Do we have any decision support system in tanzania ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Do we have any decision support system in tanzania ?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Dec 18, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi

  Kwenye elimu tulizosoma za IT tulifundishwa kuwa kuna aina at least tatu za Mifumo ya computer.

  1. Transaction Process System
  2. Management Information Sysstem
  3. Desion SUppport system
  Vile Vile kwenye mammbo ya management wansema Organisation inaweza ikatengwa katika makundi au ngazi tatu za kiutawala/ managament na kila ngazi ina mahitaji yake ya taarifa/data/info . Ngazi zenyewe ni

  1. Operation control-
  2. Managemnt Control.
  3. Strategic Planning

  Kwa uelewa wangu computer system nyingi zinazotumiwa kwenye taasisis mbali mbali Tanzania zipokwa ajili ya kufanya Transaction processing . Niko sahihi I guess

  Sasa Hoja/Swali/Mjadala

  • Je tanzania kuna taasisi ina mfumo Decision support system au Management Information system au hata mashirika au taasisi kubwa kama ikulu wanategeme Output ya kwenye Transastion processing system ndiyo itumike kufanya Strategic Decision ?

  • Kama Ipo Taasisi yenye DSS au Management Information system ni ipi
  Soma article hii kupata mantiki zaidi ya hoja yangu
  Types of Information Systems

  Nawasilishakwa mjadala
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Consult your class notes
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hahahaha Sir
  Wht i have writen is a theoretical knowlenge and info I acqured in class many years back.

  Now am asking to have a comment frompeople and genius Like if u ever come accross a Dession Support system in real life. I hope u know a lot than waht u ve commented .

  otherwise pass my greeting to Raj Patel .

  Thanks
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hahaa sisi wengine tulikimbia hizo major baada ya kugundua kuwa C++ ni compulsory.
   
 5. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Mkuu mtoa maada, ni kweli swali lako bado lina leta utata sana si hapa Tanzania bali katika nchi ambazo viongozi wao wanapenda siasa kuliko taaluma. Nakumbuka Obama alipo ingia madaraka ali-introduce kityu kilicho kuwa kinaitwa IT dashboard. Kilikuwa kitatoa mwelekeo wa mambo ya serikali yake kwa wanainchi wa marekani.

  Kikwazo kingine tunachokumbana nacho hapa kwetu Tanzania ni mitaala ya elimu ambayo ni static, haibadiliki kilingana na mahitaji ya kijamii na uchumi kwa ujumla. Sasa hivi operations systems zina data nyingi kupta kiasi.

  Vyuo vingi katika nchi zilizo endelea vinafundisha masters and engineering courses in decision engineering, Business intelligence, financial engineering, traffic engineering, operational research, Data analysis and data mining etc. Na hizi course mara nyingi ni professional course ZINAZO LENGA KUWA ANGA DESIONSUPPORT SYSTEMS DESIGNERS AND ENGINEERS. Inasemekana kuwa Master in Business Intelligence (MBI) WILL REPLACE THE TRADITIONAL MBA.

  Tulirudi kwenye maada yetu, Je decision support systems zina exiting hapa Bongo??. Mie binafsi naamini zipo hasa katika mashirika makubwa ya simu, Bank etc. Kwa nini aamini hivi, ni kutokana naukweli kuwa tunapo sema decision support systems ni mfumo wowote ambao unamsaidia manager kuchukua maamuzi sahihi. Pia Namini wengi mmesha sikia wakitaka Data warehouse specialist, Business intelligence specialiast ect. Hizi ni badhi ya kazi ambazo zinaonyesha watu wana DSS , labda tujadili complexity ya hizo systems. Na mara nyingi hizi systems zinatumia Transaction Systems or operational systems as a source of data.

  Nimewahi kushiriki project moja, ya kudesign desion support systems. Transaction systems ilikuwa ni systems moja inayo process millions of data per day. Kwa hiyo jamaa walikuwa wanapata shinda Sana kufanya maamuzi kwani lichukua muda mrefu kuja kupata information ambayo ni supportive kwenye decision zao. Sio we designed something that we called '' Dashboard systems"" reflecting to the reel dashboard we use when we drive vehicles, na ilibidi to sychronise data in real time (database mbili ziwe na the same data ) kwani kuna alarm nyingine zilitegemea kila data inayo ingia kwenye TS. Huu ni mfano wa dashboard yako ya gari, inatakiwa kutoa indicators zote za mambo yanayo endelea ndani ya gari lako, matatizo, na uwasaidie wengine mlio katika njia moja kuchukua maamuzi sahihi kwa mfano, ukitaka kukata kona lazima, utaona indicator na Yule mliye naye njia moja atajua nini unafanya.

