Dkt. Wilbroad Slaa ndio chanzo cha migawanyiko CHADEMA

Dkt. Wilbroad Slaa ndio chanzo cha migawanyiko CHADEMA

Mtahangaika sana. Nyumba yenu ina nyufa mnahangaika na nyumba ya jirani
 
tangia lini magamba wakatoa ushauri wa kuiboresha CHADEMA? Huyo huyo dr slaa ndo kikwazo kwenu mnaangaika usiku kucha mnamsema yeye tu.
 
vijana wapewe zaidi nafasi wazee wabaki tu km washauri kwani wameshazeeka na haifai kung'ang'ania madaraka mwishoe unaharibu

wassira,tendwa,lubuva,kinana,pinda,sitta nk ni vijana? Umetumwa wewe,kachukue buku saba then zama kwenye viroba
 
Umeleta thread ili wachangie kwa maana asipomtaja Dr Slaa siku hiyo boom la buku saba halisomi. Slogani ya magamba iko hivi usipofikia wachangiaji 70 buku saba huzipati ng'oooo
 
Chilisosi,

Upotoshwaji ikiachwa kuendelea kwa muda mrefu hatimaye kuna watu wataamini ni ukweli. Naomba kujibu Mimi mwenyewe hoja zote zilizotolewa na mleta thread.

1) Ni dhahiri lengo la mleta thread ni kupotosha umma, na kujaribu kuchanganisha viongozi. Kuondolewa kwa Shonza, Mwampamba na kundi Lao ni matokeo ya tabia ya mbovu, utovu wa nidhamu, siyo tu ndani ya Chama, Bali hata ndani ya Chombo chao BAVICHA. Kamati ya kuwachunguza iliundwa Morogoro Katibu Mkuu hakuwepo. Hivyo ni wazi mleta mad a hajui au kwa makusudi tu ameamua kupotosha. Kwa Katiba ya CHADEMA namabaraza yake kuchukuliwa mtu hatua ya kinidhamu ni mchakato mrefu na unapitia vikao mbalimbali. Maswala ya nidhamu yanasimamiwa na Katiba ya Chama Toleo la 2006 Ibara za 5.4(1-4); Kukoma kwa uongozi ( Ibara 6.3.4(b na c na e). Mamlaka za Nidhamu zinatajwa Ibara ya 6.3.6 pamoja na Kanuni Mbalimbali za Chama nazo ziko ndani ya Kitabu cha Katiba. Mto mada au hajasoma, au ni mbumbumbu tu mwenye kutumika au mpotoshaji tu. Kama anavyosema mleta mada ni kweli, Dr Slaa anaweza kuamua tu, basi Dr Slaa ni sawa na Mungu. CHADEMA ni Kati ya vyama vichache vinavyofanya vikao vya kikatiba, siyo tu kwa mujibu wa Katiba na Mara nyingi kwa kutumia mamlaka ya vikao vya dharura. Kauli ya mleta mada ni matusi kwa wanachadema wote na hasa Kamati Kuu na Baraza Kuu, ambazo indigo vyombo vya maamuzi.

2)Barua ya Siri kuvuja. Hiki ni kichekesho. Ebu to a hadharani barua iliyovuja. Kwanza barua hiyo ikiwasilishwa kwa Katibu Mkuu kwa Dispatch ya Tarehe ngapi na nani kwa mujibu wa dispatch kaipokea. Hiyo itaonyesha Kama kweli barua hiyo ya siri ikiwasilishwa under tight confidential system. Pili, weka barua hiyo hadharani ili WanaJF waone Kama in a mhuri wa siri. na Kama imewekwa muhuri kwa siri imeandikwa kwa Katibu Mkuu peke yake au imenskiliwa kwa wengine. Iwapo imenakiliwa kwa watu wengine, kwanini hoja iwe imefuja toka kwa Dr Slaa. Barua iliyoko kwa Ofisi ya Katibu Mkuu imenakiliwa kwa watu au vyombo vinginevyo pia. Huhitaji kuwa na elimu ya darasa la kwanza kujua kuwa jambo lililopelekwa kwa watu wengi, huwezi kusema tu fulani ndiye kavujisha, labda uwe tu na sababu zako binafsi kusema hilo.

3) Hoja ya Profesa Baregu kutakiwa kujitoa kwenye Tume.Kama Source ya Gazeti basi nafikiri unasababu zote kumwuliza Prof. Baregu, nini hasa tulizungumza, na kama kuna wakati wowote alitakiwa ajitoe. Aidha, mwulize Profe. baregu Kama hayo tuliyozungumza ni ya Dr Slaa au ni utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya maamuzi. No research no right to speak. Rafiki yangu kana unaandika kwa dhamira njema chunguza kwanza nafsi yako, na uwe na hofu ya Mungu. Kuwapotosha Watanzania kutakuwa na gharama kubwa kwa vile kuna siku uzalendo utatushinda Kama ilivyo Leo, na nitatetea chama na procedures za chama. CHADEMA inaongozwa kwa Katiba, Kanuni na Taratibu, ni wazi Dr Slaa asingeweza kwa utashi wake kutoa amri yeyote kwa mtu yeyote yule.

