Lucy Lameck alifariki baada ya kuugua muda mrefu. Alilazwa muda mrefu tu pale hospitali ya KCMC, lakini kwa hakika sifahamu ni nini kilichokuwa kikimsumbua.
Kithuku,
Huyu Lucy Lameck tena ni nani mie naona nimepita kapa hapo!
Maana kuna "taarifa" kwamba alikuwa na "uhusiano" na Rais wetu wa kwanza .... ??!! ... sijui kama naweza ku-connect dots hapa.
Taarifa za "redio mbao" mbona zilimpakazia Nyerere na wengi tu, wapo waliodai ati alikuwa anamchukua Bibi Titi (ujana wake alikuwa na umbo lile la kimanyema hasa, tukunyema mpaka chini! Japo sijui kabila lake), ukiuliza ushahidi unaoneshwa picha ya Nyerere akicheza naye muziki kwenye party ya kusherehekea uhuru 1961! Wengine wakamsema na Secretary wake mzungu Joan Wickens, lakini yote hayo hayakuwahi kuthibitishwa beyond rumours! Na yalikuwa yanasemwa sambamba na yale mautani aliyokuwa anasemwa nayo mzee Kawawa, na ile "miujiza" ya kifimbo cha Nyerere, ambayo yote sidhani kama kuna lenye ukweli.
Mkuu Field Marshall ES Heshima, na wengineo pia heshima mbele. Huu mjadala nami umenifanya nimjue huyu Dr. Kleruu, na zaidi Mwamwindi ambaye nilikuwa sijui haya. Sasa nataka Mkuu FM ES hapo unapozungumzia Mwalimu Nyerere anajutia kifo kimoja alichoidhinisha, huenda hapa tunacheza na lugha, katika vifo 10 (kama nadhani Kuhani alipoonesha majibu bungeni, vilivyotekelezwa awamu ya kwanza), huenda ni hicho cha Mwamwindi tu ndio anaona hakuwa fare. Lakini vile tisa alivyoviafiki huenda anaona kulikuwa hakuna tatizo. Ni hayo tu wakuu.
Mfumwa,
Nashukuru umekuja na macho yaliyo na nguvu na kuliona hilo kuwa Nyerere alijutia hukumu moja ya kifo aliyoidhinisha kwa kuwa dhamira yake ilimsuta. Hao tisa wengine wala hakujigusa na nakumbuka vizuri kuna Mhindi ambaye alinyongwa kwa kumuua mkewe kwa makusudi ili apate bima ya maisha! Huyu Mdosi, inasemekana Nyerere wala hakusubiri muda kutafakari maana huyo mke alikuwa ama wa pili au watatu kufa kwenye "ajali"!
Lucy Lameck alifariki baada ya kuugua muda mrefu. Alilazwa muda mrefu tu pale hospitali ya KCMC, lakini kwa hakika sifahamu ni nini kilichokuwa kikimsumbua.
Mwalimu Nyerere anajutia kifo kimoja alichoidhinisha, huenda hapa tunacheza na lugha, katika vifo 10 (kama nadhani Kuhani alipoonesha majibu bungeni, vilivyotekelezwa awamu ya kwanza), huenda ni hicho cha Mwamwindi tu ndio anaona hakuwa fare. Lakini vile tisa alivyoviafiki huenda anaona kulikuwa hakuna tatizo. Ni hayo tu wakuu.
... wakati umefika sasa tumuache Mwalimu apumzike!
Na wakati wa kumuacha Mkapa apumzike umefika?
Hii ya tukunyema kazi kweli kweli sina mbavu tena hapa, LOL
.
Kuhusu vijiji vya ujamaa kwa kweli huu ulikuwa ni UKOMBOZI mkubwa kwa tulio wengi. Tuliweza kupelekwa shule baada kutolewa huko porini tulikokuwa tunaishi, kwa mara ya kwanza tulitibiwa kwenye zahanati; UTANZANIA wetu ulijengeka maradufu; na hadi leo tunaishi kwenye vijiji hivi.
Mheshimiwa WildCard
Hivyo vijiji vya ujamaa vilivyokusaidia kusoma vilivyoko hadi leo viko wapi,mkoa gani wilaya gani na vinaitwaje? Na vilikusaidia kusoma hadi darasa la ngapi?
FMES is right...ni kweli kulikuwa na hizo hukumu,lakini mpaka Mwalimu anatoka madarakani hayo ma file yalikuwa bado yako kwenye desk lake bila ya signature yake.Aliye sign alikuwa Mwinyi,fuatilieni jamani
Kwani nae amefariki?