  Naamini zipo desion support systems nzuri sana baadhi ya companies, kwa mfano kuna jamaa ( siwataji) wana systems ambayo inatoa alerts za warning za critical issues zote kwa sms, hizi alerts ni combination of analysed information from all sources (databases) of the company. Kwa hiyo boss unaweza toa uamuzi, au au ukabadili kabisa strategy ya business yako wakati wowote sio lazima uwe ofisini.

  These systems uses a lot of mathematics (classification, regression, operational research, probability etc to generator information (indicators) from different sources (databases) according to company's standards and objectives.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli kamanda umechambua vizuri sana hii issue kungekuwa na uwezo wa kutoa thanks 20 ningekupa Sasa tuendeleena mjadala.

  Nimepata swali hili sababu najiuliza kwa nini bado taasisi kubwa tena zenye fedha na Mifumo mizuri ya kompyuta bado unakuta zinafanya maamuzi mabovu amabyo ni obvius.

  • Je inawezekana strategic decision makers wanapata info in a form amabyo sio helpful kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi
  Mfano Najiuliza je Tume ya kubinasfisha mashirika ya umma wanayo hata simple IS ya kuwasidiia kufiltter out wawekezaji wababaishaji. Maana uzur wa system inaweza kuweka viegzo na indicators amabzoo kichwa cha binadamu kinaweza kisikumbuke wakati huo.

  Hasa hasa nilitaka kujua kama kuna any form of DSS katika govermnet parastals
   
 7. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  .

  Mkuu,nimeupenda machnago wako sana, Kwanza fikirina uelewa wa IT wa wale wazee walio shikiria vitengo. Atafikiria sa ngapi kama kuna kitu cha kumsaidia kutoa maamuzi .

  Kwanza ni wazee wanaoogopa IT kama okoma eti utawafukuzisha kazi. Nasikia kuna boss mmoja alikuwa hataki computer zinunuliwe kwani hata kuitumia alikuwa hajui, sasa alikuwa anaona noma kuaibika. sasa tutafika kweli huko. Tunatakiwa kurecycle wale wazee wote au tuwatimue, tuweke vijana wenye maono na taaluma zao ndipo mambo yatakaa vizuri.
  .
  Kama viongozi wetu wangeweka IT mbele naamini tungefanya mambo ya ajabu. Tunegeweza kuwa intelegence systems ambazo zingekudanya data toka database zote (google principle) tukapato nini position yetu na wapi twende, mshindani wetu ni nani, na ana nini ambacho sisi hatuna, na tukifanya nini, nini kitatokea.

  Angalia rwanda walivyo invest katika IT, ni mfano wa kuigwa. Lini tutakuwa na systems ambazo hata Raisi wetu atakuwa na uwezo wa kutupa jicho mara moja na kujua mwelekeo wa taifa lake kwa miezi sita ijayo,na wapi limetoka ????. Labda tuwaalike wazee hapa JF. asanteni
   
 8. scheduler

  scheduler Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili desa tosha kabisa. Lakini nipeni hatua na namna ya kudesign hizi systems.
   
 9. scheduler

  scheduler Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya ya IT inahitajika TZ
   
 10. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtazamaji tunashukuru kwa kuleta mada nzuri bila kubaki mtamazaji.

  Mr. Politician ni wimbo ambao untakiwa kupigwa kabla ya hii mada.

  Kwa nini?

  Rwanda tunayoitumia kama mfano wana nini mpaka wako pale walipo?

  Utashi wa kisiasa unahitajika sana ili kitu chochote kiwezi kustawi. Wala sio swala la DSS, katika dunia ya leo, Kama unataka mafanikio kwenye kipengele chochote cha huduma (product/service) unahitaji uongozi wa juu utoe dira na welekeo katika masuala ya utumiaji wa ICT.