4) Ujio wa Obama na kauli mbalimbali zilizotoka nimejibu Leo asubuhi. Sijakagua, labda Mods awe ameondoa majibu yangu. Vinginevyo siwezi kujibu hoja hiyo hiyo, tena ya kipuuzi tu na au ya ki propaganda.

WanaJF na wote wenye mapenzi mema. Narudia tena hoja za aina hii zany lengo la ki propaganda zisitupotezee muda, na ndiyo maana Mara nyingi sizijibu. Mkiona nimepuuza hoja mjue kuwa nimepuuza kwa kuwa ni ya ovyo. Wapuuzeni wahusika hao Kama ambavyo tupuuze hoja zao.




Jaribuni sometimes kujibu hoja na sio matusi
 
Chilisosi,

Upotoshwaji ikiachwa kuendelea kwa muda mrefu hatimaye kuna watu wataamini ni ukweli. Naomba kujibu Mimi mwenyewe hoja zote zilizotolewa na mleta thread......
Heshima yako Dr,

Nashukuru kwa kutumia muda wako kujibu hoja kama inavyotakiwa.

Pamoja na kuwa sikubaliani na majibu yako lakini at least nimefarijika kuona unatoa mfano bora kwa makamanda wako namna ya kujibu maswali kiungwana na sio kutumia lugha ya matusi kama tulivyozoea kuona majibu ya wanachadema hapa jamvini pale wakitupiwa hoja ambayo inawagusa.

I hope makamanda watafuata mfano wako na nimekuwa kila kukicha nikiwaambia kuwa kama ni umaarufu utaupata kutokana na hoja zako kisiasa na sio vurugu, maandamano yasiyo na vibali au matusi

AHSANTE.
 
....Upotoshwaji ikiachwa kuendelea kwa muda mrefu hatimaye kuna watu wataamini ni ukweli. Naomba kujibu Mimi mwenyewe hoja zote zilizotolewa na mleta thread......

Dr Slaa vipi na ile hoja ya mzee Mwanakijiji? kwa maelezo yako ni kwamba nayo ni ya kipuuzi maana hukujibu chochote kwenye hoja yake. Ingawa kuna maeneo yalihitaji ufafanuzi wako wewe kama katibu mkuu wa chama.
 
Dr.
Unamoyo sana kujibu hoja za buk 7...ukiwaendekeza hawa watakuweka busy hawakosi la kusema maana ndo ajira yao.
 
Tusijichanganye kuwajibu wachumia tumbo, tuwapuuze! Wakiandika uzi wao tusichangie, that's the only solution!
 
DR SLAA NA UTENDAJI KAZI
KATIBU MKUU wa chadema DK WILBROD SLAA ndio chanzo cha migawanyiko chadema moja alichangia sana kuondoka kwa makamanda shonza na mwampamba,pili katika ofisi yake barua za siri zimekua zikivuja mfano ni barua ya zito ambayo tuliisoma hp mtandaoni,tatu kumshinikiza prof baregu ajitoe katika tume ya katiba bila kutoa 7bu za kueleweka na kusababisha mjadala mkubwa ndani na nje ya chama,tano kukurupuka na kusema chadema hawatashiriki ujio wa obama kisha tunamwona mwenyekiti wake akiwa ikulu jambo hili limeleta mkanganyiko na migawanyiko source akiwa dr SLAA.NAFIKIRI IMEFIKA WAKATI CHADEMA WAKATAFUTA MTENDAJI MKUU HUYU AKAWA MSTAAFU KWA SASA KWANI MGEMA AKISIFIWA TEMBO HULITIA MAJI

kugawanyike wagawanyike wao
kuumia uumie wewe
kushauri ushauri wewe..
pole utaambulia
lolote hapa..
pia hebu jaribu kusoma comment zote kwenye huu uzi
alafu ufanye tathmini ni wangapi wanaokuunga mkono!
shtuka mkuu hapa haya mambo mnayoyaleta hapa hayaipungizii CDM kitu chochote kile
Zaidi mnaongeza chuki dhidi ya CCM

Coz the more u write the more people hate!!

tumieni mbinu nyingine hii imeshawashinda#
 
vijana wapewe zaidi nafasi wazee wabaki tu km washauri kwani wameshazeeka na haifai kung'ang'ania madaraka mwishoe unaharibu

Vijana gani unamaanisha?Wale waliokwapua simu?Heri wazee kuliko vijana wanaoshiriki katika vitendo vya aibu kama wizi na kujigamba kwa ushirikina.Ni fedheha kwa vijana.Dunia inaendeshwa kisayansi mzee,hakuna ujanja ujanja
 
Dr.
Unamoyo sana kujibu hoja za buk 7...ukiwaendekeza hawa watakuweka busy hawakosi la kusema maana ndo ajira yao.
Ana jibu kwa sababu hoja imewekwa kistaarabu na kiungwana bila lugha chafu ya matusi.

