Dkt. Nyantahe: Mabadiliko ya masoko yameua Viwanda

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Viwanda vingi nchini vimekufa na kuacha kuendelea kuzalisha na kuuza mali kutokana na ubadilikaji wa masoko ya nje, ukosefu wa mali ghafi na sera zetu nyingi zinazotungwa hazizingatii kuinua viwanda.

Dr-Samuel-Nyantahe.jpg

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe wakati akizungumzia dhamira ya serikali ya awamu ya tano kutaka kuvichukua viwanda ambavyo havizalishi kwa muda mrefu hivyo wameiomba serikali iweke dhamira na sera itakayowasaidia wazalishaji kuzalisha na kuuza.

Amesema sera hiyo iwe endelevu na isaidie kulinda viwanda vilivyopo na kuhamasisha watu waingie katika uzalishaji ambao utaweza kupunguza bidhaa nyingi kutoka nje na kuon geza pato la taifa.

Aidha amewataka wazalishaji wa bidhaa nchini kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye viwango na ubora unaotambulika kimataifa.
 
Tatizo la Viwanda vyetu ambavyo vingi vilikuwa vya Umma viliendeshwa kisiasa:

  1. Teknoliojia yake ni ya zamani sana ... ambayo inaajiri watu wengi sana. Kwa mtindo huu huwezi kuwa comptetitive
  2. Management yake ilikuwa ya kisiasa-
  3. Corporate gorvance ilikuwa zero- wizi, uvivu,
  4. Lack of investment plan
  5. Hata leo hii viwanda kama Urafiki, tanneries, General tyre- vikirudishwa serikalini haviwezi kuwa competitive kwa sababu technolojia ni ya kizamani sana
 
Pia Rushwa za ngono, wasomi feki wanaomiliki vyeti lakini kichwani hawana Taaluma huku Ufujaji na Ufisadi ikiwa ni sifa kuu ya kuwa kiongozi kwenye viwanda.
 
Kuhimiza maendeleo ya viwanda si lazima mtu amiliki kiwanda kwani kama hamiliki kiwanda hana nafasi ya kutoa ushauri?
hivii unajua cheo chake au umekurupuka kutoka usingizini. Mtu anaweza kuwa nahodha wa timu halafu asiwe mchezaji?
 
Kule Tanga, moshi, morogoro mpaka kilosa kuna viwanda vingi vilikufa na watu wakabeba mitambo Magari na vifaa vingine wakauza hakuna wa kuthubutu kuwauliza hadi leo na wengine wamegeuza matumizi ya viwanda na kuvifanya kuwa maghala ya mizigo yao na kukodishia watu ama kuwapangisha wengine.
 
hivii unajua cheo chake au umekurupuka kutoka usingizini. Mtu anaweza kuwa nahodha wa timu halafu asiwe mchezaji?
Huo mfano wako hauendani na kinacheongelewa ww utakuwa upo Tarime unavuta Bangi au kuuza huko kenya, unahodha wa timu na viwanda ni vitu viwili tofauti, hivi wazili anapohimiza maendeleo kwa wafanyabiashara kwani yeye lazima awe mfanyabiashara? Kuongoza Taasisi yeyote ya biashara si lazima na uwe na kiwanda na hata kama ana kiwanda Sidhani kama anapaswa akueleze kiwanda chake kipo wapi, Acha kukariri mifano isiyoendana na mada.
 
Kw
Tanzania ya viwanda ni mtoto aliyefia tumboni.
kweli mkuu maana awamu ya kwanza ilikuwa na viwanda vingi sana. Awamu ya mwinyi ikavimaliza na awamu ya mkapa ikaviuza na awamu ya JK haikujali viwanda ndipo wengi wakavigeuza maghala na matumizi Mengineyo huku wengi wakivitelekeza kabsa, wale wote waliosababisha haya wanapaswa wasakwe wakamatwe washitakiwe ili iwe fundisho.
 
Viwanda vingi nchini vimekufa na kuacha kuendelea kuzalisha na kuuza mali kutokana na ubadilikaji wa masoko ya nje, ukosefu wa mali ghafi na sera zetu nyingi zinazotungwa hazizingatii kuinua viwanda.

View attachment 317059
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe wakati akizungumzia dhamira ya serikali ya awamu ya tano kutaka kuvichukua viwanda ambavyo havizalishi kwa muda mrefu hivyo wameiomba serikali iweke dhamira na sera itakayowasaidia wazalishaji kuzalisha na kuuza.

Amesema sera hiyo iwe endelevu na isaidie kulinda viwanda vilivyopo na kuhamasisha watu waingie katika uzalishaji ambao utaweza kupunguza bidhaa nyingi kutoka nje na kuon geza pato la taifa.

Aidha amewataka wazalishaji wa bidhaa nchini kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye viwango na ubora unaotambulika kimataifa.
Walitelekeza viwanda wasakwe washitakiwe kwa kuisababishia Nchi hasara.
 
Back
Top Bottom