  Suala siyo kwamba viongozi wanajua ICT au la bali ni utashi.
  Kuna mambo mengi unaweza kuyaeleza kama sababu za kwa nini hatuendi mbele.. lakini miye nitarudi pale kwenye mwelekeo kama taifa tunataka nini?
  Mpaka 2010 inaisha bado hatuna sera na mipango mikakati mizuri ya utumiaji wa masuala ya ICT kwenye nchi. Mipango mikakati ambayo itaelekeza taasi zozote kuzifuata ili kufika pale ambapo tunataka kufika.

  Sitapenda kulaumu watu wa ICT kwa sababu pale kufanya anayohitajika na wakuu wao.
  1. kuna masuala ya upangaji na ugawaji wa rasilimali (watu na fedha) ni tatizo lakini yanaingia kwenye sera na mipango mikakati
  2. Rushwa na ubadhiru vinatawala sana sekta hii, kwa hiyo hata ukiwa na sera nzuri na mipango bado utahitaji viongozi wakusimamia
  3. Elimu na ujuzi wa wataalamu hauendani na mahitaji ya nchi na dunia.

  Naomba niishie hapo kwa leo, ninasikitika kuona Tanzania bado hatuko tayari kuweka kwa umakini katika sekta hii. Tunaabaki kukiri tu kwamba ni muhimu kwa maendeleo lakini waulize viongozi kweli wanamaanisha wanachosema? sera na mipango mizuri iko wapi?

  Nawasilisha thumuni yangu
   
 11. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe for 100% na umenipa mwanga hapa kwamba utashi wa mambo yanavyo takiwa kwenda ni mhimu zaidi. Lakini swala la DSS kwa wakati huu ni muhimu mno tena sana , kwa nyakati tulizo nazo. Hatuta weza kwenda na wenzetu, lazima tutadanganywa.
  Ni kweli tunakiongea kitu ambacho bado tukiwa na challenge nyingi, ikiwemo nafasi ya ICT katika mipango yote inayo indeshwa na serikali.

  Mimi sioni kazi inayo fanywa na Wizara ya Sayansi na technologia hapa TZ.
   
 12. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Jamani,tunazungumzia DSS,AI,Google systems etc,wakati serikali yetu haina hata Phone Directory online ya viongozi na taasisis za serikali.
  a simple Database available online ambayo unaweza kumpata mtumishi wa umma nchini.
  Email ukituma serikalini haijibiwi.
  nashauri wataalam wa IT tuanze na fundamentals ,basic things first, like address book,e forms and services then tuanze na analysis and decision support systems hivyo vitu ni ndoto kwa serikali na taasisi zetu,
  ukienda Voda,private banks kidogo ndo unaweza kuona hizi systems lakini ukija serikalini mtaalam wa IT ni yule aneyejua kufungua PC,kuweka Operating systems and trouble shooting,ktk software and other solutions ni kwa wahindi and contractors ambao wanatoa hongo kubwa kuuza solutions za kijinga as a result hazina support yoyote ktk serikali.
  by the way mwalimu nyerere alipiga marufuku komputer in the 70's to 80's na hiyo ban on computers haijawahi kuwa lifted,hivyo komputer zinatumika kienyeji.kwani hilo tamko la kiongozi halijawahi kufutwa na viongozi waliofuatia nyuma yake.
   
 13. Supa.engineer

  Supa.engineer Member

  #13
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawapongeza wote hapa juu. hizi ndo topic za kuongea hapa.
   
 14. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Maelezo mazuri ila Decision Support Systems na Dashboard Systems ni vitu viwili tofauti kabisa licha ya kuwa yote ni sehemu ya Enterprise Systems.
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kweli wajumbe
  Ndhani Managers na Decion makers kwenye Serikali ,mashirika ya binafsi na taaasisi wajue na watambue Information system can do more than storing and prosseing information faster.
   
 16. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  upo sahihi kabisa kwani mtu kuwa na simple information system naona kesha fika. Ni ngumu kukubali maamuzi ya systems hasa katika mashirika ya uma kwani maamuzi yanafanyika kwa maslahi binafsi. Na kikwazo kikubwa naamini ni hicho kwani mikataba mingi BIBOVU tusinnge saini.