Hata nyie mkijirekebisha tabia na kuacha kuporomosha matrusi viongozi wa chama tawala watakuwa wanakuja kuwajibu hoja zenu

JITAMBUE
 
Tusijichanganye kuwajibu wachumia tumbo, tuwapuuze! Wakiandika uzi wao tusichangie, that's the only solution!

Unazuia watu kuchangia? teh teh teh.

Hivi umekuja humu JF kutoa 'solution' kwa members? ungekuwa Mod, ungekuwa rais, sijui ingekuwaje?

Jifunzeni kukubali hoja za wenzenu hata kama zina kera, ndio demokrasia na siasa yenye ushindani ilivyo.
 
Vijana gani unamaanisha?Wale waliokwapua simu?Heri wazee kuliko vijana wanaoshiriki katika vitendo vya aibu kama wizi na kujigamba kwa ushirikina.Ni fedheha kwa vijana.Dunia inaendeshwa kisayansi mzee,hakuna ujanja ujanja
Sayansi ipi unayoizungumzia?? Ya kutembea na sumu hadi bar ukivizia kuwalisha wenzio? Kumwagia watu tindikali?? Poor u.
 
wewe unayemwambia mwenzio akachukue posho Lumumba hebu tuambie wewe unachukua Bilicanas au Freemason Chagawood Ltd? funguka. inaelekea humu mnalipwa kwa kuandika utumbo
Mnamwogopa..anawapa jambajamba 2015.....kachukue posho lumumba umemaliza kazi yako.
 
Una uwezo mdogo sana kufanya propaganda, ukijumlisha na hao uliowataja ambao kikweli wangekuwa bado cdm ni kama mzigo wa misumari.
Lete hoja za msingi,
-je anasababisha ufaulu wa wanafuni kushuka zaidi ya 50%?
-je anasaini mikataba ya madini yetu kwa manufaaa ya wageni?
-je amesafiri zaidi ya mara 500 nje ya nchi? ampiga picha na Bolt? Amepiga picha akibembea? Amepiga picha na kombe la dunia?
-JE, amejenga kasri chalinze?
-Je, ana hisa 45% tanzanite one?
-je, anasababisha hospitali kuu hasa za rufaa kutokuwa na vipimo?
-je, anasabibisha mfumuko wa bei nchini?
-je, anasababisha watu kutolewa kucha, meno na macho kisha kutumbukizwa kisimani?
-je, msafara wake unatumia magari 20 ya kifahari wakati wananchi wake waliowengi hawamudu mlo mmoja?
-je, ana mtoto muuza unga?
-je, anahusika katika manunuzi ya magari ya kifahari yanayotumiwa na serikali?
-je, ameamuru polisi wanaosafirisha bangi na kupiga chenji kota ya cocaine kwa unga wa mahindi, wachukue hatua mikononi kupiga raia?
-je, ni kweli Dr Slaa huku akiwa hamjui mwenye Richomond, Dowans.....sasa Symbion walimlipa nani wakati wakinunua huo mtambo?
-Je, kupanda kwa umeme kisirisiri na mbali ya kupatikana kwa gesi, slaa anahusika?
-Badala ya kuaimarisha bandari iliyopo, kwanini ianzishwe nyingine tena mkoa...?
-je, ni Dr Slaa anasababisha raia wa nchi hii kunyang'anywa ardhi yao na kupewa waarabu? kwani ni dr slaa aliyehongwa suti?
-Tumesafisha jiji letu ili mgeni (obama) akija akute mji msafi...lakini tumesahau kigezo kikubwa wanachotumia wamarekani kuujua mji na nchi chafu kuwa ni KUNGURU...je ni Slaa aliyewaleta hao kunguru?

Yoote hayo ni mizigo kwa wananchi ambapo, wahusika hamuwataji....mnawafumbia macho....matokeo yake mnafanya mfanyayo kwakuwa mnalipwa....kwakua matumbo yenu yanashibishwa na hao wanao sababisha mizigo kwa wananchi!
 
Mleta mada, ulijitambulisha kwamba wewe ni mzalendo na huna chama. Ila michango yako iliyofuata ndo inanipa wasiwasi kwamba either wewe ni mmojawapo wa viongozi wa chama flani au ni njaa ya hzo sijui elfu saba wanazosemaga vijana wa Bavicha humu ndani.
 
Back
Top Bottom