tukachukua viti na kukaa,L akaniomba akajisaidie toi nikamwambia poa

Kumbe alikuwa amefanya makosa makubwa sana kuniacha alone, ghafla binti anasimama mbele yangu ananishika mikono ananinyenyua tucheze,dah alikuwa J ,basi nikawa nadance mdogo mdogo,akanishika mkono akanivuta akanipeleka kona nyingine ambapo kuna watu wengi

Aliponifikisha maeneo hayo ,akaanza kulalama"Hivi Ammy ulikuwa unanipenda au kunitamani? Nikajibu kwa nini umeniuliza hivyo? Akajibu " umeniona kwenye harusi hii ukanikaushia ukawa bize na L ," Alivyomtaja jina nikashtuka,nikamuuliza *Ina maana unamfahamu?" Akasema "Ndio tumesoma naye na tumehitimu wote mwaka jana

Basi binti anaendelea kulalama" kama unanipenda mbona unanisaliti kwa L? Mi nikajibu unajua hali hiyo imetokea nilivyokuwa nakutongoza ukawa unakataa unasema una wako basi nikawa na L" akaniuliza kumbe umeanza muda na L" Nikajibu hapana,L tumefahamiana jana wala sio siku nyingi" Basi mtoto akiwa amelaza kichwa kifuani kwangu "Akaniuliza" mlisha sex na L ? Nikajibu hapana bado" akauliza "Sema kweli" nikamwambia "Huo ndo ukweli" Binti akanambia " Nimekusamehe mme wangu usije ukarudia tena kunisaliti,mi sikuwa na mtu bali nilikuwa nakutathimini kama unanipenda kweli au unanitamani,ila nilikuwa nimekuelewa" Basi nami sikumnyima mtoto furaha ,nikampa ushirikiano

Simu yangu ikawa inaita by vibration akawa anataka kujua huyo anayenipigia kila dakika ni nani? Akasema nimpe simu yangu,nami nimeishajua ni L ananipigia

Nikamwambia "Subiri nitakupa baadae" Akabinua midomo akasema" nanipa hunipi nijue"? Nikasema isiwe taabu sana nikampa,alikuwa L ndo ananitafuta,akazima sim yangu akawa ameweka kwa mkoba wake
.
Tukacheza hadi saa 8 hivi akanambia "Love nimehisi kuchoka twende kwako tupumzike" basi nikamkubalia mtoto ,nikachukua Tax hadi ghetto

Nikamuita mpangaji mwenzangu maana ndipo huwa natunzia funguo,mpangaji mwenzangu akaamka akanambia,"Ammy vipi unataka funguo,yule mwanamke uliyekuja naye jana amekuja amechukua nadhani atakuwa ndani"

Nikachoka akili,nikawaza sasa ndo nini,hapa nafanyaje kwa mfano,J ananibana"Nataka nijue huyo mwanamke aliyelala humo ndani ni nani,hivi Ammy mbona wewe ni malaya hivi? Kafungue mlango,ikabidi nigonge nikawa nimejua ni L akafungua mlango ,akawasha taa,dah alikuwa amejifunga kanga ,ghafla J akaingia ndani wakasalimiana na L maana wanafahamiana

Ghafla midomo ikaanza kuvutwa mpaka basi wakaanza kurushiana maneno,masikini najiuliza sasa hawa wanarushiana maneno humu ndani na hakuna niliyemuonja

Basi J akazira na kuondoka,Mara na L akaanza kuvaa nguo na kuchukua mkoba naye kasepa

Dah sikulamba kitu jamani_hivi ingekuwa ni wewe unafanyaje kwa hali hiyo
 

Stanboy

JF-Expert Member
Jul 4, 2013
912
1,000
Pole sana,ila ukiamua hao utapiga wote..ni rahisi sana...wafuate kila mmoja kwa wakati wake omba msamaha halafu mponde mwingine mbona easy tu..wanawake wana huruma sana..niamini mimi
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
10,454
2,000
Wanawake mna huruma sana,akiamua anaweza kuwapata wote kila mtu kwa wakati wake
Aisee kwa niaba ya wanawake wenzangu nasema hivi hatuwezi kumhurumia mtu asiyetuhurumia pia! Angeweza kumwambia ukweli mmojawapo kwamba anampenda or not ili kuepusha hilo lililotokea. πŸ˜€
 

Gastony

Member
Dec 12, 2018
25
45
Aliyemwambia ana mtu ndo ilikuwa plan yake na alihustle hata kupata namba tu...huyu mwingine kakutana naye accidentally tu...mapenzi ni magumu kuliko Physics nyieπŸ˜€πŸ˜€
Nakubali mapenzi n magumu lkn mziki wa Physics kuusoma kwa shule za kata dah,,unakosea ktk hili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom