PreGE2025 Dkt. Tulia azindua gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mwakibete, jijini Mbeya

PreGE2025 Dkt. Tulia azindua gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mwakibete, jijini Mbeya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 19 Aprili 2025, amezindua gari la kubebea wagonjwa (ambulance) lililotolewa na Serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mwakibete, jijini Mbeya. Uzinduzi huo unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wakati kwa wakazi wa Jiji hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Tulia amewashukuru Viongozi wa Serikali kwa kuendelea kupeleka huduma muhimu kwa wananchi, huku akiwataka wakazi wa Jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kumpigia kura kwa kishindo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ishara ya kutambua na kuunga mkono kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika kuboresha maisha ya Watanzania.
 
1745061051680.gif
 
Huyu mhe. Tulia Ackson anapiga sana kazi. Akiacha uchawa na akafuata katiba inavyotaka sioni wa kumuondoa hapo mbeya.
 
Hata wasomi wetu hawaishiwi upumbavu, yaani spika anajitangaza kuzindua ambulance!
 
Back
Top Bottom