  Kwa hiyo lazima tupate viongozi wenye mitazamo chanya na walio tayari kutetea maslahi ya umma. Ni jambo la kisiasa zaidi kuliko kitaluma.
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa waliosoma IT na computer watakubaliana na somo au topi inayotwa IS development. Zipo approach/ methodology nyingi inategemea na nture ya Problem.

  Approach moja iliyokuwainatumika sana mwazoni ni SDLC(System development life cycle) unweza ku google hilo neno kwa kuanzia gonga hapa Systems Development Life Cycle - Wikipedia, the free encyclopedia

  Kuhusu swali lako namna ya kudesign au kuipmliment system itategemea na ni approach gani imetumika. Na kuchagua approach gni utumie inategemea na nature of the probblem

  Mfano Hospitali ya Muhimbili inataka kweka system ya kumanage taarifa za wagonjwa, madawa,shift za madkatari, etc

  Kwa kufuata approach ya SDLC lazima kwanza Ianze hatua ya Analysis. Hatua hii muhimu sana. bila hatua hii ni sawa nakuanza mradi bila kufanya uchambuzi yanikinifu.

  Kwneye hatua hii ndipo unaweza ujua suluiho la system yako litapatikana kwa

  • kununua already available HR commercial software ambayo labda itafanyiwa customisation ili iendanene na mahitaji
  • Kutumia inhouse power au kutengeneza prog yako
  Ingawa hii ni disciplinei IS development ni tofauti lakini principle zake zinaeendanaendana na Project management

  But msingiwa system za kisasa hautakiwi kuw tu kihifadhi kumbukumbu bali unatkiwa system iwe msaada kwa watendaji kufanya maamuzi sahihi
   
 18. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Asante sana Kwa swali lako zuri. Kwanza nimpongeze mtazamaji ( systems developement cycle) kwa kujibu swali lako vizuri na nimepata nguvu kidogo kuja kuongelea kigodo , how to design decision support systems.

  Ili kudesign any systems unatakiwa kufuata methodology ambayo itakusaidia kujua nini cha kufanya, nini utumia, mahitaji ya systems hadi kutest systems yako na kuwafundisha watumiaji. ona vizuri maelezo ya Mtazamaji na fuata link wikipedia utaelewa vizuri.

  Sasa nini tofauti ya approch katika kudesign decision systems na transaction systems? je kuna ulazima wowote wa kutumia aproch tofauti na kwanini.

  Tunapo design systems za kawaida (TS) lengo hasa inakuwa ni kuhifadhi kumbukumbu kwajili ya matumizi ya sasa naya baadaye. Ili kufanya vizuri unaweza kutumia lugha (languages) za kitaalamu kama UML, MERISE etc zinazo kuongoza nini cha kufanya hadi upate systems inayo kidhi mahitaji ya mtumiajai.

  Na hizi systems zinaweza tumiwa na mtu yoyote awe kwenye operations departement ( accounting, billing etc) au kwenye management kujua baadhi ya vitu kama statistics etc.

  Lakini ukija kwenye decision systems, hapa unatakiwa kudesign kitu kitakacho msaidia manager (pilot) kupata indicatiors za mwenendo wa kampuni yake yote ukizingatiahis/her objective, plan of actions and the whole strategy of your company. Mara nyingi utatumia data ambazo zipo kwenye transaction systems zote za company all data sources). Na hapa ndoo tunalazimika kutumia medhodology nyingine itakayo tusaidia kuapa objectives of each level, indicators, plan of actions, identification of pilots (managers) etc.

  Njia raisi ni kutumia vitu kama Balanced score card (BSC), GIMSI etc. hizi ni methodology ambazo zitakusaidia kupata vyote nilivyo kutajia hapo juu. Soma hapa utapata maelezo zaidi kuhusiana na BSC.

  Vilevile huwezi kutengeneza database kama ile ya transaction systems kweni hapa kwenye decision systems utahitaji query complex, hivyo utalazimika kuto normalize sana your database. Kinacho hitajika hapa ni kuongezeza uwezo wa kupata taarifa haraka zenye uhakika. Read here how to design a data warehouse.. asante
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhani hata viongozi wetu hawajui potentials za IS na ICT inaweza kusaidiaje katika majukumu yako. With intern how was it possible TANESCO kuingia mkataba na kampuni Hewa .Na bado hata Wizara na Ofisi ya PM hawakuweza kuugundua mapungufu hayo.
   
Loading...